Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uswidi: Kisimamo kwa Anwani "Sitisheni Uhamisho wa Odiljon Jalilov"

Hizb ut-Tahrir nchini Uswidi iliandaa kisimamo mbele ya Idara ya Uhamiaji ya Uswidi kutaka kusitishwa kwa uhamisho wa Ndugu Odiljon Jalilov, ambaye alizuiliwa na polisi wa Uswidi jioni ya 29 Oktoba 2021 M, kwa ajili ya maandalizi ya kuhamishwa kwake hadi Uzbekistan, ambayo ina historia ndefu na inayojulikana sana kwa ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa, na mbaya zaidi dhidi ya wapinzani wa Kiislamu miongoni mwa mashababu wa Hizb ut-Tahrir.

Mashababu wetu wameteseka kwa miongo kadhaa kutokana na vifungo virefu gerezani, unyanyasaji, mateso na hata kuuwawa mashahidi nchini Uzbekistan. Vyanzo kutoka kwa familia ya Odiljon Jalilov nchini Uzbekistan vinasema kuwa polisi wa Uzbekistan wamekuwa wakiwasiliana na familia yake na kuwafahamisha kuwa Odiljon Jalilov atarejea hivi karibuni. Kisimamo hicho kilisisitiza kwamba kufukuzwa na kusalimishwa kwa Ndugu Odiljon Jalilov, kwa utawala dhalimu wa Uzbekistan kunawakilisha tishio la kweli kwa maisha yake, ambayo mamlaka ya Uswidi itawajibikia.

Ijumaa, 07 Rabi' ul-Akhir 1443 H sawia na 12 Novemba 2021 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Sweden:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Sweden

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / sweden

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu