Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Halaqa ya Mjadala Mjini Tatvan Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi

Ndani ya wigo wa msururu wa makongamano, semina na halaqa zilizoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", na sanjari na mnasaba wa kumbukumbuka ya miaka 101 Hijria ya kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Muharram 1342 H, Hizb ilikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi mjini Tatvan katika mkoa wa Bitlis.

Wazungumzaji katika mkutano huo walikuwa ni maustadh; Mehmet Emin Sheman (Msimamizi wa jarida la kokludegisim katika Mkoa wa Bitlus), Suleiman Ugurlua (Mhariri Mkuu wa jarida la kokludegisim), Muhammed Hanafi Yagmur (Mtaalamu wa uchumi wa Kiislamu), na Abdullah Imamoglu (imam na khatibu).

Katika mkutano wetu, ilisisitizwa udharura wa kuwekwa masuluhisho na hukmu za Uislamu katika kila nyanja kwenye ajenda, na kwamba Uislamu una masuluhisho ya kina na ya asili katika utawala, uchumi, elimu na nyanja za kijamii, na kwamba ni lazima yabainishwe katika kila jambo.

Mkutano wetu ulimalizika kwa hamu na msisitizo juu ya udharura wa kuwekwa mikutano hii ya mashauriano na masuluhisho mara kwa mara katika maeneo yote.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Jumapili, 12 Rajab Al-Muharram 1443 H sawia na 13 Februari 2022 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu