Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Hotuba za Halaiki dhidi ya Muundo wa Makubaliano katika Msikiti Mkuu jijini Khartoum - Siku ya Kwanza

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan iliandaa hotuba za halaiki dhidi ya muundo wa makubaliano ya katika Msikiti Mkuu wa Khartoum mnamo siku ya Jumatatu sawia na 02/01/2023 M, baada ya swala ya adhuhuri, kukataa makubaliano ya mfumo unaoanzisha maisha nchini Sudan kwa msingi wa itikadi ya Magharibi Kafiri na kuondosha hukmu za Uislamu ziliyobakia katika maisha na jamii, katika mlango wa kuamrisha mema na kukataza maovu, na kuwakumbusha Waislamu juu ya wajibu wa kusimamisha Sharia na kutabikisha hukmu za Mwenyezi Mungu (swt). Katika hotuba hizi, wazungumzaji walieleza hatari ya dola ya kisekula (isiyokuwa na dini) katika sehemu zake mbili, kiraia na kijeshi, kwa sababu inatenganisha dini na mifumo ya maisha na sheria, na inaujaalia utungaji wa sheria kuwa wa wanadamu katika nchi ambayo zaidi ya Asilimia 98 ya wakaazi wake ni Waislamu!

Na wakabainisha kuwa katika Uislamu aqida ya Kiislamu ndio msingi wa dola na ndio msingi wa mifumo ya maisha na msingi wa sheria, na kwamba mfumo wa utawala katika Uislamu ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume na ubwana ndani yake ni wa Sharia.

Idadi ya waliohudhuria walitamka (haki imekuja na batili imetoweka. Hakika, batili ilikuwa ni yenye kutoweka), na walifanya maingiliano na waliohutubia kwa maswali na michangio kwa ukarimu, wakithibitisha msimamo wao kukataa muundo wa makubaliano na kutangaza uungaji mkono wao kwa fikra hizi tukufu ya zilizozungumziwa kwenye hotuba.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

- Ripoti ya Picha juu ya Ufanisi wa Amali ya Hotuba za Halaiki -

Hotuba iliyozungumzwa na Ustadh Abdullah Abd al-Rahman (Abu al-Ezz) Katika Lango la Kaskazini la Msikiti Mkuu jijini Khartoum

Hotuba iliyozungumzwa Ustadh Abdel Qader Abdel Rahman Katika Lango la Kusini la Msikiti Mkuu jiji Khartoum

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu