Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Ombi la Kiongozi wa Mashtaka la Kuwafunga Wanachama 4 wa Hizb ut Tahrir Miaka 52.5 kwa Jumla

 

Kiongozi mmoja wa mshtaka aliomba kifungo cha miaka 52.5 kwa jumla kwa wazungumzaji 4 wa kongamano moja ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika mnamo 2017 lakini likazuiwa pasi na sababu msingi.

Kongamano hilo lilipangwa kufanyika mnamo 5 Machi 2017 kwa anwani: "Kwa nini ulimwengu wahitaji Khilafah" lilizuiwa pasi na sababu yoyote ya maana, na mashtaka yakafunguliwa dhidi ya wazungumzaji MAHMUT KAR, ABDULLAH IMAMOGLU, MUSA BAYOGLU na OSMAN YILDIZ.     

Wakati wa mashtaka hayo yaliyofanywa mnamo 27/11/2020 na Mahakama Kuu ya Jinai ya 30 ya Istanbul kiongozi wa mashtaka aliomba miaka 52.5 kwa jumla kwa watu 4 kwa tuhuma za "kuwa mwelekezi na mwanachama wa Hizb ut Tahrir" na "kuunda propaganda ya Khilafah".

Kwa ombi hili la Kiongozi wa mashtaka, kulikuwa na majibu mengi kutoka kwa makundi tofauti ya jamii wakiwemo wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, magazeti, wavuti, mawakili na waandishi.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Uturuki

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 10 Disemba 2020 15:02

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu