Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Mkao wa Kadhia za Ummah "Bwawa la Mwamko"

Hizb ut Tahrir / Wilaya Sudan ilifanya mkao wake wa kila mara, mkao wa kadhia za Ummah, siku ya Jumamosi 4 Dhu al-Hijjah 1441 H sawia na 25/7/2020 M, na ambao ulikuwa kwa anwani:

Bwawa la Mwamko: Kupotea kwa Haki za Ummah Chini ya Kivuli cha Kukosekana Ngao ya Imam

Waliozungumza katika mkao huu ni:

  • Ustadh Abdullah Abdulrehman (Abu Al-Izz) – Mwanachama wa Baraza la Wilaya la Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan.
  • Ustadh Nasser Ridha (Abu Ridha) – Raisi wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan.

Mwanzoni mwa kalima yake, Ustadh Abdullah Abdulrehman alizungumzia kuhusu dori ya Hizb ut Tahrir katika hamu yake kwa kadhia za Ummah, na akaashiria idadi kadhaa ya kadhia nyeti ambazo Hizb imezitabanni; na miongoni mwao ni kadhia ya kutenganishwa kwa eneo la (Sudan) Kusini, na akasema: Baadhi ya wanahabari waliandika, pindi Hizb ilipozungumzia uhalifu wa utenganishaji huo kupitia maandamano, makongamano, matoleo, mihadhara, na hotuba tofauti tofauti na visimamo na utiaji mamilioni ya saini, wanahabari hawa wakasifia kwamba Hizb ut Tahrir inaimba nje ya kundi, na akasema: Na pindi utenganishaji ulipotokea kivitendo na hali za watu kuwa hawakubainisha maneno yangu hadi mchana wa kesho, na akataja kwamba Hizb ilizungumzia kadhia ya bwawa la mwamko tangu zamani sana na akabainisha kwamba Hizb ilitoa kijitabu tangu mwaka wa 2017 M kwa anwani: "Bwawa la Mwamko: Nadhiri ya Vita vya Maji Uzembe wa Watawala na Wajibu wa Ummah", na akakinyanyua kitabu hiki mbele ya waliohudhuria, na akasema: hakika kijitabu hiki ndani yake mna ufichuzi na ubainifu kikamilifu kwa kadhia ya bwawa la mwamko, na akasema: hakika Hizb imekifikisha kitabu hiki kwa serikali mbili iliyoko sasa na iliyo tangulia, na akasema: kitabu hiki asili ni kuwa hivi sasa kinatakiwa kiwe kwa Al-Burhan, na kiwe kwa naibu wake, na kiwe kwa Waziri wa Kigeni aliye tangulia, na Profesa Yassir Abbas waziri wa sasa, na kiwe kwa Waziri Mkuu Hamdouk, kama ambayo Hizb ilifanya mikao na hotuba nyingi na vidokezo vya mazungumzo katika suala hili.

Muhammad Jameh (Abu Ayman)

Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Wilaya Sudan

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 28 Julai 2020 16:48

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu