Jibu la Swali: Mabalozi katika Uislamu
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kifiqh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Nina swali kuhusiana na rasimu ya katiba ya Hizb. Katika ibara ya 7 kifungu cha F inasema: "Dola itatabikisha hukmu zote za Sharia na mambo yote ya Shari'ah ya Kiislamu, kama vile miamala, kanuni za adhabu, ushahidi, mifumo ya utawala na uchumi miongoni mwa mengine kwa usawa juu ya Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, Dola pia itatabikisha hayo hayo juu ya wale walio na mkataba, wanaomba hifadhi na wale wote walio chini ya mamlaka ya Uislamu kwa njia hiyo hiyo.