Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa: Kutoka Al-Khalil, Watu wa Palestina Wanaelekeza Wito wa Haraka kwa Umma na Majeshi Yake

(Imetafsiriwa)

Chini ya kauli mbiu (Enyi Umma wa Kiislamu, Nusra Nusra, Tusaidieni kabla Hatujamalizika), Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa Palestina iliandaa kisimamo kikubwa katika mji wa Al-Khalil mnamo Jumanne, 12 Disemba 2023 M, ambapo watu wa Palestina wanaume kwa wanawake, walielekeza wito wa haraka kwa Umma na majeshi yake na nguvu zake zilizo hai kutaharaki kwa haraka kunusuru Gaza na damu ya watoto wake, na kwa Palestina na watu wake na Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa.

Kisimamo hicho kilijumuisha kalima mbili zilizotolewa na Ustadh Abu Mu’min na mmoja wa kina dada, ambapo wanawake walishiriki katika kisimamo hiki kwa sura ya kustaajabisha.

Katika kalima kuu, Abu Mu’min aliwasilisha picha mbili kutoka Gaza; ya kwanza ni ile ambayo watu wa Gaza wanakabiliwa na mauaji, umwagwaji damu, njaa, na mauaji ya halaiki mikononi mwa adui katili, ambaye uchi wake umefunuliwa, na uongo wake umefichuka, na yeye husaidia na kupewa nafasi na watawala wasaliti na kiongozi wa Uovu Marekani na washirika wake.

Ama picha ya pili, ni ushujaa wa Mujahidina uliotokana na imani na silaha kwa msaada wa Mwenyezi Mungu mbele ya silaha na vifaa vya Mayahudi, wanazopewa na dola kubwa.

Akisisitiza kwamba "Mujahidina wa Gaza ndio mashujaa wa vita, kama ilivyo hali kwa Umma huu tangu mwanzo wa Uislamu, hata ikiwa wameachwa kupambana kati yao na adui wao uso kwa uso, mtu mmoja kwa watu kumi, vita vimetulia, lakini watu wa Gaza waliotengwa na kuzingirwa, wamekusanywa pamoja na mabomu ya Mayahudi, silaha za Magharibi, usaidizi wa watawala, kizuizi cha majirani, na Mujahidina wa Gaza hawamiliki isipokuwa zenye kumuumizi adui Katika uwanja wa mapambano, hawamiliki ndege, makombora, wala vifaru mpaka wawalinde watu wa Gaza kutokana na masaibu yao.

Abu Moamen kwa niaba ya watu wa Palestina alielekeza wito kwa Waislamu na majeshi yao kwamba msaada msaada na nusra nusra, na watu wa Gaza hakubakisha isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) apanue vifua vyenu kwa ajili ya nusra yenu. Gaza ya leo inasema kwa Umma La Ilaha illa Allah mtutambue msitutambue.

Mmoja wa kina dada alitoa kalima kwa niaba ya wanawake wa Palestina, ambayo kwayo alielekeza wito kwa maafisa na askari kutoka kwa majeshi ya Waislamu kwa kusema, "Sisi ni binti zenu, dada zenu na mama zenu miongoni mwa wanawake wa Ardhi Iliyobarikiwa, Palestina, tumetoka kuwalilieni basi tusikilizeni, tumetoka tukiomba nusra yenu basi tutazameni, je! Sisi sio heshima yenu? Je! Sisi sio utukufu wenu? Je sisi sio fadhila zenu? Je, sio shahidi anayekufa kwa ajili ya kutuhami sisi...?! je, iko wapi hamasa yenu? Je, iko wapi ghera yenu? Je, iko wapi fahari yenu? Je, iko wapi shajaa yenu? Je, iko wapi haiba na nuru yake? Je, ziko wapi panga na sauti zake? Je, iko wapi mikuki na mirusho yake? Viko enyi ndugu zetu pokeeni bishara njema? Mko wapi enyi mama zetu mtapata? Mko wapi enyi dada zetu msioogope wala msihuzunike...?! Hakika wakati umewadia kutokana na bidii yake, na hakika adui amefichua meno yake, basi ima muharakishe hivyo mufaulu kutokana na sisi tuliobakia, au muzinyime nafsi zenu endapo hamtatusaidia.”

Kisimamo hicho kilisheheni vifijo kutoka kwa halaiki ya watu ambao waliwataka majeshi kutaharaki mara moja, na walinyanyua miito na kubeba bendera za Raya.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Sehemu ya Amali ya Kisimamo

- Angazo la Amali ya Kisimamo -

- Video za Habari Ziada za Kisimamo -

- Mahojiano na Mikutano na watu wakati wa Amali -

- Ujumbe kutoka Ardhi Iliyobarikiwa kwenda kwa Watu wa Uturuki na Jeshi Lao -

Dkt. Ibrahim Al-Tamimi

 - Uamuzi wa Vita Lazima Uondolewe Mikononi mwa Tawala zilizoko ili Kuwaokoa watu wa Palestina  -

Dkt. Ibrahim Al-Tamimi

- Marekani Inalisambazia Umbile la Kiyahudi Mabomu, Je, Umma na Majeshi yake Yamefanya nini kwa Gaza?! -

Dkt. Ibrahim Al-Tamimi

- Je! Jeshi la Misri, Jordan na Uturuki Linasubiri Nini ili Kusonga na Kuwaokoa Watu wa Gaza? -

Dkt. Ibrahim Al-Tamimi

- Ujumbe kwa Viongozi wa Majeshi na Makamanda! -

Dkt. Mus’ab Abu Arqoub

- Watu wa Al-Khalil Wanalilia Umma wa Kiislamu! -

Dkt. Mus’ab Abu Arqoub

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu