Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wilayah Sudan: Taarifa kwa Vyombo vya Habari 05/09/2020 M

Hizb ut-Tahrir ilifanya amali kadhaa katika wiki iliyopita; ambapo hotuba za halaiki zilifanywa mjini Omdurman, katika maeneo ya soko la Sabireen na Al-Thawra 17 na jijini Khartoum katika maeneo ya Kalakila na Dukhainat ambapo anwani za hotuba hizi zilikuwa: "Usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi ni uhalifu mkubwa na khiyana kuu", "Watawala vibaraka wa Waislamu wako chini ya ishara za maelekezo ya Magharibi kafiri katika kupitisha mipango yake.", "Mikataba ya amani na uingiliaji wa kutoka nje", "Kwa kufuata nyayo za Naivasha ... serikali ya mpito inataka kuirarua Sudan iliyosalia" na "Namna Khilafah itakavyo shughulikia Mafuriko, Mvua kubwa na Maafa" ambapo wasikilizaji walihutubiwa na wazungumzaji tofauti tofauti katika wanachama wa Hizb ut-Tahrir Wilayah ya Sudan. Mwisho wa hotuba zao, wazungumzaji wote waliashiria jinsi gani Khilafah inaweza kuyaondoa majanga yote wanayopitia Waislamu nchini Sudan na kwengineko kama mchungaji wa mambo yao.

Maingiliano ya watu na hotuba hizi yalikuwa changamfu kwa miito kama 'Hapana Mola wa Kweli isipokuwa Mwenyezi Mungu na Khilafah ni Ahadi ya Mwenyezi Mungu', 'Zimefeli, Dola zote Zifeli na Khilafah ndio Suluhisho'; Huku baadhi ya wahudhuriaji wakichangia kwa maneno mazito yaliyo chochea zaidi hisia za hadhira kwa kusema kwamba wako tayari kupigana Jihad na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa kutokamana na uchafu wa Mayahudi.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Sudan

Mkusanyiko wa Picha

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 14 Septemba 2020 14:02

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu