Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Kashmir iliyo porwa inamsubiri Khalifah Muongofu ambaye Atajibu Vilio vya Watoto Wake kwa Kutumia Vikosi vya Jeshi vyenye Kutembea kwa ajili ya Ukombozi Wake!

Bila kuangalia, Modi, Raja Dahir wa enzi zetu, angeendelea na kutokujali kumwaga damu takatifu ya mama, dada, kaka na watoto wetu.

Tangu tarehe 5 Agosti 2019, washirikina wa Dola ya Kibaniani walianzisha vita dhidi ya kaka na dada zetu Waislamu katika Kashmir iliyoporwa, wakainyakua kwa nguvu, wakipofushwa kwa vijibomu, wakiwakatakata vipande vipande na kuuwawa kwa risasi.

Ni wazi kama ulivyo mwangaza wa mchana kuwa licha ya ukandamizaji wa kutisha na wa kinyama uliofanywa huko Kashmir, utawala wa sasa wa Pakistan usingesonga mbele hata kwa inchi moja au msuli kwa ajili ya kuwasaidia Waislamu. Utawala usio na hisia huhesabu miili ya waliokufa, hufanya rufaa kwa jamii ya kimataifa, hutuma nukuu za tweet na kutenda kama mtu wa kawaida kwa Umoja wa Mataifa. Bila aibu, serikali hii inafanya kana kwamba imetimiza lake kwa Kashmir.

Wakidhihirisha unafiki huu kwa jina la ‘Dola ya Madina’, uongozi wa namna hii kamwe hauwezi kuandaa na kuunganisha majeshi yetu kwa ajili ya kuikomboa Kashmir.

Dola ya Khilafah ni kinga na ngao ya Waislamu, Mtume (saw) anasema,

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imamu ni Ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo.” [Muslim].

Fuateni njia nzuri ya Abu Bakr As-Siddiq (ra), aliyetuma majeshi kuwashinda manabii wa uongo, wale waliokataa kutoa Zaka na kupigana na Warumi. Abu Bakr (ra) alisisitiza kupeleka majeshi akisema ataendelea kutuma majeshi hata ikiwa hiyo ingemaanisha kutokuwa na ulinzi huko Madina dhidi ya wanyama wa porini.

Enyi Waislamu wa Majeshi ya Pakistan!

Waislamu wa Kashmir iliyo porwa, hawasubiri Jamii ya Kimataifa ambayo imewasaliti kwa miongo kadhaa, lakini wanakungojeeni nyinyi, kizazi cha Khalid bin Waleed (ra), Salahudeen na Muhammad bin Qasim, ambao watawakomboa. Toeni Nussrah sasa kwa ajili ya kuregeshwa Khilafah (ukhalifa) kupitia Njia ya Utume (saw) kwa hivyo mnaamriwa kutembea kuelekea Srinagar ili kuitikia vilio vya waliokandamizwa, bila kuchelewa zaidi.

Alkhamis, 11 Dhul-Qi'dah 1441H - 02 Julai 2020M

#KhilafahItaikomboaKashmir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu