Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Hizb ut Tahrir Imekoleza Kampeni zake za Kujenga Ufahamu na Kuunganisha Ummah

Kwa kuzingatia muongozo wa chama kushiriki katika maslahi ya Ummah, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, eneo la Omdurman Magharibi, ilifanya warsha kubwa ya kisiasa mnamo 14, Disemba 2019 kwa anwani: “Matatizo ya Kijiji cha Al-Ikhlas yapo baina ya Dola ya Ustawi na Dola ya Ukusanyaji”, ambayo ilipokelewa kwa maingiliano na uchangamfu mkubwa. Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil) pamoja na Ustadh Muzammil Seddik, waliizungumzia, na waliwasilisha kupitia hotuba zao mtazamo wa kina juu ya suala la kijiji cha Al-Ikhlas.

Jambo jema zaidi ni kwamba kulikuwepo na mkusanyiko mkubwa uliojumuika katika kijiji cha Al-Ikhlas kumpokea msemaji rasmi wa chama pamoja na waliojumuisha wazee wengi wa kijijini hapo, viongozi wenye usemi na kukubalika fikra na mawazo yao, na watu wengine maarufu.

Ijumaa, 23 Rabi Al-Akhir 1441 H sawia na 20 Disemba 2019 M

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah ya Sudan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 16 Mei 2020 07:06

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu