Jumanne, 07 Rajab 1446 | 2025/01/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Kisimamo cha Kupinga Ziara ya Rais wa Umbile Nyakuzi la Kiyahudi Nchini Uturuki

Kwa kuzingatia hali ya wasiwasi katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kutokana na unyakuzi wa umbile la Kiyahudi wa ardhi hiyo iliyobarikiwa na mashambulizi yake ya kuendelea dhidi ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na kuzingirwa kwake na mashambulizi ya miaka 16 ya Ukanda wa Gaza, Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa visimamo vya kupinga dhidi ya ziara ya mhalifu Herzog, rais wa umbile nyakuzi la Kiyahudi nchini Uturuki, na kukaribishwa kwake na serikali ya kisekula nchini Uturuki, ikiwakilishwa na sura ya Erdogan, ambaye alikula njama na makafiri wa Magharibi kuizima kadhia ya Palestina kwa maslahi ya Mayahudi wanaoikalia kwa mabavu.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Jumatano, 06 Shaaban 1443 H - 09 Machi 2022 M

- Nyakati za Visimamo -

Tulikusanyika mbele ya ubalozi wa umbile la nyakuzi Kiyahudi (Israel) katika kitongoji cha Sogutozu jijini Ankara, kuandaa maandamano na kusoma taarifa kwa vyombo vya habari, saa 20:00 siku ya Jumatano, Machi 9, 2022 M.

Ili kuandamana jijini Istanbul, tulikutana mbele ya ubalozi mdogo wa umbile nyakuzi la Kiyahudi eneo la Levent saa 21:00 siku ya Jumatano, Machi 9, 2022 M.

Tuliwaalika Waislamu wote kuungana nasi katika maandamano yetu dhidi ya ziara ya mhalifu huyo na kukaribishwa kwake na serikali ya kisekula inayotawala nchini Uturuki.

- Amali za Kisimamo cha Kupinga Jijini Ankara -

(Video ya Amali za Kisimamo Jijini Ankara)

Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki, kwa neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, iliandaa kisimamo cha kupinga ziara ya Isaac Herzog (rais wa umbile nyakuzi Kiyahudi) nchini Uturuki, ambapo idadi kubwa ya Waislamu walishiriki katika amali ya kusomwa kwa taarifa kwa vyombo vya habari nchini jijini Ankara.

Baada ya takbira na tahlil, Ustadh Abdullah Imamoglu alisoma taarifa kwa vyombo vya habari yenye kichwa "Herzog Gaidi anayeukalia Msikiti wa Al-Aqsa... Ondokeni katika ardhi zetu!" Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa katika bustani ya Seğmenler Park karibu na nyumba ya wageni ya "Israel", Ustadh Imamoglu alisema,  "Rais wa umbile gaidi la Kiyahudi, Herzog, alikaribishwa kwa sherehe rasmi kana kwamba sio gaidi mnyakuzi, na mazungumzo rasmi yalitangazwa kuboresha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili huku picha za maiti za watoto wetu na mabaki yao kutoka katika Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na Gaza bado zikiwa mbele ya macho yetu. Misimamo ya joto na ya dhati imetangazwa kati ya Uturuki na rais wa umbile hili nyakuzi.

Waislamu jijini Ankara walipinga ziara ya rais umbile hilo nyakuzi la Kiyahudi Herzog kwa sauti moja na walionyesha hisia zao za hasira kwa kuimba miito kama vile "Herzog muuaji aondoke", "Herzog muuaji" na "Umma huu kiongozi wake ni Muhammad kamwe hautashindwa."

Amali hii ambayo mabango mbalimbali yaliinuliwa, yakiwemo “Hakuna atakayeukomboa Msikiti wa Al-Aqsa isipokuwa Dola ya Khilafah Rashida” ilihitimishwa kwa dua na maombi kwa Mwenyezi Mungu (swt).

- Amali za Kisimamo cha Kupinga Jijini Istanbul -

(Video ya Amali za Kisimamo Jijini Istanbul)

Huku ikipinga ziara ya rais gaidi wa umbile vamizi la Kiyahudi, Isaac Herzog, nchini Uturuki, Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki, kwa neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, iliandaa kisimamo cha kupinga mbele ya ubalozi mdogo wa umbile la Kiyahudi huko Levent, Istanbul.

Katika kisimamo hicho cha kupinga ziara ya mhalifu Herzog, watawala waliomwalika Herzog nchini Uturuki walilaaniwa, na ilithibitishwa kwamba Herzog, ambaye alikuja Uturuki kama mwakilishi wa umbile nyakuzi la Kiyahudi, ni gaidi ambaye hatofautiani kabisa na gaidi Sharon au gaidi Netanyahu!

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa na Ustadh Musa Beyoglu, aliwakosoa vikali viongozi na watawala wa Umma wa Kiislamu wanaoona kuwa kila aina ya uhusiano na wavamizi hao inajuzu kwa jina la manufaa, na kubainisha kuwa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa hautakombolewa isipokuwa na watu watukufu mithili ya Omar Ibn Al-Khattab, Salahuddin Al-Ayyubi na Khalifa Abdul Hamid wa Pili, ambaye alitoa muhanga wa thamani zaidi kwa ajili ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa.

Kwa neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, Waislamu waliiunga mkono amali ya Istanbul kwa ushiriki mkubwa, na amali hii ikahitimishwa kwa dua na maombi kwa Mwenyezi Mungu (swt) ili aharakishe nusra yake na tamkini kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili itakayoukomboa Msikiti wa Aqsa uliobarikiwa na Ardhi yote Iliyobarikiwa (Palestina).

Wakati wa amali hii ya kisimamo, mabango mbalimbali yaliinuliwa dhidi ya umbile vamizi la Kiyahudi, na washiriki waliimba miito kama vile "Gaidi Herzog toka Uturuki," "Wito wa Herzog ni usaliti kwa Umma," "Jeshi na lichangamke kwenda Al-Aqsa,” “Jeshi la Muhammad na lichangamke kwenda Al-Qudsi Jerusalem,” pamoja na takbira na tahlil.

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#Aqsa_calls_armies

#AqsaCallsArmies

#OrdularAksaya

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu