Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 31/05/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 11 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 31 Mei 2023 M

Bajeti Nyengine ya IMF iko Njiani Kuihujumu Pakistan

Waziri wa Fedha alikagua mapendekezo ya bajeti mnamo tarehe 22 Mei 2023. Mapendekezo hayo si ya nyumbani, yaliojengwa juu ya msingi wa mahitaji ya Pakistan. Bajeti hiyo ni mujibu wa mapendekezo ya maafisa wa IMF waliozuru mnamo Februari 2023. Hakika, kila bajeti ya Pakistan ni kwa mujibu wa Itifaki ya wakoloni wa baada ya Washington. Sera ya kikoloni inahakikisha Ulimwengu wa Kiislamu unazama katika madeni na hauwezi kutengeneza silaha na teknolojia ya hali ya juu. Khilafah itajenga uchumi imara wa Kiislamu kupitia ukusanyaji na matumizi kwa mujibu wa Shariah.

06 Dhul Qa’adah 1444 H - 25 Mei 2023 M

Huduma ya Afya Haihusu Hotuba kwenye Makongamano bali Mabadiliko ya Hadharani

Katika Mkutano wa Sabiini na Sita wa Afya Duniani, Waziri wa Afya alisema, "Pakistan ina hisia kubwa ya uwajibikaji na kujitolea katika kuboresha matokeo ya afya ya watu wao." Kwa miongo kadhaa, kipote cha watawala hawana matokeo na hawana mpango. Wanasafiri ng’ambo kwa ajili ya huduma zao wenyewe za afya. Utawala unahusu tu kujali maslahi yao, sio ya watu. Huduma ya afya ni wajibu kwa Kiongozi wa Waislamu. Ni Khilafah ndiyo iliyoanzisha huduma za afya bila malipo, ikiwa na hospitali za kufundishia zilizoongoza ulimwengu katika upasuaji na tiba kwa karne nyingi.

06 Dhul Qa'adah 1444 H - 26 Mei 2023 M

Vunjeni Miundombinu ya Kigaidi ya Kimarekani nchini Pakistan ili Kulinda Wanajeshi wetu

Mnamo tarehe 24 Mei 2023, jeshi lilisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, "Vikosi vya usalama na vyombo vya kutekeleza sheria vya Pakistan vimedhamiria kuondoa tishio la ugaidi." Wanajeshi wetu wanalengwa kila mara na washambuliaji wa kujitoa mhanga. Chanzo cha ugaidi ni mtandao wa kigaidi wa Marekani. Suluhisho ni kuondolewa kwake. Fungeni vitui vya ujasusi ndani ya ubalozi wa Marekani na afisi ndogo za ubalozi. Wafukuzeni maafisa wa uhusiano wa Kimarekani ndani ya makao makuu ya jeshi. Fungeni njia ya anga inayotumiwa na droni za Kimarekani. Simamisheni Khilafah ili kuhakikisha hilo linafanywa.

07 Dhul Qa'adah 1444 H - 27 Mei 2023 M

Uislamu Unalazimisha Uhamasishaji wa Kijeshi Kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa, sio Msaada wa Kimaadili Pekee

Katika mkutano wake na waandishi wa habari wa Mei 25, Afisi ya Mambo ya Nje iliahidi "msaada wa kimaadili, kidiplomasia na kisiasa" kwa Kashmir. Kwa hiyo, watawala huzuia majeshi yetu, huku wakiomba Umoja wa Mataifa, ingawa ni chombo cha ukoloni, ambacho kinahakikisha kukaliwa kwa mabavu Kashmir na Palestina. Uislamu unalazimisha uhamasishaji wa jeshi ili kuzikomboa Ardhi za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu. Kwa karne nyingi, kabla au baada, majeshi ya Khilafah yaliwafukuza wavamizi na wakaliaji kimabavu wote. Khilafah ndiyo itakayohakikisha umoja wa Waislamu, maandalizi ya vikosi vyao vya kijeshi na ukombozi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

08 Dhul Qa'adah 1444 H - 28 Mei 2023 M

Mfumo wa Uchumi wa Kirasilimali Unafeli Kote Duniani

Gavana Christopher J. Waller wa Hazina ya Marekani alisema mnamo tarehe 24 Mei, "kuanzia na uchumi, shughuli zimepungua... mfumko wa bei uko juu mno." Licha ya madai ya Biden, uchumi wa Marekani unabaki katika mgogoro mkubwa. Asili ya mgogoro huo ni mfumo wa kifedha uliojengwa juu ya riba, uliozidishwa na mfumo wa hifadhi wa benki na sarafu isiyo na thamani ya dhati (fiat). Urasilimali umefeli duniani kote, vipi utafanikiwa Pakistan? Khilafah itatabikisha mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu, ambao ulifanikiwa kwa karne nyingi, ukitoa ustawi katika mabara matatu.

09 Dhul Qa'adah 1444 H - 29 Mei 2023 M

Watawala wa Pakistan Wanasherehekea Youm-e-Takbir, Huku Wakijitahidi Kuachana na Silaha za Nyuklia

Mnamo tarehe 28 Mei, afisi ya habari ya jeshi ilisherehekea Uwezekano wa Kujiuia kwa Uchache kwa Pakistan. Walakini, baada ya kuisalimisha Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, kuwazuia wanajeshi wetu, na kusawazisha mahusiano na India, watawala kuachana na silaha za nyuklia ni uwezekano unaokua. Uislamu unaamuru ubora wa kijeshi juu ya maadui wote, ili kuhakikisha utawala wa Uislamu duniani kote. Khilafah iliongoza ulimwengu katika teknolojia ya kijeshi kwa karne nyingi. Baada ya kuasisiwa kwake, hivi karibuni inshaaAllah, Khilafah kwa Njia ya Utume itatia hofu katika nyoyo za kila dhalimu, kwa mara nyengine tena.

10 Dhul Qa'adah 1444 H - 30 Mei 2023 M

Balozi wa Marekani ni Naibu wa Raj wa Ukoloni wa Marekani nchini Pakistan

Mnamo tarehe 26 Mei 2023, Waziri wa Fedha alimweleza Balozi wa Marekani kuhusu mipango inayohusiana na mapato na matumizi, kwa ajili ya kutimiza majukumu ya kimataifa ya kifedha. Kama ilivyo katika Ulimwengu mzima wa Kiislamu, balozi wa Marekani ndiye mtawala halisi wa Pakistan. Watawala wa Pakistan ni makarani tu wa kupiga chapa sera za kiuchumi za wakoloni. Bila ya Khilafah, hakuna dhana ya uhuru au mamlaka, katika nyanja yoyote, uchumi au nyengineyo.

11 Dhul Qa'adah 1444 H - 31 Mei 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu