Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Kongamano la Kila Mwaka (2022): “Ruwaza ya Kiuchumi ya Hizb ut Tahrir”

Ulimwengu wa leo ungali unaishi juu ya athari za mgogoro mpya wa kiuchumi. Bali, ungali unaendelea kuungua kutokana na masuluhisho maovu na kuwa mbali kutokana na maudhui makubwa ya uchumi, haswa chini ya utawala wa mfumo wa kirasilimali wa kiulimwengu na benki zake na mifuko yake ya fedha ya kimataifa zinazodhibiti njia za dola, serikali na watu, na kwamba migogoro inayotokana na utabikishaji wa urasilimali, pamoja na yale Tunisia inayoyapitia, itaendelea maadamu wanadamu hawatarudi kwenye njia na kutambua njia ya wokovu wake, kwani hawaufikii na kamwe hautafikiwa isipokuwa kwa kutabikishwa Uislamu na mfumo wake adilifu wa kiuchumi na masuluhisho yake halisi ya kiwahyi. Kutokana na haya, ilikuwa ni wazi kwamba matatizo ya umaskini wa watu na kufilisika kwa serikali, kwa hakika, yanaakisi mgogoro wa mfumo ambao haufai tena kuchunga mambo ya watu, na kwamba dola ya kitaifa inayoyumba si dola tena ya uchungaji bali ni dola ya ukusanyaji ushuru inayoendeshwa na wafanyakazi na madalali katika taasisi za riba za kimataifa, na kwa hiyo yeyote anayebeba njia mbadala ya kiuchumi iliyosimama juu ya msingi wa Uislamu, asitumie juhudi zozote katika kudhihirisha ruwaza yake ya uchumi na kuwasilisha ruwaza hii kwa watu kama suluhisho na tiba halali ya kisheria yenye kutimiza wajibu wa kisheria na kubadilisha uhalisia wa kisiasa kwa wakati mmoja, mradi tu uchumi ndio anwani ya mgogoro.

Katika muktadha huu, Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia ilichagua kuwa Kongamano la kila mwaka la Khilafah, liwe kongamano la kiuchumi kwa ubora wake, lenye kichwa:

"Ruwaza ya Kiuchumi ya Hizb ut-Tahrir"

Ambapo linaangazia ndani yake hali ya kiulimwengu ya mgogoro wa kiuchumi, na sababu halisi zilizosababisha mgogoro nchini Tunisia. Kisha, linawasilisha jinsi Uislamu unavyotatua matatizo ya umaskini, ukosefu wa ajira, na madeni, na kutoa mipango mipana ya sera ya pesa na fedha katika dola ya Khilafah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Jumamosi, 26 Dhul-Qa’adah 1443 H - 25 Juni 2022 M


Ili Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari Iliyotolewa na

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia

Ya Kulitangazia Kongamano la Kiuchumi kwa Anwani:

“Kongamano la Kila Mwaka la Khilafah la Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Jumatatu, 22 Dhul-Qa’adah 1443 H - 21 Juni 2022 M

Bonyeza Hapa

- Video Kamili ya Amali ya Kongamano la Khilafah la Kila Mwaka -

Kongamano la Kila Mwaka la Khilafah 2022:

Ruwaza ya Kiuchumi ya Hizb ut Tahrir lililofanywa nchini Tunisia

Hizb ut Tahrir/ Wilayah Tunisia ilifanya kongamano mnamo Jumamosi 26 Dhu al-Qa’dah 1443 H sawia na 25 Juni 2022 M. Kundi la wasomi na wataalamu walikuja kutoka nchi mbalimbali ili kuwasilisha masuluhisho ya kimsingi yatakayotatua mgogoro wa kiuchumi. Utenganishaji dini na dola, umewafanya watu wa Tunisia kuteseka kutokana na umasikini, maradhi, ukosefu wa ajira na uchungaji duni.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

- Video ya Kualikia Kongamano (1) -

- Video ya Kualikia Kongamano (2) -

- Video ya Kualikia Kongamano (3) -

- Video ya Kualikia Kongamano (4) -

- Video ya Kualikia Kongamano (5) -

- Video ya Kualikia Kongamano (6) -

- Video ya Kualikia Kongamano (7) -

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu