Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Wilaya Afghanistan:

Msimamo Imara kwa Ummah Ulio Amka

Mnamo Septemba 17 katika mkoa wa Laghman, mauaji ya wanawake 14 na watoto wasio na hatia yaliyo fanywa na makruseda, wakimtukana Mtume wetu (saw) na kama kawaida majibu ya aibu ya watawala wasaliti, ambayo hayajawahi kuwepo katika miaka 1400 ya historia, na uhaini mwingine kama huu unaofanywa na maadui wa Uislamu ni kutokana na kukosekana kwa ngao yenye ikhlasi (Khalifah) na Dola ya Khilafah.

Siku chache tu zilizopita, washenzi wa kisekula wa kidemokrasia walimtukana Mtume wetu (saw) kwa kutengeneza video fupi. Katika kujibu hili Ummah ulitaka kuondolewa kwa mabalozi wa Amerika na kufungwa kwa Balozi zote za Marekani katika ulimwenguni wa Kiislamu, lakini watawala wasaliti wameanza kuwakinga na kuuthibitishia Ummah kwamba wana wathamini mabwana wao zaidi ya umoja wa kisiasa na kijiografia wa Waislamu bali kihakika wao ndio kikwazo halisi katika njia umoja.

Mnamo Jumapili, 6 Septemba, katika kupinga dhidi ya kitendo hiki kiovu, walimu na wanafunzi wa Vyuo Vikuu jijini Kabul waliongoza maandamano makubwa na kufikisha ujumbe mzito kwa Wamagharibi, hususana Amerika na wakaitaka Serikali ya Afghanistan kusitisha mahusiano na Amerika na kumaliza maramoja mpango wa kimkakati. Waandamanaji pia walichoma moto bendera za Amerika na Israel vilevile na picha za Rais wa Amerika. Walikuwa pia wakiimba kauli mbiu “Demokrasia ni Nidhamu ya Kikafiri, Kuitabikisha na kuifanyia kazi ni Haram,” “Muda si mrefu tutawajibu hawa wahalifu,” “Waislamu wanahitaji Umoja wa Ummah,” Mwenyezi Mungu Mmoja, Aqeedah Moja, bendera moja, jeshi moja, dola moja, mfumo mmoja, mtawala mmoja, nchi moja, ni wajibu wa Ummah”. Pia walipaza sauti dhidi ya kinachoitwa Uhuru na vima vya kidemokrasia, waliwasifu Mujahidina wa Libya kwa kumuua balozi wa Amerika na watu wengine watatu kama majibu dhidi ya matusi kwa Mtume (saw).

Tofauti baina ya maandamano ya siku zilizopita na haya ya sasa ni kwamba hakuna yeyote aliyekuwa amebeba bendera za Taifa mikononi mwao, na hakuna maandamano yoyote katika Ulimwengu wa Kiislamu ambapo waandamanji walikuwa na bendera za Mataifa yao bali pindi waandamanaji katika nchi nyingine za Waislamu walipoziondoa bendera za Amerika walipandisha bendera ya Muhammad (saw) badala yake.

Tunaunga mkono maandamano yote ya namna hii sehemu zote ulimwenguni na kufanya kazi bila ya kuchoka kwa kufuata njia ya kisiasa na ya kifikra ya Muhammad (saw), na kuufahamisha Ummah kwamba suluhisho pekee la kukomesha vitendo viovu kama hivi, kulinda damu, rasilimali na ardhi ya Ummah, ni kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha tena dola ya Khilafah.

"Hakika Imamu ni Ngao, Nyuma yake Ummah unapigana na Kujilinda wenyewe" (Muslim)

Saifullah Mustanir
Kabul

Kwa picha zaidi:

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 29 Juni 2020 09:27

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu