- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Kwa Mara ya Pili, Hotuba za Halaiki Zilitolewa dhidi ya Mfumo wa Makubaliano katika Msikiti Mkuu wa Khartoum
Katika muendelezo wa kampeni dhidi ya Mfumo wa Makubaliano, Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ilitoa hotuba za halaiki kwa mara ya pili leo Jumatano tarehe 4/1/2023 M, baada ya swala ya Adhuhuri katika Msikiti Mkuu wa Khartoum, zikibainisha hatari ya fikra ya uhuru iliyodhaminiwa na Mfumo wa Makubaliano hayo.
Kwa mara hii hotuba hizi zilizungumzia juu ya kujitolea kwa wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, na kujitahidi kusimamisha Sharia na kutabikisha hukmu za Mwenyezi Mungu (swt):
Hatari ya fikra ya uhuru, kama ilivyo katika nidhamu wa kidemokrasia ya kisekula ambayo ilijumuishwa katika mfumo wa makubaliano, na kwamba lengo la uhuru huu ni kusambaratisha jamii ya Kiislamu kwa kuishambulia familia kupitia kuwapa wanawake haki ya kuwa na mahusiano nje ndoa, na kusafiri bila ya Mahram, kwani inaruhusu uasi, upotovu, ushoga, na mambo mengine yenye kuangamiza. Wakathibitisha kwamba uhuru wote huu umejengwa juu ya mikataba ya kimataifa, ambayo inagongana na aqida ya Kiislamu, hivyo Muislamu, awe mwanamume au mwanamke, ni mja wa Mwenyezi Mungu (swt), ambaye ni lazima ajifunge na amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu.
Na wakaonyesha hatari ya kuwa tegemezi kwa maelekezo ya balozi na mashirika ambayo yameegemezwa katika msingi usiyo wa Kiislamu, kama vile Umoja wa Mataifa, ambayo haijuzu kushiriki ndani yake, wala kufuata mikataba yake. Na wakavionya vikosi vya kisiasa vinavyohusiana nao, vikiwemo vya kijeshi na raia, juu ya hatari ya kutekeleza ajenda za dola hizi za kikoloni, balozi na mashirika yao. Na kwamba suluhisho msingi ni kukataa makubaliano hayo kwa kuwa kinyume kwake na Uislamu, na kufanya kazi ya kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume. Waumini walifanya maingiliano kwa kupiga takbira na tahlil, kushangilia na kutamka: (Dola zote zimefeli, Khilafah ndio suluhisho), (Hakuna njia kwetu isipokuwa kwa Uislamu) na (Sio utawala wa kijeshi wala wa kiraia, bali Khilafah ya Kiislamu).
Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
- Ripoti ya Picha juu ya Ufanisi wa Amali ya Hotuba za Halaiki / Siku ya Pili -
Hotuba iliyotolewa na Ustadh Abdullah Hussein
Katika Lango la Kusini la Msikiti Mkuu jijini Khartoum
Hotuba iliyotolewa na Ustadh Ahmad Abbakar
Katika Lango la Kaskazini la Msikiti Mkuu jijini Khartoum
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/sudan/2983.html#sigProId021d043c07
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan