Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uholanzi: Ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan Kutaka Kukomeshwa kwa Utekaji Nyara wa Naveed Butt!

Ndani ya wigo wa kampeni ya kiulimwengu iliyozinduliwa na Hizb ut Tahrir kutaka kukomeshwa kwa utekaji nyara wa Mhandisi Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir nchini Uholanzi, ukiongozwa na mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir huko Uholanzi, Ustadh Okai Bala, na akiandamana na Ustadh Bilal Qassem na Ustadh Suleiman Tahtali, katika ziara ya ubalozi wa Pakistan jijini The Hague, ili kumkabidhi balozi au mwakilishi wake, taarifa iliyotolewa na Mhandisi Salah Eddine Adada / Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa anwani "Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan".

Ujumbe huo ulizungumza na balozi msaidizi na kuitaka serikali ya Pakistan, kupitia yeye, kufichua hatima ya mhandisi Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, na kumaliza kumpoteza kwake kwa nguvu, ambako kumedumu kwa zaidi ya miaka tisa baada ya kutekwa nyara mbele ya watoto wake na huduma za usalama za Pakistan. Pia ulivitaka vyombo vya habari vya Pakistan, na kila mtu anayefanya kazi kufikia haki na kila mtu aliye na uwezo, kubeba jukumu na kutafuta kutoa mwanga juu ya suala la utekaji nyara wa Naveed Butt.

Baada ya kumalizika kwa mazungumzo, ujumbe huo ulimkabidhi rasmi Balozi huyo Msaidizi taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir iliyopewa anwani  "Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan".

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Nchini Uholanzi

Ijumaa, 07 Dhu al-Qa'adah 1442 H sawia na 18 Juni 2021 M

#FreeNaveedButt
#TimeForIslam
#TimeForKhilafah
#HizbBritain

Kwa maelezo zaidi zuru mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Akaunti ya Twitter ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Ukurasa wa Instagram wa Hizb ut Tahrir / Uholanzi

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu