Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  14 Sha'aban 1445 Na: HTY- 1445 / 24
M.  Jumamosi, 24 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mahouthi Waainishwa kama Magaidi na Trump na Biden
(Imetafsiriwa)

Mnamo Februari 16, 2024, uainishaji wa kundi la Houthi kama Kundi Lilioundwa Maalum kwa Ugaidi Ulimwenguni (SDGT) ulianza kutumika. Je, ni faida zipi Marekani inazopata kutokana na uainishaji huu, na ni zipi athari zake kwa kundi la Houthi baada ya miaka kumi tangu kuingia kwao Sana’a?

Kwanza, inafaa kuzingatia kwamba uainishaji wa Rais wa sasa wa Marekani Joseph Biden wa Mahouthi mnamo Januari 17, 2024, kama "shirika maalum la kigaidi la ulimwengu" unatofautiana sana na uainishaji wa mtangulizi wake Donald Trump wa kundi hilo mnamo Januari 11, 2021 kama "shirika la kigaidi la kigeni". Uainishaji wa Biden hauwanyimi Mahouthis mtiririko wa kuendelea wa misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na chakula na mafuta, wala haizuii makampuni ya meli, benki, na mashirika ya Magharibi kufikia na kuamiliana nao. Wakati huo huo, uainishaji wa Trump wa Mahouthi kama "shirika la kigeni la kigaidi" ulizuia usambazaji wa misaada kwa Yemen, kuziweka mbali kampuni za usafirishaji wa meli, benki na mashirika kutokana na kushirikiana nao, uliweka marufuku ya usafiri kwa wanachama wa kundi hilo, na kuruhusu vikwazo kwa wale wanaotoa "msaada wa nyenzo." kwao, kwa mujibu wa Wizara ya Kigeni ya Marekani. Kwa ujumla, uainishaji wa utawala wa Biden wa Mahouthi sio mkali kuliko ule wa Trump.

Utawala wa Biden, kwa kukiri kwamba uainishaji huu uliwekwa, ili usiathiri vibaya Mahouthi ambao hawawezi kustahamili mateso yanayoongezeka ya watu ikiwa msaada kwa Yemen utakatwa, umeruhusu pengo la siku 30 kati ya kupitishwa kwa sheria na utekelezaji wake.

Vile vile, utawala wa Trump, ulioingia madarakani mwaka wa 2017, ulishughulikia Mahouthi nje ya mfumo wa ugaidi katika miaka yake minne, na uainishaji wao kama magaidi ulileta kikwazo kwa utawala wa Biden, ambao uliibatilisha mara moja baada ya kuingia ikulu ya White House mnamo Februari 16, 2021. Kwa hivyo, uainishaji wa Mahouthi kama magaidi ulianza 2021 na hauhusiani moja kwa moja na mashambulizi ya meli katika Bahari Nyekundu, kwani kuna miaka miwili kamili kati yake na uainishaji wa Biden.

Uainishaji wa Mahouthi kama magaidi ni chombo kinachotumiwa na tawala zilizofuatana katika Ikulu ya White House kujionyesha kama wanapambana na ugaidi, na hivyo kupunguza aibu ya umma ndani na kimataifa kwa miaka kuhusu kundi ambalo halikutumia mchakato wa uchaguzi kupata mamlaka. Ili kuwafanya Mahouthi watii Marekani zaidi chini ya shinikizo linaloelekezwa kwao, mali zao za kifedha zimefungiwa, vikwazo vya kifedha vinawekwa, visa zinanyimwa ili wao kuingia Marekani, na wamegawanywa baina ya wahafidhina wa mbali na wanamageuzi wa karibu. Hii inaonyesha kwamba Marekani imeshughulika na Mahouthi na kutoa msaada wa kifedha na vifaa kwa taasisi zao kwa miaka mingi. Wengine wanaowaunga mkono wanatishika kujihusisha na siasa za Marekani badala ya kuzipinga. Hivyo basi, sheria ya Washington inayowaainisha Mahouthi kuwa ni kundi la kigaidi inalenga kuwafanya wafuate waziwazi sera fulani.

Hali inabadilika na kugeuka kwa haraka. Mwanzoni mwa milenia ya sasa, Mahouthi walishiriki katika "vita dhidi ya ugaidi" na waliamini kuwa kuwaita wengine miongoni mwa Waislamu kama magaidi kungewalinda dhidi ya kuainishwa chini ya neno hili. Leo wanatajwa kuwa ni magaidi wenyewe! Je, watu wa imani wametambua kwamba Marekani inalenga hadhara ya Uislamu, na kuuona kama tishio kwa hadhara yake fisidifu ya kibepari? Marekani inaunyanyapaa Uislamu kama ugaidi wa kuupiga vita na kuzuia mradi wake wa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume usitokee kwenye jukwaa la dunia, kwa kupendelea utawala wake wa kibepari na kuenezwa kote duniani. Mwenyezi Mungu anasema;

[قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ]

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Aal-i-Imran:118]. Tunafafanua matukio haya ili watu waelewe njama zilizopangwa dhidi ya Ummah huu na jinsi makafiri wa Magharibi wanavyotumia mbinu na vitendo ili kuficha uhaini wa watawala wetu, wanaoendelea kututawala kupitia jamaa zetu ambao wameuza dini yao, wakidhani wanafanya vyema! Ufahamu wa kisiasa na kutazama matukio kwa mtazamo wa imani hulinda Ummah kutokana na makosa na kutumbukia katika mitego ya makafiri. Hizb ut Tahrir inatoa wito kwa Ummah kwa suluhisho msingi la kutoka kwenye giza la ukoloni na kuingia kwenye nuru ya Uislamu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu