Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wazuru Makao Makuu ya Shirika la Leba la Tunisia

Mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 06/06/2024 M, ujumbe kutoka Hizb ut  Tahrir/Wilayah Tunisia, ukiongozwa na Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri, Mkuu wa Afisi ya Kisiasa, Ustadh Yassin Bin Yahya, Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano, na Ustadh Muhammad Al-Habib Al-Hajjaji, Mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb, ulizuru makao makuu ya Shirika la Leba la Tunisia.

Ujumbe huo ulikutana na Katibu Mkuu wa shirika hilo Ustadh Muhammad Al-Asaad Obaid na kufarijiwa kuhusu hali yake ya kiafya ambayo inaendelea kuimarika, alhamdulillah.

Mkutano huo pia ulijadili hali jumla ndani na nje, hasa yale ambayo watu wetu wa Gaza na Ardhi nzima Iliyobarikiwa (Palestina) wanakabiliwa nayo kutokana na uvamizi wa umbile la kikatili la Kiyahudi chini ya mwavuli wa Mkruseda Magharibi, inayoongozwa na Marekani.

Ujumbe huo pia uliwasilisha maendeleo ya Hizb na njia yake kuelekea lengo linalotarajiwa, kuanzisha tena maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ujumbe huo unamshukuru Katibu Mkuu wa Shirika la Leba la Tunisia, Ustadh Mohamed Al-Assaad Obaid, kwa mapokezi yake mazuri, makaribisho na nia yake ya kuhuisha mkutano huu.

Alhamisi, tarehe 29 Dhul-Qi’dah 1445 Hijria inayolingana na tarehe 6 Juni, 2024 Miladia.

Alhamisi, 29 Dhu al-Qa’adah 1445 H sawia na 06 Juni 2024 M

- Sehemu ya Amali ya Ziara -

2024 06 06 TNS WAFD PIC

- Alama Ishara za Amali -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu