- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa:
Kitengo cha Wanawake “Kalima kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 104 ya Kuvunjwa Khilafah!”
Kwa mnasaba wa ujio wa kumbukumbu ya miaka 104 ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu na makhaini wa Kiarabu na Kituruki iliyoasisiwa na Bwana wa Mitume Muhammad (saw) na maswahaba zake watukufu na waliobarikiwa, Mwenyezi Mungu awawie radhi, na kukomeshwa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab al-Muharram katika mwaka wa 1342 H sawia na 03/03/1924 M, Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika The Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kinawasilisha mkusanyiko wa kalima hizo.
Jumanne, 28 Rajab Tukufu sawia na 28 Januari 2025 M
- Ahadi ya kweli na Bishara za Ushindi Zinakaribia -
Enyi Umma wa Uislamu, ahadi ya kweli imekaribia, na upepo wa Khilafah na dalili za ushindi zimeonekana kwenye upeo wa macho tufungeni safu na tuzidishe kazi kwa ajili ya kuregea kwa mama yetu, Khilafah. Na siku hiyo waumini watafurahia ushindi wa Mwenyezi Mungu.
- Enyi Waislamu, Regesheni kwa Umma Izza na Utukufu Wake -
Simameni, enyi Waislamu, na mshirikiane pamoja na wanaofanyakazi kurudisha izza na utukufu wa Umma kwa kuregea Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
- Enyi Maafisa wa Jeshi, Haijuzu Kuzembea katika Faradhi ya Kufanya Kazi ya Kusimamisha Khilafah -
Enyi Umma wa Kiislamu, mpaka lini mtapuuza faradhi hii kubwa, je, ni lini mtahamasika, enyi maafisa wa Kiislamu? Je! hamjasikia vilio vya waliodhulumiwa, Fanyeni haraka, enyi maafisa, ili mupate utukufu wa ushindi na kupandisha bendera ya Uislamu kwenye kuta za Al-Qudsi?
- Umma wa Kiislamu una Shauku ya Kuinuka kutoka kwenye Vifusi -
Katika kumbukumbu ya mwaka wa 104 wa kuvunjwa Khilafah, mmoja wa wanawake wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) anasema kuwa, Umma wa Kiislamu bado unadunda kwa matumaini na imani na kuwataka watu wenye nguvu na uwezo wanyanyuke kwa ajili ya izza yao.
- Alama Ishara -
#أقيموا_الخلافة
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
#خلافت_کو_قائم_کرو
#TurudisheniKhilafah