Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 17/04/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 08 Shawwal 1445 H sawia na 17 Aprili 2024 M

Haitoshi kukumbuka Palestina na Kashmir Pekee. Ummah na Majeshi yake Lazima Yahamasike

Katika ujumbe wake wa IDD wa 9 Aprili 2024, Waziri Mkuu wa Pakistan alisema, "Ninawasihi pia Waislamu ulimwenguni kote kuwakumbuka ndugu zao wa Palestina na Kashmiri ambao wanakabiliwa na aina mbaya zaidi ya ukatili wa vikosi vya uvamizi na watadhibitiwa kufurahiya furaha za Idd." Ni wazi kwa Waislamu kwamba watawala wa sasa wa Ummah wa Kiislamu ndio sababu ya shida na udhalilishaji wake. Lazima sote tujitahidi kusimamisha, Khilafah Rashida. Ni hapo ndipo Khalifa Rashida atahamasisha vikosi vyetu kuwanusuru waliokandamizwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema, إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ  "Hakika, Imam (Khalifa) ni ngao. Watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye." [Muslim]

02 Shawwal 1445 H - 11 Aprili 2024 M

 

Je! Watoto wa Makamanda wa Jeshi wenye Kugeuza Wimbi la Vita?

Mfano pekee wa afisa wa jeshi wa Kiislamu ni Muhammad al-Mustafa ﷺ. Wakati Waislamu walipovunja muundo ya kijeshi kwenye Vita vya Hunain, Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisimama kidete kwa kuwakusanya askari na kutangaza, akapiga kelele kwa sauti kubwa, أنا النبي لا يكذب  "Mimi ni Mtume asiyedanganya." [An-Nawawi]. Mara moja Waislamu waligeuza wimbi la vita hadi waliposhinda. Kwa hivyo wako wapi makamanda wa Kiislamu wa leo, ambao watasimama kidete na kugeuza wimbi la vita dhidi ya Gaza, wakilishinda umbile la Kiyahudi na wafuasi wake wa wakoloni?

03 Shawwal 1445 H - 12 Aprili 2024 M

Pakistan na Saudi Arabia, zlizounganishwa chini ya Khilafah, Zinaweza Kuondoa kwa Urahisi Minyororo ya Utumwa kwa Marekani

Saudi Arabia imeonyesha nia ya kuwekeza dolari bilioni 1 katika mradi wa Reko Diq, wa shaba na dhahabu nchini Pakistan. Licha ya kuwa dola ya nyuklia, Pakistan inategemea Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kwa dhamana ya kifedha. Vivyo hivyo, mzalishaji wa pili mkubwa wa mafuta ulimwenguni, Saudi Arabia inategemea Marekani kwa usalama wake. Kwa kukomesha dola za kitaifa na kusimamisha Khilafah, nchi hizi mbili za Kiislamu na rasilimali zao zitaunganishwa. Zote mbili zingeokolewa kutoka kwa utumwa wa Marekani. Mfumo  wa Kilimwengu wa Marekani utapingwa kwa urahisi na ulimwengu wa Kiisilamu ulioungana. Hakutakuwa na kikwazo katika kutuma vikosi vya jeshi kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir na Palestina.

04 Shawwal 1445 H - 13 Aprili 2024 M

Kilio cha Umma Kufuatia Tukio la Bahawalnagar Kinasisitiza Haja ya Haraka ya Kubadilisha Mfumo wa Mfumo wa Sasa kwa Khilafah

Katika kipindi cha Idd, tukio la Bahawalnagar lilizua hasira kote Pakistan. Watu walionyesha kufadhaika na ufisadi ulioenea ndani ya polisi wa Punjab na kukashifu umakini wa ndani wa jeshi, badala ya kupanua kunyosha nusra kwa Palestina na Kashmir. Maswali yaliibuka kuhusu madhumuni ya gwaride la kijeshi, haswa mnamo tarehe 23 Machi, wakati vikosi vyetu vya jeshi havipelekwa kuinusuru Gaza. Kukataliwa kulikoenea kwa watawala wa sasa na mfumo uliopo kunaashiria mauti yake yaliyokaribia. Uislamu unasimama kama nguvu pekee ya kuunganisha Waislamu, ikionyesha Khilafah kama njia pekee ya mageuzi ya Pakistan. Ni muhimu kwamba watu wenye ikhlasi ndani ya vikosi vya jeshi mara moja wapeane Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa usimamishaji wa Khilafah kwa njia ya Utume.

05 Shawwal 1445 H – 14 Aprili 2024 M

Riba ni Mzigo wa Dhambi. Walakini, Waziri wa Fedha wa Pakistan Amekwenda Washington ili Kuiongeza

Mnamo Aprili 12, Waziri wa Fedha alikutana na Waziri Mkuu kujadili mikutano yake iliyopangwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia na taasisi zingine za wakoloni. Mikutano kama hiyo haina maana. Pande hizo mbili tayari zimekubaliana juu ya sera za uharibifu za makubaliano ya baada ya Washington. Wanajadili tu njia za mikopo mpya. Pakistan imezama katika deni la riba. Watawala hawatoi njia ya kutokea isipokuwa kwa deni zaidi na riba zaidi. Ni mabadiliko makubwa pekee kwa msingi wa Uislamu ndiyo yanayoweza kutuondoa kwenye kinamasi hiki. Hilo linawezekana tu kupitia kusimamishwa Khilafah Rashida.

06 Shawwal 1445 H - 15 Aprili 2024 M

Je! Kujizuia ni kwa Majeshi ya Waislamu Pekee?!

Baada ya droni na makombora ya Iran kurushwa dhidi ya umbile la Mayahudi, Wizara ya Mambo ya nje nchini Pakistan ilisema mnamo tarehe 14 Aprili 2024, "Tunatoa wito kwa pande zote kujizuia kikamilifu." Je! Kujizuia ni kwa majeshi ya Waislamu pekee? Droni na makombora yalipaswa kuwa utangulizi wa vita vyetu yote kwa kutumia ndege za kivita, vifaru na vikosi vya Ummah. Kwa hivyo, Iran ilijizuia kiusanii. Ama kwa Mfalme wa Jordan, alizidungua droni, akiwaogesha watu kwa uchafu. Ama kwa watawala wa Pakistan, wanatoa wito wa kujizuia mbele ya maadui wa Waislamu, lakini wako tayari kupigana na Waislamu baada ya simu moja tu kutoka Washington. Ni kwa Ummah na majeshi yake kuwang’oa watawala hawa na kusimamisha tena Khilafah Rashida kumaliza mateso na udhalilifu.

07 Shawwal H - 16 Aprili 2024 M

Khilafah Rashida Italishinda Jeshi la Marekani na Umbile la Kiyahudi kutoka Pande Zote Inshaaallah

Amri Kuu ya Jeshi la Marekani ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari mnamo tarehe 14 Aprili 2024 na kichwa "Sasidho la Utetezi wa Vitendo vya 'Israel'." Sasa kwa kuwa Magharibi na umbile la Kiyahudi zimefichua mbinu zao za utetezi, Ummah na majeshi yake lazima yasonge. Misri lazima ifungue mpaka wake wa Rafah kwa ajili ya kuvuka kwa askari na vifaru vya Ummah. Jordan, Syria na Uturuki lazima zifungue kambi zao za anga kwa ajili ya ndege za kivita za Ummah. Dola za Ghuba lazima zifungue bandari zao kwa ajili ya manuari za Ummah. Dola zote zinazoizunguka Palestina lazima zifungue anga zao kwa ajili ya makombora ya Pakistan. Watawala wa sasa kamwe hawatafanya hivyo. Khilafah Rashida, Inshaa Allah itafanya hivyo hivi karibuni. Basi hebu Ummah na majeshi yake na yawapindue watawala hawa na kuhamasisha chini ya Khalifa Rashid kunusuru Gaza.

08 Shawwal H – 17 Aprili 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu