Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  1 Jumada I 1446 Na: HTY- 1446 / 06
M.  Jumapili, 03 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Vitendo vya Baraza la Uongozi wa Rais na Serikali yake ni Mithili ya Sarabi Jangwani, na Kuporomoka kwa Sarafu ni Shahidi wa hilo
(Imetafsiriwa)

Sarafu ya nchi katika maeneo yanayodhibitiwa na Baraza la Uongozi wa Rais imeshuhudia mporomoko wa kihistoria dhidi ya sarafu za kigeni kwa wiki kadhaa, huku riyal ya Saudia ikivuka kizuizi cha riyal 535, na dolari ya Marekani ilivuka kizuizi cha riyal 2,000. Wakati huo huo, baadhi ya miji ilishuhudia uasi mdogo wa kiraia na kufungwa kwa maduka ya kupinga kuporomoka kwa sarafu hiyo, na maduka kadhaa ya kubadilisha fedha yalifunga milango yake kwa watu baada ya janga hili la kuporomoka na kutoweza kwa serikali kutafuta suluhisho mwafaka kwa hilo.

Watu wa Yemen bado wanaishi katika janga la vita vya kipuuzi ambavyo vimeendelea kwa takriban muongo mmoja, vinavyosonga kati ya migogoro ya maisha mfululizo; Tukianza na kuzorota kwa usalama, kukatizwa kwa mishahara, kuporomoka kwa huduma, hasa umeme na maji, huduma duni, kuenea kwa umaskini, magonjwa na ukosefu wa ajira. Kuzorota kwa kiasi kikubwa kwa sarafu hiyo kumesababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa za msingi za chakula na kushindwa kwa watu katika maeneo yanayodhibitiwa na Baraza la Uongozi la Rais kupata riziki muhimu na ya msingi katika janga baya na la muda mrefu zaidi la kibinadamu duniani. kwa mujibu wa ripoti za UN.

Kuanguka kwa sarafu sio ghafla, kwani ilianza polepole tangu mwanzo wa vita. Kuporomoka kwa kasi kulianza wakati Benki Kuu jijini Sana'a ilipopiga marufuku toleo jipya la riyal ya Yemen iliyochapishwa na kutolewa na mshindani wake, Benki Kuu jijini Aden, katikati ya Disemba 2019. Benki Kuu ya Sana'a iliwapa wakaazi wa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake kipindi cha muda wa mwezi mmoja kubadilisha toleo jipya “haramu” kwa matoleo ya zamani, uamuzi uliofuatiwa na hali ya machafuko. Kuporomoka huku kuliendelea na kuongezeka wakati Mahouthi walipoizuia serikali ya Baraza la Rais kusafirisha mafuta ghafi mwishoni mwa 2022. Ingawa Benki ya Aden ilitekeleza hatua nyingi dhidi ya Benki ya Sana'a katika mwaka huo, zilizuiwa na amri kutoka nje, kulingana na kwa Gavana wa Benki Kuu jijini Aden, Ahmed Al-Ma'baqi.

Licha ya mikutano ya Waziri Mkuu inayoendelea, wa mwisho ulikuwa mnamo Alhamisi, tarehe 31/10/2024, pamoja na mikutano ya mabalozi wa nchi za nje na viongozi wa kiuchumi, pamoja na mkutano wa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi na Usimamizi wa Migogoro pamoja na Kamati na Mkuu wa Timu ya Uchumi mnamo tarehe 20/10/2024 kujadili maendeleo ya hali ya uchumi, fedha na pesa na kuratibu hatua na mamlaka zote ili kukabiliana na mfumko wa bei na kuimarisha nafasi ya sarafu ya taifa na kuzungumzia mipango ya uokoaji wa uchumi na hatua za kiuchumi na taratibu za kudhibiti mfumko wa bei. Habari na mazungumzo haya yalikuwa maongezi tu hewani na hayakuwa na masuluhisho yoyote ya kiutendaji mashinani, na watu hawakuona uboreshaji wowote wa bei za bidhaa kama matokeo ya kuporomoka huku.

Hoja zinazodaiwa na maafisa katika yale yanayoitwa maeneo halali za kusitisha uuzaji wa mafuta nje ya nchi na kuongeza gharama ya usafirishaji si lolote bali ni kuwatia watu ganzi. Makusanyo ya ushuru na forodha yanaendelea, kama vile rasilimali za bandari na utajiri wa samaki, pamoja na ukweli kwamba huduma zote zinazotolewa kwa watu hulipwa na hubeba gharama za usafirishaji kama nyongeza ya thamani juu ya bidhaa, na vile vile serikali kupokea ruzuku na amana za kigeni pamoja na misaada ya kibinadamu. Pamoja na kodi hizi zote, rasilimali na usaidizi wa kigeni, haijaboresha huduma za msingi au kubadilisha hali ya maisha, lakini nyingi huingia kwenye mifuko ya watu wenye ushawishi, pamoja na ukweli kwamba ukusanyaji wake ni kinyume na hukmu za Sharia ya kweli.

Sababu zilizozaa migogoro hii mfululizo, na sio tu tatizo la kuporomoka kwa sarafu, zinaongozwa na ufisadi na ubatili wa kanuni ya kibepari pamoja na itikadi na mifumo yake inayotekelezwa kwa watu. Tatizo la kiuchumi si katika uzalishaji kama wanavyodai wakuu wa mfumo wa kibepari, bali katika ugavi wa mali kwa raia mmoja mmoja. Miongoni mwa sababu hizo pia ni kutengwa kwa dhahabu na fedha katika sarafu na matumizi ya karatasi zisizo na thamani ya dhati kama vile dolari, uchumi wa kibepari kutegemea riba, na ukomo usio sahihi wa umilikaji kwa umiliki wa kibinafsi na umiliki wa dola, wakati uhalisia ni kwamba ni aina tatu za umilikaji: Umiliki wa serikali, umiliki binafsi, na umiliki wa umma unaogawiwa kwa raia kama vile mafuta na umiliki mwingine wa umma, pamoja na kuwepo kwa watawala vibaraka wanaotumikia Magharibi kafiri; kuelewa ala zinazomwaga balaa na matatizo na kuwakandamiza watu, pamoja na Yemen kuangukia kwenye mshiko wa mzozo kimataifa wa Uingereza na Marekani kupitia vibaraka wao wa kieneo, hususan watawala wa Al Saud na watawala wa Imarati, ambapo watawala wa Al Saud wanafanya kazi usiku na mchana katika maeneo yanayotawaliwa na kile kinachoitwa uhalali (vibaraka wa Waingereza) ili kuwazuia na kuwawekea masharti wakati wa kuwapa amana na ruzuku, na wanafanya hivyo kwa kumtumikia bwana wao Amerika ili kuwafukuza vibaraka wa Uingereza na kuwaweka vibaraka wake mwenyewe.

Ni wajibu wetu kutopuuza sababu zilizopelekea migogoro hii, kubwa zaidi ni mfumo wa kibepari wa kisekula unaotawala nchi yetu na nchi zote za Waislamu, na kuunganisha maisha ya watu na riziki na sarafu ya karatasi inayofuata dolari inapopanda na kushuka. Mfumo huu ndio sababu ya masaibu ya mwanadamu na kuporomoka kwa maisha yao, na suluhisho pekee la kutoka katika janga hili ni kung'oa mfumo huu kwa aina zote, nembo na ala kutoka kwa watawala vibaraka, na kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kwa njia ambayo Mtume (saw) alifuata kwa kuzingatia elimu, elimu ya pamoja, mgongano wa kifikra, mapambano ya kisiasa na kutafuta nusra kutoka kwa watu wenye nguvu na madaraka ili kuasisi mfumo adilifu kwa wanadamu wote; Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu