Ijumaa, 29 Sha'aban 1446 | 2025/02/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kitengo cha Wanawake: “Enyi Mujahidina wa Ash-Sham! Wacha iwe kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu!

Mnamo siku ya Jumapili tarehe 8 Disemba 2024, watu wa Syria na Waislamu duniani walifurahishwa na taarifa kwamba dikteta katili, Bashar Al Assad amepinduliwa madarakani na wapiganaji wa upinzani, katika mzozo ambao mamia kwa maelfu wameuawa shahidi mikononi mwa utawala huu wa mauaji uliokuwa madarakani kwa miongo kadhaa.

Video hii ni mwito kwa Mujahidina na watu wa Syria kukataa uungaji mkono wowote wa kisiasa, masuluhisho, mazungumzo na ‘fedha chafu’ kutoka kwa Umoja wa Mataifa, Marekani na dola nyengine za magharibi pamoja na tawala zao wakala katika ardhi za Waislamu ambazo ndizo zilizojaribu kuvuruga mapinduzi ya Kiislamu nchini Syria tangu mwanzoni mwake na kumbakisha Assad mahali pake.

Video hii pia inazungumzia jinsi ushindi na mafanikio ya kweli kwa nchi ya Syria na kwengineko yanaweza kupatikana tu kupitia kuziondolea ardhi zetu mabaki yote ya uingiliaji kati na utawala wa wakoloni - ikiwemo vipengele vyote vya mfumo wao wa kisiasa na imani, na kuikumbatia ruwaza ya kweli ya Kiislamu iliyo huru.

Hili linaweza kupatikana tu kwa kutekeleza Sheria na Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ukamilifu chini ya kivuli cha Khilafah kwa njia ya Utume.

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Jumamosi, 02 Sha’aban 1446 H - 01 Februari 2025 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu