Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Ardhi ya Baraka - Palestina:

Kitengo cha Wanawake Kimeandaa Warsha kuhusu CEDAW

Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir ndani ya Ardhi ya Baraka (Palestina) kiliandaa mnamo Jumatano, 23 Rabii' Awwal 1441 H – 20 Novemba 2019 M warsha kubwa baada ya swala ya Asr ndani ya Msikiti wa Al-Sha'rawi huko Hebron (al-Khalil) ikiwa ni sehemu ya kampeni ya uzindushi dhidi ya CEDAW.

Dada Umm Muath alifungua warsha kwa dua na kumtakia amani Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuwakaribisha kina dada waheshimiwa kuzungumzia hatari inayotokana na makubaliano hayo; ambapo alizungumza kuhusu ufahamu wa ulinzi, hadhi na stara na kuzungumzia kuhusu zama za Ujahiliya mpaka ulipokuja Uislamu. Pia alijadili vipengee vya CEDAW na kupitishwa kwake na Mamlaka ya Palestina. Mzungumzaji alivirudia baadhi ya vipengee vyake ambavyo vinakwenda kinyume na hukmu za Mwenyezi Mungu kama vile vya umri wa ndoa, ufahamu juu ya usimamizi (wali) ambao wanataka kuupiga marufuku, ufahamu wa usawa wa kijinsia katika kila kitu ikijumuisha mirathi pamoja na kuchanganyika huru na taasisi nyingi za kiukombozi wa wanawake zilizotumwa huku na kule na haki za wanawake na mada nyingi zinazohusiana.

Yote haya yametokea baada ya kupoteza Khilafah, ambapo Waislamu wamekuwa kama mayatima katika meza za mbwa mwitu na Waislamu wameanguka ndani ya mikono ya Wamagharibi. Wanataka kuwatoa wanawake Waislamu nje ya utukufu wa Uislamu, wanafanyakazi kuitia ufisadi familia yote na wanataka kuwalazimishia watu makubaliano yao na licha ya kwamba hakuna makubaliano yaliyowapa wanawake haki zao na heshima yao na kuwahifadhi kama ulivyofanya Uislamu. Dada Umm Muath alisisitiza kwamba hakuna suluhisho kwetu isipokuwa ni kuweza kurudia Hukumu ya Mwenyezi Mungu (swt).

Wahudhuriaji walitangamana na kuelezea kufurahishwa kwao na kile kilichowasilishwa na warsha hiyo. Idadi ya wahudhuriaji ilikuwa takribani wanawake 600. Alhamdulillah.

Jumatano, 23 Rabii' al-Awwal 1441 H - Novemba 20, 2019 M

Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Ndani ya Ardhi ya Baraka (Palestina)

نرفض_سيداو#
#WeRejectCEDAW
#CEDAWreddediyoruz

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 16 Februari 2020 13:13

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu