- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Amali za Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ili Kuwanusuru Watu wa Turkestan Mashariki
Hizb ut Tahrir/ Wilayah Uturuki iliandaa amali za kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuwanusuru watu wa Turkestan Mashariki ambapo wanakandamizwa kwa mikono ya Wachina kwa anwani, “Nani Ataipa Nussrah Turkestan Mashariki… Nani Atasitisha Ukandamizaji wa Uchina?!” Ilifanyika baada swala ya Juma’ katika miji saba.
Ijumaa, 16 Rabii' al Akhir 1441 H - 13 Disemba 2019 M
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI iliyosomwa katika mikutano kwa vyombo vya habari
"NANI ATAISAIDIA TURKESTAN?! NANI ATAKAYEMZUIA DHALIMU WA UCHINA?!"
WAISLAMU WA UTURUKI HAWAKUBAKIA KIMYA KWA UKANDAMIZAJI WA UCHINA!
Umati wa Waislamu ulijitokeza katika mikutano kwa vyombo vya habari iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki katika mikoa saba ya Uturuki, iliyofanyika kwa anwani, “Nani Atakayeisaidia Turkestan?! Nani Atamzuia Dhalimu wa Uchina?!”
Tofauti na watawala katika ardhi za Waislamu, Waislamu waliilaani serikali ya kikomunisti ya Uchina, ambao inawatesa ndugu zao Wauyghur na kuwalingania watawala wao kuchukua hatua badala ya kunyamaza kimya.
Mikutano kwa vyombo vya habari ndani ya Adana, Ankara, Gaziantep, Hatay, Istanbul na Mersin ilifanyika mnamo Ijumaa, ilhali mkutano na vyombo vya habari ndani ya Izmir ulifanyika mnamo Jumapili, 15 Disemba 2019.
Mkutano kwa vyombo vya habari ulioandaliwa na Hizb ut Tahrir ndani ya Adana katika Msikiti wa Mkubwa wa Adana taarifa ilisomwa na Metin Inalpulat.
Ndani ya Ankara ilisomwa na mwandishi wa Köklü Değişim na mwanatheolojia Abdullah Imamoglu katika Msikiti wa Melike Hatun. Mkutano kwa vyombo vya habari ulihudhuria na mashirika yasiyokuwa ya serikali na wawakilishi wa vyama kama vile Mazlumder, Yeni Dünya Vakfı, na Hüdapar.
Mkutano kwa vyombo vya habari uliokuwa umepangwa kufanyika katika Msikiti Mkubwa, lakini ukahamishwa katika Mbuga ya Kırkayak baada ya Gavana wa Gaziantep kukata kutoa idhini. Taarifa ilisomwa na Ferhat Okur.
Hizb ut Tahrir ndani ya Hatay ilisoma taarifa katika Msikiti wa Antakya Küçük Sanayi Sitesi. Ilisomwa na Oğuzhan Yalçın.
Taarifa kwa vyombo vya habari ndani ya Istanbul ilitangulizwa na Ramazan Gümüş, na kusomwa na mwandishi wa Köklü Değişim, Musa Bayoğlu mbele ya Ubalozi wa Uchina Istanbul. Kwa kuongezea, Mr. Erdal Elibüyük, Mkuu wa Mkoa wa Hüdapar Istanbul (chama cha kisiasa); Mr. Burhan Kavuncu, Rais wa Wakf wa Turkestan; Hamza Er, Mwenyekiti Muasisi wa Aksa İlim ve Davet Merkezi (Kituo cha Aksa cha Ilm and Dawah); Ali Öner, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mazlumder Istanbul (NGO), na mwandishi wa Köklü Değişim, Muhammed Hanefi Yağmur, walitoa hotuba fupi fupi. Tukio liliisha kwa kisomo cha Qur’an kutoka kwa Hafidh Salih Yakut.
Mkutano kwa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir ndani ya Mersin ulifanyika katika Msikiti Mkubwa wa Mersin.
Taarifa ilijumuisha kauli zifuatazo:
“Leo zaidi ya ndugu zetu Waislamu milioni 5 Wauyghur wanateswa kimwili na kiakili ndani ya kambi zilizojaa.Familia za Waislamu hawa milioni 5 wanakabiliwa na mateso zaidi. Kwani wanaume Wachina wamewekwa ndani ya kila nyumba pasina kuzingatia faragha ya familia.
Vilio ndani ya Turkestan Mashariki vinatikisa mbingu, je munavisikia? Mayowe ya kuomba msaada kutoka kwa ndugu zenu imetanda angani, je munayasikia? Ndugu zetu Waislamu wa Turkestan Mashariki wanauliwa – sio polepole, bali kwa haraka pasina huruma, je munawaona?
Nani atasitisha ukandamizaji huu! Umoja wa Mataifa? Watawala wa ulimwengu wa Waislamu?
Je sio Umoja wa Mataifa –hivi majuzi kama ambaye ni jana – waliwasalimisha Waislamu wa Bosnia kwa Masabia wauwaji? Je mauaji ya maelfu ya ndugu zetu Wabosnia kwa mikono ya Waserbia hayakupuzwa na kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa? Umoja wa Mataifa ni kikaragosi cha Amerika… Kwani wanafanya maamuzi pekee ambayo ni ya kuhifadhi maslahi ya Amerika, ambaye anaharibu ardhi za Waislamu? Hivyo basi; kuuwacha mustakbali wa Waislamu wa Turkestan Mashariki kwa Umoja wa Mataifa na kutarajia kupata suluhisho kutoka UN ina maana kuwasalimisha ndugu zetu Waislamu kwa muuaji na kuwatupa motoni huku tunafahamu.”
Je ni Pakistan, ambayo ilitoa ahadi ya ushirikiano na Uchina kuhusiana na suala la Turkestan Mashariki, ndiyo itakayositisha ukandamizaji huu? Au ni Saudi Arabia, ambayo ili tiangaza kuunga mkono “juhudi za Uchina kuhifadhi ubwana wa kitaifa, usalama na utulivu,” na inapinga “uingiliajikati katika mambo ya kindani ya Uchina”? Au ni Misri, ambayo imewarudisha Waislamu Wauyghur 6,000 kwenda Uchina au kuiruhusu Uchina kuwahoji Waislamu Wauyghur?
Au ni Rais Erdogan, aliyesema kwamba “Uturuki inapinga misimamo mikali, na ingependa kuboresha mahusiano ya kisiasa na Uchina ili kuboresha ushirikiano wa kiusalama”?
Sehemu ya mwisho ya taarifa ilikuwa ni kuwalingania Waislamu, iliyosema yafuatayo:
Enyi Waislamu!
Msibakie mmeduwaa pasina hisia kama watawala mbele ya mayowe ya ndugu zenu bali wapeni masikio yenu! Lau hata ulimwengu mzima utawatelekeza basi nyinyi hamutawawacha! Ni dharura muwahesabu watawala wenu kwa kutoitikia vilio vyao! Hasira zenu zisielekezwe tu kwa Jamhuri ya Kikomunisti ya Uchina bali pia muwalinganie watawala wenu ambao wamewatelekeza Waislamu wachukue hatua! Na fanyenikazi ya kusimamisha Khilafah Rashidah, ambayo itasitisha mateso haya na kuwahesabu madhalimu! Fanyakazi kwa juhudi zako zote ili kuurudisha Uislamu utawale maisha kwa mara nyingine. Na wanusuru wale wanaofanyiakazi lengo hili! Musisahau kwamba Mwenyezi ni Mshirika na Muungaji mkono wa Waislamu.
“Ewe Mwenyezi Mungu! Tunakuomba katika muda huu wa Juma’ ambapo Dua zote zinajibiwa. Tunasikitikia udhaifu wetu, kutokuwa na msaada na kukosa nguvu kwetu dhidi ya madhalimu. Wewe ndiye Mwenye Rehema katika wote wanaoonyesha huruma! Wewe ndiye Bwana wa madhaifu; tupe nguvu…
Tunakuomba msaada Wako kwa ajili ya ndugu zetu Waislamu. Usaidie Ummah wa Uislamu …. Ewe Mwenyezi Mungu! Wasaidie ndugu zetu wa Turkestan Mashariki!
#DoğuTürkistanaSahipÇık
Yaliyofanyika mnamo Ijumaa, 13 Disemba 2019
Istanbul – Ubalozi wa Uchina: 16:00
Ankara – Msikiti wa Melike Hatun (baada ya Swala ya Juma’)
Mersin – Msikiti wa Ulu (baada ya Swala ya Juma’)
Adana – Msikiti wa Ulu (baada ya Swala ya Juma’)
Gaziantep – Msikiti wa Oulu (baada ya Swala ya Juma’)
Hatay – Msikiti wa The Industrial Mosque (baada ya Swala ya Juma’)
• Izmir - Konak Square on Jumapili 15 Disemba (baada ya Swala ya Juma’)
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/uturuki/162.html#sigProIdc579c6bbe3