Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ripoti ya Jukwaa la Masuala ya Ummah la Kila Mwezi:

Wingi wa Majeshi na Wanamgambo ni Ishara ya Kuangamia kwa Dola, kwa hivyo ni ipi Njia ya Kutokea?


Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ilifanya Jukwaa la Kila Mwezi la Masuala ya Ummah, mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 5 Jumada Al-Akhir 1446 H sawia na tarehe 7 Disemba 2024 M lenye kichwa: Wingi wa Majeshi na Wanamgambo ni Ishara ya Kuangamia kwa Dola, kwa hivyo ni ipi Njia ya Kutokea?”

Wazungumzaji walijumuisha wafuatao: Ustadh Nasser Ridha Muhammad Othman, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan. Ustadh Ahmed Abkar, Wakili, Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan. Afisa wa Jukwaa alikuwa Sheikh Abdul Jalil Adam, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Ustadh Nasser Ridha alizungumza kuhusu historia ya kuanzishwa kwa wanamgambo na vuguvugu la silaha nchini Sudan, malengo yao, na uungaji mkono wa nje kwao, na jinsi walivyowakilisha matukio mashuhuri zaidi ya mzozo kati ya dola za kikoloni juu ya ushawishi nchini Sudan, haswa kati ya Amerika na Uingereza. Alieleza kuwa hatari za wanamgambo hao ni pamoja na kueneza mapigano ya kikanda na kikabila na kuisambaratisha nchi kwa jina la shirikisho, kujitawala, na kile kinachoitwa kujiamulia wenyewe. Pia alieleza kwamba walimpa nguvu mkoloni kafiri katika ardhi yetu. Alieleza kuwa serikali zinashiriki katika uhalifu wa kuunda majeshi hayo kwa kuwapa uhalali na kwa kuwatambua kupitia wazo la kugawanya mamlaka na mali na kugawanya nao nyadhifa za kiutendaji na kuwapa silaha kwa yale yanayowatia nguvu na kuwa hatari kwa wananchi.

Mzungumzaji wa pili, Mwanasheria Ahmed Abkar alieleza Hukm Shari' inayohusiana na wingi wa majeshi, na akaeleza uharamu wa hilo kwa ushahidi wa Sharia, na akaeleza kwamba jeshi katika Uislamu ni jeshi la dola pekee, na kwamba Khalifah ni kamanda halisi wa jeshi, na yeye ndiye anayewateua makamanda wa vitengo na brigedi, na akaeleza kuwa matakwa katika Uislamu hayatokani na kuinua silaha bali ni kazi ya kisiasa yenye msingi wa Uislamu. Jeshi hilo ni jeshi moja, likiwemo la usalama wa ndani na polisi. Na Dola ya Khilafah haitaruhusu kuanzishwa kwa wanamgambo au vuguvugu lolote linalotishia usalama wa watu na kusababisha maafa na majanga kama ilivyotokea kwa Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) na kile kinachotokea leo kwa utambuzi wa serikali ya wanamgambo na harakati za silaha. Kwa hivyo uhalisia huu hautabadilishwa isipokuwa kwa kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo ndiyo suluhisho na njia ya kutoka katika machafuko ya wanamgambo na harakati za silaha zinazotokea leo.

Katika sehemu ya maingiliano, kulikuwa na uingiliaji kati mkali na mijadala mikali kutoka kwa wataalamu kadhaa wa vyombo vya habari na wanasiasa juu ya mada hiyo, haswa mtaalamu mkongwe wa habari na mwanahabari, Bw. Asim Al-Bilal, Naibu Mhariri Mkuu wa Gazeti la Akhbar Youm, Bw. Mohamed Abdullah, Mhariri Mkuu wa zamani wa Gazeti la Sudan Vision, Dkt. Zuhair Abdel Rahman, mtaalamu wa masuala ya habari na uchumi, na Ust. Hatem Jaafar, wakili na mshauri wa sheria. Wazungumzaji walijibu uingiliaji huo kwa njia imara na maridadi.

Mwishoni mwa kongamano hilo, afisa wake, Ust. Abdul Jalil Adam, aliwashukuru waliohudhuria kwa ushiriki wao, maingiliano makubwa, na usikivu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Kalima na Ustadh Nasser Ridha

Hatari ya Wingi wa Majeshi na Wanamgambo

Kalima ya Wakili na Ust. Ahmed Abkar

Jeshi katika Uislamu: Vigezo, Shabaha na Malengo

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu