- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi “Njia ya Ukombozi wa Palestina… Maandamano ya Umma na Kupinduliwa kwa Mafirauni wa Zama Hizi!
Matembezi ya 41 mfululizo tangu kuanza kwa Vita vya Kingunga cha Al-Aqsa yalifanyika mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu Tunis, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, watu wa Zaytouna na kichwa chake kilikuwa “Njia ya kuikomboa wa Palestina... maandamano ya Umma na kupinduliwa kwa Mafirauni wa zama hizi!” Kama vile yaliotangulia, yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu, ambapo walizunguka katika barabara za mji mkuu kuelekea Barabara ya Al-Thawra, mabango yaliinuliwa huku bango kuu likiandikwa: Faradhi ya Jihad na ukombozi wa Palestina unakungojeni... basi je mutafanya nini?” Bango jengine lilionyesha takwimu za mashahidi na waliojeruhiwa, na kama kawaida, koo za wahudhuriaji zilikuwa zikinguruma na kuimba wakati wote wa maandamano, miito kama vile “Enyi majeshi ya Umma, tuondoleeni wingu,” “Kueni, enyi majeshi, viangamizeni viti hivi vya enzi,” “Enyi watawala wa aibu, Gaza iko chini ya moto,” na kauli mbiu nyingine zinazowahimiza wanyoofu miongoni mwa Maafisa wa jeshi kutaharaki kuinusuru Gaza na kupindua viti vya ukandamizaji kutoka kwa watawala wa Waislamu na matembezi hayo yalihitimishwa kwa kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu hizb ambapo aliwataka wananchi wa Tunisia hususan na Waislamu wote wajibu wa kuwanusuru ndugu zao wanaodhulumiwa nchini Palestina na udharura wa kufanya kazi ya kusimamisha dola ya Khilafah Rashida pili kwa njia ya Utume.
Hivyo basi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inaendelea na kazi yake isiyochoka na endelevu tangu kuzuka kwa cheche za Kimbunga cha Al-Aqsa katika kuuhimiza Umma kuwanusuru ndugu zao na kubainisha suluhisho la kisheria kwa kuyakusanya majeshi hasa baada ya kupita miezi tisa ambapo matukio na uhalisia umethibitisha kwamba hakuna wokovu kwa Gaza na kina dada wa Gaza kama Arakan (Myanmar) na Uzbekistan Mashariki ya Turkestan, Syria, na Yemen, isipokuwa kwa kusimamisha jengo kubwa la Uislamu upya, katika kusadikisha wa bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), "... ثم تكون خلافة على منهاج النبوة" “... Kisha itakuwepo Khilafah njia ya Utume.”
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Ijumaa,13 Dhu al-Hijjah 1445 H sawia na 19 Juni 2024 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
-
View the embedded image gallery online at:
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/4119.html#sigProIdd5cf6727c0
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia