Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Amali kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 101 ya Kuvunjwa Khilafah

Katika mwezi Mtukufu wa Rajab mwaka huu 1443 H / 2022 M na kwa mnasaba wa kumbukumbu mbaya ya wahalifu kuivunja Dola ya Kiislamu na kuuondoa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) tarehe 28 Rajab 1342 H sawia na na Tarehe 3 Machi mwaka wa 1924 M.

Ukurasa huu tutaangazia amali zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 H ya kuvunjwa Dola ya Khilafah tarehe 28 Rajab Tukufu 1342 H kama sehemu ya amali za kimataifa za Hizb ut Tahrir.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa’la aharakishe kusimama kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya hilo.

Ijumaa, 03 Rajab Tukufu 1443 H sawia na 04 Februari 2022 M

- Ripoti ya Wiki ya Kwanza ya Amali za Kumbukumbu za Miaka 101 ya Kuvunjwa Khilafah -

Jumamosi, 11 Rajab Tukufu 1443 H sawia na 04 Februari 2022 M

Mwezi mwema wa Rajab umeujia Umma wa Kiislamu mwaka huu wa 1443 H, huku ukiishi kwenye giza usiku na mchana, kwani miaka 101 imepita tangu kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah tarehe 28 Rajab 1342 H. Ardhi zao zimekaliwa, heshima yao kuvunjwa, matukufu yao kuchafuliwa, na dini yao kutengwa na utawala na usimamizi wa mambo ya watu. Na kafiri mkoloni akatawala katika nchi za Kiislamu moja kwa moja, na kupitia kwa vibaraka wake watawala na wanasiasa, ameudhalilisha Umma na kuiba mali yake, na ukaanza kukabiliwa na njaa, umasikini, na maradhi, na kuenea kwa ufisadi na fikra potofu, kama vile fikra ya uhuru, usekula, serikali ya kiraia, demokrasia, na mapinduzi ya kijeshi. Udhalilifu baada ya udhalilifu.

Kwa kukumbuka kumbukumbu hii chungu, na kuuamsha Ummah kwenye wajibu wake, katika wiki ya kwanza ya mwezi wa sasa wa Rajab 1443 H, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa amali mbalimbali katika mji mkuu, Khartoum, na miji mbalimbali ya Sudan, ambapo maelfu ya vipeperushi viligawanywa masokoni na sehemu za umma.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan pia waliandaa hotuba za halaiki katika maeneo tofauti tofauti: katika eneo la Al Kalakila walitoa hotuba ya hadhara katika Msikiti wa Sheikh Bakri Al Kalakila Al Wahda ili kuwakumbusha Waislamu juu ya kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah mikononi mwa mkoloni kafiri Magharibi, ikiongozwa na Uingereza na Ufaransa, kwa msaada wa wasaliti wa Kiarabu na Waturuki. Kwa kuanguka Khilafah, Ummah ulipa hasara kubwa sana.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Kaskazini pia waliandaa hotuba ya hadhara kuhusu uingiliaji kati wa kigeni katika masuala ya nchi hii bila kuwepo kwa Dola ya Khilafah. Nchi hii imegeuka kuwa kivutio cha kazi za mabalozi, mashirika na idara za kijasusi za nje, kwani ni kazi iliyoandaliwa na nchi za kikoloni kwa msaada wa mawakala wao nyumbani. Ilikuwa ndio sababu muhimu zaidi iliyofungua njia kwa uingiliaji kati huu. Kuondolewa kwa dola ya Khilafah iliyoukumbatia Umma wa Kiislamu kwa zaidi ya karne 13, na kupinduliwa kwake mwaka 1924 ambako kulipelekea kusambaratika na kugawanyika kwa Umma, na kuanzishwa kwa maumbo bandia yaliyo dhaifu juu ya magofu ya Dola ya Khilafah, yaliyotawaliwa na tawala za kisiasa ambazo dhamira yake ni kuupiga vita Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, na kupotosha sura ya Uislamu wa kisiasa kifikra na kihistoria.

- Ripoti ya Wiki ya Pili ya Amali za Kumbukumbu ya Miaka 101 ya Kuvunjwa Khilafah -

Jumamosi, 18 Rajab Tukufu 1443 H sawia na 19 Februari 2022 M

Ikiendelea kukumbuka kumbukumbu ya miaka 101 ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah, na kuuamsha Ummah kwenye wajibu wake, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika wiki ya pili ya mwezi huu wa Rajab 1443 H iliandaa, katika mji mkuu, Khartoum, na miji mbalimbali ya Sudan, amali mbalimbali, ambapo maelfu ya nakala za bendera ya tatu ziligawanywa katika masoko na maeneo kwa umma katika miji anuwai ya nchi zenye maneno yafuatayo:

Kutokana na kanuni za mfumo wa serikali chini ya Dola ya Khilafah: 'Ubwana ni wa Shariah', na 'Mamlaka ni ya Ummah'. Kwa hiyo, fikra za ubwana wa sheria ya watu, uasisishaji wa mabaraza ya kutunga sheria, usimamizi wa jeshi juu ya nchi, na unyakuzi wao wa mamlaka ya Umma. Yote haya ni hali ya batili ambayo lazima ibadilishwe kwa msingi wa Uislamu.

Mashababu wa Hizb pia waliandaa hotuba za halaiki katika maeneo tofauti tofauti

- Alama Ishara za Kampeni -

#أقيموا_الخلافة

#الخلافة_101

ReturnTheKhilafah#

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu