Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Indonesia
Mamia ya Wanachuoni wametangaza kuunga mkono Khilafah

Zaidi ya Wanachuoni Waislamu Masunni wamehudhuria Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (saw) katika Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Al Muntaha Madura, Indonesia, Ruwaza Moja ya Kuendeleza Nidhamu ya Khilafah.

Mwezi wa Rabiul Awwal ndio aliozaliwa Mtume Muhammad (saw). Waislamu ili kudhihirisha hisia na mapenzi yao kwa Mtume ndani ya mwezi wa Rabiul Awwal waliandaa maadhimisho mnamo Jumapili, Novemba 17, 2019 sawia na 20 Rabiul Awwal 1441 Hijria katika Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Al Muntaha, Bangkalan, Madura, Indonesia yaliyosimamiwa na wanachuoni wakiongozwa na Al Hajj Muhammad Toha Cholili.

Zaidi ya wahudhuriaji 700 wakijumuisha wanachuoni, wawakilishi wa Shule za Kiislamu za bweni kutoka Indonesia yote na Wahubiri (maustadh) wetu vipenzi walikuweko katika haflah (maadhimisho) ya kuzaliwa kwa Mtume (saw).

Miongoni mwa Wanachuo Waislamu Masunni waliohudhuria walikuwa ni:

KH. Syakhkrowardi, Mwanachuoni Muislamu Msunni kutoka Banten, Indonesia
KH. Rahmat S Labib, Mwanachuoni Muislamu Msunni kutoka Jakarta, Indonesia
KH. Mansur Muhyidin, Mwanachuoni Muislamu Msunni kutoka Banten, Indonesia
KH. Yasin Munthohar, Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Al Abqory, Banten, Indonesia
KH. Cecep Abadul Halim, Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Darussalam, na Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Al Bayyinah, Garut, West Java, Indonesia
KH. Ali Bayanullah, Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Darul Bayan, Sumedang, West Java
KH. AA. Syamri, Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Pancaran Amal, Gunung Pancar, Sentul, Bogor,
KH. Misbah Halimi, Mwanachuoni Muislamu Msunni kutoka Jombang, East Java
KH. Farid Makruf, Lc, Shule ya Kiislamu ya Bweni ya Al Mimbar, Jombang, East Java
KH. Muhammad Nizar, Mwanachuoni Muislamu Msunni kutoka Al Mimbar Jombang, East Java

Wanachuoni walitoa ruwaza ya kuendelea na mchakato wa kurudisha mpangilio wa Dola ya Kiislamu ya Mtume (saw) na Seerah yake. Napia wanatamani sana kutekeleza mwenendo wa maisha kwa njia ya Mtume kwa ukamilifu wake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir /Indonesia

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Julai 2020 19:16

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu