Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 6 Sha'aban 1445 | Na: 1445 / 22 |
M. Ijumaa, 16 Februari 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nini Kinachotofautisha Uteuzi wa bin Mubarak kutoka kwa bin Abdul Malik katika Serikali ya Aden?!
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 6/2/2024, uamuzi ulitolewa na Baraza la Rais mjini Aden kumteua Ahmed Awad bin Mubarak kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Aden, akimrithi Maeen Abdul Malik. Uteuzi wa Ahmed bin Mubarak umekuja baada ya Baraza la Rais kufeli katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake kuafikiana juu ya idadi ya wagombea wa nafasi ya uwaziri.
Kubadilisha sura ili kuwabangaranisha watu ni hulka ya ubepari. Wakati matumaini ya watu yakiwa yamefifia kutokana na maisha magumu kutokana na kuzorota kabisa kwa huduma, huku kukiwa na hali ya kutoridhika na serikali ya Maeen Abdul Malik, Ahmed bin Mubarak anateuliwa kuwa mrithi wake huku mawaziri wa serikali wakisalia kwenye nyadhifa zao, kana kwamba mabadiliko haya ndiyo wanayoyatafuta watu wa Yemen, na ndiyo yatakayoondoa ufisadi na kufikia maisha ya staha ambayo yamekuwa ni ndoto chini ya watawala hawa vibaraka!!
Mabadiliko haya yanathibitisha kufilisika kwa kituo cha siasa za wakala nchini, kwani yanawapata tu watu ambao ni walaji, watu waliojaribu ufisadi wao na kuonja majanga ya utawala wao, chini ya mfumo huu wa kibepari potofu. Hata yakileta mfumo wa kisiasa ulio safi zaidi, hayawezi kurekebisha hali kwa sababu ufisadi ndio mzizi wa mfumo huu. Tatizo msingi halipo kwenye ufisadi wa viongozi pekee, bali mzizi wa tatizo ni mfumo wa kibepari ambao tunatawaliwa nao. Bila kujali shakhsiya ya Waziri Mkuu, uharibifu wa uchumi wetu hautakoma maadamu mfumo huu ungalipo.
Mgeni huyu atasema yale yale aliyosema mtangulizi wake, na atataka kuwahakikishia watu uongo kuwa nchi inapitia kipindi kigumu, na atajaribu kutatua matatizo yake!! Watu wamesikia uwongo kama huo katika miaka iliyopita. Watu wa Yemen lazima wasidanganywe na ahadi za uwongo na uwongo uliochosha. Bin Mubarak na bin Abdul Malik ni pande mbili za sarafu moja.
Watu wa Yemen lazima wajue kwamba mabadiliko haya ni ubadilishaji kibaraka mmoja kwa kibaraka mwengine. Wakati wao huko Aden wanakanusha kuwepo kwa uingiliaji kutoka nje katika uteuzi wa Ahmed Awad bin Mubarak, wanakiri kwamba vyombo vya kimataifa vilitia shinikizo kuharakisha mabadiliko ya mawaziri, na kwamba Marekani na Uingereza zilitoa ahadi kwa bin Mubarak kutoa msaada wa ukarimu kwa serikali yake kwenye faili zenye miiba.
Mzozo mkubwa na unaoendelea wa kimataifa juu ya Yemen kwa jumla na haswa kusini mwa nchi hiyo ndiyo sababu halisi ya kuchafuka kwa maisha nchini Yemen. Mzozo huu ni kati ya Uingereza (ukoloni mkongwe), ambayo haijaondoka Yemen Kusini tangu ilipoiacha kijeshi mnamo 1967, ikidumisha ushawishi wake wa kisiasa ndani yake hadi sasa, anayeitumikia kikanda ni Sultan wa Imirati Zayed bin Sultan na wanawe, Marekani (ukoloni mpya), ambayo inataka kuchukua nafasi ya ukoloni mkongwe kwa ushawishi wake wa kisiasa, kwa msaada wa Salman bin Abdulaziz na mwanawe Muhammad.
Tatizo haliko kwa watu na ubadilishwaji wao, bali katika mfumo wa utawala ambao nchi hizo mbili zinazopigana zina nia ya kuuhifadhi, na kuzuia kurudi kwa Uislamu madarakani kwa nguvu zao zote. Iwapo watu wa Yemen wanataka mabadiliko ya kweli, waondoe mfumo wa utawala wa sasa kutoka kwenye mizizi yake na kuubadilisha kwa Khilafah Rashida ya pili kwenye kwa njia ya Utume. Hizb ut Tahrir inautaka Umma wa Kiislamu kuung’oa mfumo huu wa kibepari kutoka katika mizizi yake na kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambapo watu watafurahia maisha ambayo wakaazi wa ardhini na mbinguni wanaridhika nayo.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |