Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  29 Safar 1446 Na: HTY- 1446 / 04
M.  Jumanne, 03 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa kukosekana kwa Mradi wa Kiuchumi wa Mahouthi

Kilimo cha Mkataba: Tishio Linalokaribia Kuwasagasaga Wakulima, Kuimarisha Udhibiti wa FAO, na Kushindwa Kufikia Kujitosheleza katika Nafaka nchini Yemen
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatatu, Agosti 26, 2024, Waziri wa Kilimo, Uvuvi, na Rasilimali za Maji, Dkt. Ridwan Al-Rubai, alifanya mkutano wa mashauriano na wawakilishi wa vyama vya ushirika wa kilimo na wataalam maalum ili kujadili dori muhimu ambayo kilimo cha mkataba kinacheza kama njia madhubuti na ya hali ya juu ya unadi wa bidhaa za kilimo.

Hivi ndivyo Waziri wa Kilimo alivyozindua mpango wa mabadiliko na maendeleo katika wizara yake.Wakati huo huo, Waziri Mkuu Ahmed Ghalib Al-Rahwi alisherehekea mavuno ya mazao ya biashara - makudhumani, tufaha, zabibu na tende - mnamo Jumamosi, Agosti 24, 2024, kwa kukosekana kwa mazao ya kimkakati. Sasa tuko katika mwezi wa kwanza wa Wizara wa Mabadiliko na Maendeleo!

Kilimo cha mkataba ni neno lililoanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), ambalo linafafanua kama “uzalishaji wa kilimo unaofanywa kwa mujibu wa makubaliano kati ya mnunuzi na wakulima, ambapo masharti ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa moja au zaidi za kilimo zimedhamiriwa. Bidhaa hizo lazima zifikie viwango vya ubora vilivyoainishwa na mnunuzi na ziwasilishwe kwa wakati uliowekwa na mnunuzi. Badali yake, mnunuzi anajitolea kununua bidhaa, na katika hali nyingine, kusaidia uzalishaji kwa kutoa pembejeo za kilimo, kuandaa ardhi, na kutoa ushauri wa kiufundi.” Je, ni wataalamu gani waliobobea wanaoshiriki katika mkutano huo? Je, wao sio wawakilishi wa FAO, ambayo inakikamata kilimo cha Yemen kwa kutekeleza miradi yake na kuelekeza sera yake ya kilimo kupitia kuajiri wasimamizi wa Wizara ya Kilimo?

Kilimo cha mkataba hakifanikiwi kujitosheleza, kama wengine wanavyofikiri, bali kinaimarisha udhibiti wa nje kupitia FAO na taasisi za fedha za kimataifa. Udhibiti wa FAO unakuja kwa njia ya kutoa pembejeo za kilimo - mbegu zilizobadilishwa vinasaba kutoka nje ya Yemen - na kutoa ushauri wa kitaalamu, kisha kuelekeza mazao ya kilimo kwa kugawa msimu wa kilimo kwa mazao katika awamu tatu: mapema, kuu na ya kuchelewa, kwa kisingizio cha kutoa mazao mapya ya kilimo kwenye masoko!

Kitendo hiki ni kinyume na sheria ya Kiislamu (Shariah) kwa njia kadhaa. Kwanza, inahusisha mkataba kati ya pande tatu, ambapo kazi inalenga upande mmoja, huku upande wa pili unanunua mazao kutoka kwa wa kwanza, na wa tatu hutoa mikopo ya riba. Pili, inahusisha kuuza kile ambacho mtu hana, kwani huuza zao la kilimo kwa wafanyibiashara kabla hata halijapandwa. Tatu, inajihusisha na mikopo yenye riba ya muda mfupi inayotolewa na benki kwa wakulima.

Miaka minne imepita tangu kuanza kwa kilimo cha mkataba nchini Yemen, na utegemezi wetu wa chakula kutoka nje ya nchi unaendelea. Utoshelevu haujapatikana na hautapatikana kwa njia hiyo, kwani hili linaweza kutimizwa tu kwa kukataa riba na kuwafukuza wakoloni wanaotoka nje ya mipaka na mawazo yao yenye madhara na yasiyofaa, kama vile mbegu zinazoangamiza ardhi, wanadamu, na wanyama. Hili linaweza kupatikana tu kwa kutabikisha nidhamu za Uislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itawatosheleza wakaazi wa ardhini na mbinguni. Hapo, mbingu hazitazuia mvua yake, na ardhi haitazuia neema zake.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللهُ إِلَيْكَ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ إِنَّ اللهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ]

“Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.” [Surat Al-Qasas:77].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu