Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Kisimamo cha Ezz “Miaka 12 Tangu Mapinduzi na Serikali Ingali Haijaporomoka

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia yaandaa kisimamo cha Ezz kwa anwani “Miaka 12 Tangu Mapinduzi na Serikali Ingali Haijaporomoka... Hakuna Wokovu Isipokuwa kwa kupitia Mfumo wa Dola ya Kiislamu, Dola ya Khilafah Rashida

cha kulingania kung'olewa kwa ushawishi wa ukoloni kwa nguzo, zana na mfumo wake uliowafanya watu kuonja taabu, mateso na ugumu wa maisha...

Kuweni pamoja nasi katika miadi hii ...

Jumamosi, 21 Jumada ul-Akhir 1444 H – 14 Januari 2023 M

- Sehemu ya Amali ya Kisimamo -

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Kisimamo cha Ezz... “Miaka 12 Tangu Mapinduzi na Serikali Ingali Haijaporomoka”

(Imetafsiriwa)

Katika kumbukumbu ya miaka kumi na mbili ya kutoroka kwa Ben Ali aliyebanduliwa madarakani, na katika ukumbusho wa vuguvugu la umati ambalo watu wa Tunisia walifanya usiku wa kuamkia Januari 14, 2011, na licha ya majaribio yote ya serikali ya kuwapigisha magoti wananchi na kuzima moto wa mapinduzi, na kutia giza nembo ya mahali na zama, Hizb ut Tahrir katika wilaya ya Tunis ilifanya matembezi katikati ya mji mkuu, ikiweza kupitia matembezi hayo kufika kwenye barabara kuu ya mapinduzi, ikiungana pamoja na wananchi na kukwepa mzingiro mkubwa wa usalama na vizuizi vilivyowekwa kwenye barabara mbalimbali zinazoelekea kwenye barabara hii kuu, ambapo mashababu wa hizb walinyanyua bendera za Al-Raya na Al-Liwaa huku wakishangilia na kupiga takbira, kama ambavyo mashababu hao wa hizb walibeba miito ya matembezi hayo iliyo andikwa kwa herufi zenye wino mzito: "Mapinduzi ya Ummah yanaendelea ili kupindua serikali na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume."

Wakati wa kisimamo chake kwenye Barabara ya Al-Thawra, hizb iliwasilisha jumbe za kisiasa kwa kwa ajili ya rai jumla, kupitia kauli mbiu na michangio ya mashababu wake kadhaa. Mchangio mkuu ulifanywa na Ustadh Khabib Kerbaka, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, ambaye alitoa wito moto kwa watu wa Al-Zaytouna kuzunguka pambizoni mwa Uislamu kama badali ya kihadhara na msingi wa mabadiliko msingi na njia pekee ya kukamilisha mapinduzi ya Umma dhidi ya tawala za kutenza nguvu akiwaonya juu ya hali nzima ya kisiasa inayolingania kupinduliwa kwa rais wa utawala huo, Qais Saeed, ili mmoja wao aweze kumuwakilisha katika utumishi wa ajenda ya ukoloni, akiwataka wakose fursa hiyo kwa waviziaji wa mapinduzi kutoka kwa nguvu ya ukoloni wa kimataifa na taasisi za uporaji za kimataifa.

Karbaka pia alisisitiza kupitia mchangio wake kwamba njia pekee ya kihadhara yenye uwezo wa kuamsha Umma, kuunganisha, na kujumuisha nia yake ya kukomboa na kujikomboa kutoka kwenye shingo ya ukoloni na kupata ubwana wa kweli na wenye ufanisi, ni dola ya Khilafah Rashida ambayo Mtume (saw), aliibashiria Umma huu mtukufu.

Na katika yale yaliozungumzwa na kima kaka wawili Omar al-Arabi na Muhammad Ali al-Awni juu ya ishara ya mahali hapa ambapo koo za wanaotaka mabadiliko ya utawala zilipasuka, na juu ya umuhimu wa kuzunguka pambizoni mwa Uislamu na walinganizi wake wa kimfumo, baada ya kufeli (Uislamu wa wastani) ili kuwadhibiti watu hawa, ambao hatimaye waliitikia wito wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia wa kususia uchaguzi wa Kidemokrasia, Bi Souad Khashram alitoa mchangio kuhusu dhulma ya utawala huu fisadi kwa wanawake, dharau yake kwa hadhi yake na kukanyaga utukufu wake. Na kwa hivyo,  ikafikisha ujumbe wake kwamba sio sawa kwa wanaume na wanawake wote, vijana na wazee, kukaa kimya kuhusu dhulma na ulegevu wa kusimamisha dola ya uadilifu, dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. michangio hii ilifuatiwa na shangwe zenye kutaka kupinduliwa kwa utawala mzima na kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu, Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kisha, mashababu wa hizb wakaandamana kuelekea Ubalozi wa Ufaransa, ulioko katika barabara hii hii, wakibeba kauli mbiu: "Watu wanataka kupindua ukoloni."

Kamera za vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi hazikuweza kupita kisimamo hiki muhimu katika Barabara ya Al-Thawra, kwa hivyo baadhi yao waliangazia kisimamo hiki na kuchukua baadhi ya taarifa za habari na maoni juu ya kiwango cha nidhamu na amani yake (kama ilivyoelezwa katika Diwan FM, kwa mfano), lakini baadhi ya pembe za kikoloni walikuwa wepesi kujaribu kukidogosha kisimamo hicho na kukipa sura kwamba ni sehemu ya vuguvugu la watu wengi wanaotaka kuondoka kwa Qais Saeed, ingawa kauli mbiu ya kisimamo hicho ni kuangushwa kikamilifu kwa serikali nzima na kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu juu ya magofu yake. Huu nao ni ushahidi wa ziada wa haja ya kung'oa ushawishi wa ukoloni katika nchi yetu, ili vyombo vya habari navyo vikombolewe na uingiliaji wa nje, ambao ndio sababu ya kila balaa katika nchi za Kiislamu, ikiwemo nchi ya Al-Zaytuna.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Tunisia

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu