Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Mkutano wa Waandishi Habari mjini Port Sudan

“Suluhisho Linatoka Ndani”

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya mkutano na waandishi wa habari uliofaulu wenye kichwa: “Mgogoro wa Sudan...Suluhisho Linatoka Ndani,” mnamo siku ya Alhamisi, 8 Dhul-Qa'adah 1445 H sawia na 16 Mei 2024 M, katika ukumbi wa mikutano, katika Hoteli ya Al-Basiri Plaza mjini Port Sudan.

Ukumbi ulifurika wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, huku ukihudhuriwa na mameya kadhaa, wasimamizi, wasomi na wale wanaopenda masuala ya umma, ambao walikaribishwa na afisa wa jukwaa, Ahmed Abkar, wakili na mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan.

Hizb ilianza mkutano huo kwa aya za Qur'an Tukufu, zilizozungumzia masuala ya utawala, hatari na umuhimu wake, zilizosomwa na Sheikh Yusuf Zakaria Adam.

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan iliwasilisha waraka ambao iligundua mgogoro ambao nchi inapitia na kuwasilisha masuluhisho msingi kwake. Waraka huo, ambao ulisomwa na msaidizi wa msemaji rasmi wa Hizb, Ustadh Muhammad Jami' (Abu Ayman), alieleza kuwa vita hivyo vya maafa na visivyo na maana na kuandamana kwake na uharibifu, maangamivu, uhamishaji wa watu wa nchi hii, na kuanguka kwa uchumi kunatokana na sababu zake za mzozo wa kisiasa kimsingi inasababishwa na mapambano ya kimataifa ya ushawishi kati ya dola za kikoloni za Marekani na Uingereza, ambapo Marekani iliagiza vibaraka wake wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na vikosi vya jeshi kuanzisha vita ili kuwatenga vibaraka wa Uingereza wanaojumuisha vikosi vya kiraia, haswa Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko (bila aibu), ambao walikuwa karibu na mamlaka, na udhibiti wa karibu wa vikosi vya jeshi ikiwa watafanikiwa kutekeleza Muundo wa Mkataba unaolenga kuunda taasisi ya kijeshi na usalama ili usimamizi wake uwe chini ya vikosi vya kiraia. Kisha waraka huo ulizungumzia uhasama wa kikabila na ambao ulitokana na vita hivi, ambayo kwayo watu walipanga mstari na ambavyo vilikuwa nia ya kumwaga damu iliyoharamishwa, kwa hiyo Muislamu akafanya kuwa halali kwa Muislamu kumwaga damu ya nduguye Muislamu.

Hizb imesisitiza kuwa sababu ya migogoro hiyo ni mfumo wa kibepari wa kikoloni wa kidemokrasia na kwamba migogoro hii inaweza tu kutatuliwa kupitia Aqida (itikadi) ya watu wa nchi hii na mfumo mtukufu wa Uislamu ambao ni hukmu ya Mola Mlezi wa walimwengu.

Hizb ilidhihirisha kwamba suluhisho lipo katika kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, kwa kutoa bayah (kiapo cha utii) kwa khalifa ambaye atasimamisha Dini na kutekeleza Sharia. Waraka huo ulieleza kuwa kutofanya kazi ya kusimamisha Khilafah ni dhambi kubwa, kama Mtume (saw) alivyosema: «مَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَةً جَاهِلِيَةً  “Yeyote anayekufa na hana katika shingo yake bay’ah (kiapo cha utiifu) amekufa kifo cha Kijahiliya ( Zama kabla ya Uislamu).” Bayah ni kwa khalifa wa Waislamu duniani pekee.

Mkutano huo ulishuhudia maingiliano ya hali ya juu, maswali, na mijadala mikali. Pia ulichapishwa na idadi kubwa ya magazeti na tovuti za habari, zikiwemo: (za Kiarabu)

1- Port Sudan Today: “Hizb ut Tahrir: Jeshi lazima likabidhi madaraka na kurudisha Khilafah ya Kiislamu”.

2- Fawry News: (ilichapisha hotuba nzima ya mkutano).

3- Al-Raed News: “Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Tunafanya kazi ya kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume”.

4- Al-Hakim News: ilichapisha video ya mkutano huo moja kwa moja kwenye ukurasa wake wa Facebook, ambao una wafuasi 223,000.

5- Atheer News: “Hizb ut Tahrir: Jeshi lazima likabidhi madaraka na kurudisha Khilafah ya Kiislamu”.

6- Sudanese Brief: Ilichapisha hotuba nzima ya mkutano huo chini ya kichwa: "(The Sudanese Brief) yachapisha maandishi kamili ya hotuba ya msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir."

7- Azza Press: Kichwa: (Mabishano katika Mkutano wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan baada ya kutangaza kuanzishwa kwa Khilafah ya Kiislamu kama suluhisho msingi la mgogoro wa Sudan).

8- Abu Daha News: “Hizb ut Tahrir: Kupata dola ya Khilafah ni wajibu wa kila Muislamu” kama ilivyoelezwa katika toleo lililo mwishoni mwa makala nzima.

9- Shirika la Habari la Sudan (SUNA): “Hizb ut Tahrir: Tunafanya kazi ili kuasisi dola ya haki na wajibu”.

10- Al-Hayat Press: “Hizb ut Tahrir: Suluhisho la Mgogoro wa Sudan Linatoka Ndani”.

11- Al Hurriya Net: Kichwa: Hotuba ya msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan katika mkutano na waandishi wa habari mjini Port Sudan.

Ilichapishwa chini ya kichwa chengine: "Chama cha Ukombozi cha Sudan: Suluhisho la mgogoro wa Sudan ni kurudi kwenye imani".

12- Al-Balad News: “Hizb ut Tahrir: Tunafanya kazi ya kuasisi dola ya haki na wajibu kwa mujibu wa mafundisho ya Sharia ya Kiislamu”.

13- Sudan Pulse.

Net: "Hizb ut Tahrir yaibua mabishano makali kwa kuanzisha tena mradi wa "Dola ya Khilafah".

14- Gazeti la Sudan Al-Intibaha: Hotuba nzima iliripotiwa chini ya kichwa: Hotuba ya msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan... katika mkutano na waandishi wa habari mjini Port Sudan chini ya kichwa: “Mgogoro wa Sudan... suluhisho hutoka ndani”.

15- Times News: “Hizb ut Tahrir: Vita vya sasa hivi ni vya kisiasa na havina uhusiano wowote na jihad”.

16- Hebron News: Hotuba ya msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika mkutano na waandishi wa habari mjini Port Sudan "Mgogoro wa Sudan...suluhisho linatoka ndani."

17- Al-Jumhuriya Net: “Hizb ut Tahrir: Mfumo wa kimataifa haumheshimu yeyote, na suluhisho linaweza kupatikana ndani na kupitia kutekeleza Sharia”.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah of Sudan


Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu