Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Malaysia: Kumhisabu Waziri wa Mambo ya Dini wa Malaysia

Siku moja baada ya kuikabidhi Idara ya Dini ya Kiislamu waraka wa ukumbusho kwa takriban majimbo yote nchini Malaysia, Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM) imemkabidhi Waziri katika Idara ya Waziri Mkuu (Mambo ya Kidini) waraka mwengine afisini mwake katika Jumba la Kiislamu la Putrajaya. 

Ujumbe wa chama hiki ukiongozwa na Msemaji wake, Ustadh Abdul Hakim Othman ulikaribishwa na afisa mmoja kutoka katika Kitengo cha Mawasiliano ya Jamuia, kama mwakilishi wa Waziri huyo. Lakini, ombi la Abdul Hakim la kutaka kukutana na Waziri yeye mwenyewe halikufaulu ambapo ilisemekana kwamba Waziri alikuwa yuko nyumbani akitumikia karantini ya siku 14 kutokana na tahadhari za virusi vya Koroni.

Yaliyomo ndani ya waraka huo ni kumhisabu (Muhasabah) Waziri yeye haswa, na serikali kwa jumla kwamba wamefanya madhambi makubwa ya kufunga misikiti, na chama hiki kikawasihi kuifungua tena misikiti yote mara moja baada ya kufungiwa Waislamu kutoswali swala za Ijumaa na jamaa kwa miezi mitatu.

Miongoni mwa risala muhimu zilizo tolewa katika waraka huo ni kuwa tayari kwa chama hiki kuwa na mazungumzo au mdahalo wa kifikra pamoja na serikali juu ya kadhia hii, ili kufikisha haki moja kwa moja kwa serikali.

Hata ingawa chama hiki kilimshukuru mwakilishi wa Waziri aliyeupokea waraka kwa uzuri kwa niaba ya Waziri aliye semekana kuwepo nyumbani, baadaye, Waziri huyo aliandika katika mtandao wa Twiiter kwamba kihakika alikuwepo afisini siku hiyo, ambapo karantini yake ya nyumbani ilikuwa imemalizika siku moja kabla. Ndiposa chama kimeweka swali katika tovuti na mtandao wa Facebook, ili kupata ufafanuzi kutoka kwa Waziri huyo, lakini hakuna jibu kama ilivyo tarajiwa.

05/06/2020

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu