- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Raisi Mpya wa Somali Ametangaza kuwa Nchi yake ni “Eneo la Vita”
Raisi mpya wa Somalia aliyechaguliwa hivi majuzi Mohamed Abdullah “Farmajo” ametangaza kuwa Somalia kuwa ni Eneo la Vita. Tangazo hilo alilolitoa Alhamisi 5 Aprili, 2017 linakuja muda mfupi baada ya hali ya usalama kuzidi kudorora ambapo hivi majuzi bomu liliripotiwa mji mkuu wa Mogadishu na kuua watu saba. Akiwa amevalia magwanda ya kivita aliwataka wapiganaji wa Alshabab wasalimu amri. “Tunawaambia vijana wapiganaji wa Alshabab, waliochanganywa akili kuwa wana siku sitini (60) za makataa ili kuweka chini silaha zao wanazozitumia kuwaua watu wao na wasalimu amri waje kwetu” alitamka. (Aljazeera)
Mwanzoni mwa Machi, 2017 utawala wa Trump ulichora mpango mpana wa kijeshi ambao ulijumuisha kitengo maalumu cha kijeshi cha kupigana na makundi yaliyojihami ndani ya Somalia. Taasisi maalumu ya Pentagon tayari imetuma mapendekezo ikulu White House ili kuruhusu Kitengo Maalumu cha Kijeshi cha Marekani kuongeza msaada kwa Jeshi la Taifa la Somalia na kulipa Jeshi la Marekani nguvu zaidi ili kuweza kutupa mizinga angani.
Jeshi la Marekani kuingia vitani sio jambo jipya bali ni muendelezo wa mipango iliyowekwa na utawala wa Bush. 4 Disemba, 1992, Raisi wa Marekani George H.W.Bush aliwahutubia wa Marekani, kuwaambia kuwa wanajeshi wa Marekani watatumwa kwenda Somalia. 1993 Marekani ikatangaza kampeni ya kijeshi iliyoitwa Rudisha Matumaini “Restore Hope” ambayo ilijumuisha vikosi vya kimataifa na ambavyo vilijulikana kama Muungano Maalumu wa Kijeshi UNITAF au “United Task Force”. Oparesheni hiyo ilibuniwa baada ya kuondoshwa mamlakani Siad Barre ambaye alikuwa kibaraka wa Marekani na ambaye utawala wake uliwatengea takribani thuluthi mbili za Somalia kwa makampuni ya Mafuta ya Kimarekani ikiwemo Conoco, Chevron na Philips.
Tangu wakati huo Marekani imekuwa ikimakinisha muelekeo wa kisiasa wa taifa hilo kwa kusimamisha viongozi vibaraka ambao wameletea Somalia maangamivu na kupinduliwa mara kwa mara. Kwa miaka sasa Marekani imekuwa ikiwapa wakuu wa makundi zana za kivita ambao kinaya ni kuwa wamekuwa ndani ya serikali zizo hizo. Mfano mzuri ukiwa ni mpango wa Marekani kuigawa Somalia ili iwe maoneo tofauti na kuyashajiisha maeno yaliyo na kawi nyingi kama Juba land kusitisha mizozo na kuwa chini ya maslahi yake. Kwa hiyo si ajabu kuona tamko hilo la Farmajo likitolewa muda mfupi baada ya mipango ya Marekani kuzidisha mashambulizi ya kijeshi Somalia.
Somalia nchi iliyojaa rasilimali asili nyingi imetangazwa na Marekani kama eneo “salama kwa magaidi” ili kupata sababu ya kuweza kuivamia na kufikia maslahi yake ya kichumi. Mafuta yaliyogunduliwa na tawala za Uingereza na Italia; kisha baadaye makampuni ya Ufaransa na Marekani yakaanza kuzozana na makampuni ya Uingereza na Italia ili kumiliki haki ya kibiashara na kufanya tafiti za mafuta. Hayo yote yamepelekea taifa la Somalia kuwa ndio kiwanja cha vita kati ya Ulaya na Marekani ili kupata haki ya kudhibiti utajiri wa mafuta ya Somalia. Ulaya ikiongozwa na Uingereza kuipiga Marekani kupitia kuwaunga mkono makundi ya kivita nchini humo na kuyatumia mataifa vibaraka ikiwemo Kenya, Djibout na Uganda. Marekani nayo ikiwaunga mkono wapiganaji kupitia nchi kama Ethiopia na Sudan. Hiyo ndio asili ya mzozo wa Somalia.
Somalia hivi sasa iko katika janga kubwa la kibinadamu linalosababishwa na muendelezo wa ukame na ukosefu wa chakula cha kutosha kwa miongo kadhaa mpaka sasa. Hivi sasa zaidi ya watu wapatao milioni tano (5) ya wasomali wanahitaji msaada wa dharura ili kuwalinda na ukosefu wa chakula. Huku serikali zilizofeli zikitoa ahadi tupu ikiwemo pamoja na utawala uliopo sasa, Somalia inaendelea kushuhudia maumivu ya mgawanyiko, vita vya kimbari na ukosefu wa chakula cha kutosha. Mashirika ya Kimataifa ya jiitayo mashirika ya Waislamu ikiwemo Muslimu World League, Organization of Islamic Countries pamoja na mashirika ya kimataifa mengine ima hayajaangazia kwa undani zaidi au hawajafanya chochote kuepuka hali hiyo!
Somalia kama ardhi yoyote ile ya Waislamu na nchi ya Kiafrika imejipata kwa muda mrefu ikitawaliwa na mataifa ya kikoloni. Tangu Uingereza ikidhibiti kaskazini-magharibi ya sehemu ya Somalia kwa zaidi ya miaka sabini (70), iliitwa British Somalia. Italia ilidhibiti kusini kwa zaidi ya miaka hamsini (50) na illitwa Italia Somalia na Ufaransa ilidhibiti hii inayoitwa leo Republic of Djibout. Pamoja na nchi jirani, kwa makubaliano na nchi koloni hususan Uingereza walimiliki eneo kubwa la sehemu hiyo. Hivyo basi, Ethiopia ambayo mwanzoni ilijulikana kama Abyssinia iliteka eneo la Ogadin na Kenya nayo ikateka eneo kubwa la ardhi kusini.
Hali hii ya kutamausha itabadilika tu kwa kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa Njia ya Utume. Kusimama kwake kutatua matatizo msingi yanayoikumba Somalia na ulimwengu mzima.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya