Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ujumbe kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Wabebaji Dawah Wanaotangaza Haki katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Ash-Sham
(Imetafsiriwa)

Ndugu na Dada Waheshimiwa,

Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Nimefurahishwa na misimamo yenu ya ajabu na uimara wenu juu ya haki (Haqq) bila ya kuogopa lawama za wenye kulaumu, licha ya kuwa mumezungukwa na matatizo, nafsi dhaifu, na wale ambao nyoyo zao zimejaa maradhi, na mlikuwa kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema:

[الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً وَقَالُوا حَسْبُنَا اللهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ * فَانْقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِنَ اللهِ وَفَضْلٍ لَمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللهِ وَاللهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ * إِنَّمَا ذَلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ]

“Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa*  Basi wakarudi na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Hapana baya lilio wagusa, na wakafuata yanayo mridhi Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu. * Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.” [Aali-Imran:173 - 175].

Ndugu na Dada Waheshimiwa,

Sisi tunamfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa kubeba da’wah katika hatua zake tatu, na kama ambavyo Washirikina walivyosimama vikali dhidi yake, vivyo hivyo leo watawala madhalimu wanasimama dhidi yetu, wakiungwa mkono na wanafiki, na wale ambao nyoyoni mwao muna maradhi, ambao hujivisha vazi la Uislamu, wakidhani kwamba duara linawazunguka wao na sio juu yao ambapo madhalimu hawa wanataka manufaa ya kidunia au ngawira ya muda mfupi.

[فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَنْ تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللهُ أَنْ يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِنْ عِنْدِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنْفُسِهِمْ نَادِمِينَ * وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ]

“Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao. * Na walio amini watasema: Hivyo hawa ndio wale walio apa ukomo wa viapo vyao kuwa wao wa pamoja nanyi? Vitendo vyao vitapotea bure, na wataamkia kuwa wenye kukhasirika.” [Al-Ma’idah: 52 - 53].

Ndugu na Dada Waheshimiwa,

Kutangaza kwenu haki kuliwashangaza maadui wa Uislamu na Waislamu, inakuwaje hivyo na ilhali nyinyi hamubebi silaha wala hamuongozi jeshi, lakini mukaharibu njama zao dhidi yao katika nyoyo zao na mukafanya mwisho wa mambo yao kuwa hasara, hivyo basi watu wakawakataa... Na hawakutambua kwamba watu wa batili, hata wakiinuka juu kiasi gani, wataanguka katika tope walizozitengeneza kwa mikono yao wenyewe... Hali kadhalika, hawakutambua kuwa upanga pekee hauna maana kama haukuambatanishwa na utambuzi na ufahamu... Lau washiriki wa kamati wangekuwa na busara huku wakitazama kinachoendelea katika suala la uhalalishaji mahusiano wa nchi zinazowazunguka na utawala dhalimu wa Ash-Sham, wangegundua kuwa matokeo ya yale yangewapata katika mambo mawili, lililo bora zaidi ni uchungu: kunyenyekea kwa dhalimu wa Ash-Sham, au kuandamwa na ukatili wa utawala. Kwa hivyo, lau wangekuwa na busara wangewatendea mema watu walio karibu nao, ili kupata uungwaji mkono na usaidizi kutoka kwao katika zama za dhulma ya utawala, na sio kuiga utawala katika kuwatesa wabebaji da’wah kama anavyofanya dhalimu, na kisha wanaangukia kwenye tope walizojitengenezea wenyewe… Kwa hiyo, hali yao inazidi kuwa mbaya zaidi duniani kabla ya Akhera, kisha wanajuta, na sasa sio wakati wa majuto.

Ndugu na Dada Waheshimiwa,

Bila shaka munajua kuwa mataifa ya kikafiri ya kikoloni na vibaraka wao kutoka katika nchi zilizopo katika ardhi za Kiislamu wanawakamata na kuwatesa Mashababu wetu na baadhi yao wanauawa mashahidi katika jela za mataifa hayo... Pamoja na hayo, azma yetu haidhoofiki katika njia ya Mwenyezi Mungu, na mataifa hayo yana nguvu zaidi kuliko kamati hiyo kwa nguvu na idadi kubwa zaidi... Na hiyo ni kwa sababu sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu, tunasema kweli na hatuogopi kwa Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumiwa, na tunaamini kwamba mwenye kuondoa dhiki ni Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye uwezo, ambaye huinua izza yetu na kudhoofisha njama ya adui yetu...

[وَمَنْ يَتَّقِ اللهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجاً * وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]

“Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea * Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 2-3].

Ndugu na Dada Waheshimiwa,

- Kushadidi kwa janga kunatangaza nafuu yake... Na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ayabadilishe majanga haya yanayofuatana, na kuchukua baadhi yake na mengine, ili yabadilishwe kwa ufunguzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ushindi wa karibu kwa kusimamisha Khilafah Rashida, kwani pamoja na dhiki kuna faraja mbili, si moja.

- Al-Hakim amesimulia katika Al-Mustadrak (2/329) kwa silsila ya wapokezi sahihi, ambapo Al-Hakim amesema: Ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Muslim, na Al-Dhahabi akaafikiana naye katika Al-Talkhees, kutoka kwa Umar bin Al-Khattab, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi: “Aliarifiwa kwamba Abu Ubaidah amefungiwa ndani ya Ash-Sham, na watu wamegeuka dhidi yake, basi Umar akamwandikia: Amani iwe juu yako. Ama yatakayofuata ni kwamba: Haitomshukia mja dhiki mpaka Mwenyezi Mungu Amruzuku baada ya hayo faraja, na hakuna uzito utakao shinda faraja mbili.”

- Ibn al-Qayyim (Rahimahullah) ametaja katika kitabu chake, Bada’i al-Fawa’id katika Sura: Kanuni Pana ya Mwanzo [Uumbaji]: “Kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْراً إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْراً]

“Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi, Hakika pamoja na uzito upo wepesi.” [Ash-Sharh: 5-6]. Ambapo dhiki - hata ikijirudia mara mbili - imejirudia kwa maelezo ya elimu, lakini ni moja. Na faraja ilirudiwa kwa maneno ya batili, kwa hivyo ni faraja mbili, kwani dhiki imezungukwa na faraja mbili, faraja kabla yake na faraja baada yake, kwani hakuna dhiki itakayoshinda faraja mbili.”

Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Ndugu Yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah,                                            17 Dhu al-Qa’adah 1444 H

Amiri wa Hizb ut Tahrir                                                                                6 Juni 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu