Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Majeshi ya Waislamu Ndio Safu ya Mbele ya Ulinzi kwa Ummah

Kila taifa kubwa huwa na mipaka maalumu ambayo haipaswi kuvukwa. Kutokana na hili, mataifa makubwa, hususan mataifa ya kimfumo, huchunga nguvu yao ya kijeshi pamoja na mfumo wao. Mataifa makubwa huchukua hatua ambazo zitalinda, kupanua na kuhakisha mifumo yao inatawala na hutumia nguvu yao ya kijeshi kufikia hili. Hivyo basi dola wakati huo huo hutumia nguvu za kisiasa, kijeshi na kimfumo. Lakini, kwa kuja mfumo wa kirasilimali na kutafakari kwake mambo kupitia uwezekano wa kiakili, majadiliano juu ya mipaka hii maalumu ya dola na mataifa yamekuwa ndio njia ya kivitendo kukabiliana na matishio ya kindani na kinje. Hii ilianza kwa uadui juu ya matukufu, kukiuka kwao na kuendelea kuchafua heshima. Sasa, watu wanashuhudia ukiukaji huu wa matukufu na heshima katika runinga, kana kwamba wanatazama kipindi au filamu. Na mandhari hizi kamwe hazika sisimua jamii ya kimataifa au jamii maarufu kunyosha kidole, isipokuwa kwa kiwango tu kinacho hitajika kutia shinikizo juu yao, maji yanapozidi unga. Sio kuzusha kusema kuwa njia mpya ya Kimagharibi ya kutafakari kupitia uwezekano wa kiakili ni njia duni zaidi ya tafakari kwa wanadamu. Huuwa uwezo wa akili kuhukumu uhalisia na kuchukua hatua sahihi, imara, hususan katika wakati ambapo ni lazima kutenda kwa haraka na kwa kukatikiwa.   

Ummah wa Kiislamu ndio taifa pekee katika historia lililoipa akili ya mwanadamu haki yake inayostahiki na kuheshimu matukufu ya mataifa, kiasi ya kuwa ulikuwa ni mfano wa kuigwa, katika historia ya kale na ya hivi sasa. Mifano ya historia hii ya Kiislamu iko mingi.

Mfano mmoja ni namna RasulAllah (saw) alivyo amiliana na Maquraysh juu ya Mkataba wa kusitisha mapigano wa Hudaybiyah, pindi Maquraysh walipokiuka mojawapo ya vipengee vya amani kwa kuwapa washirika wake Bani Bakr silaha na kuwasaidia kwa pesa na watu katika vita vyao dhidi ya washirika wa Mtume (saw), Bani Khuza’a. Mojawapo ya masharti ya Mkataba wa kusitisha vita wa Hudaybiyah ilikuwa makabila pambizoni mwa Makkah yalikuwa na uhuru wa kuchagua kujiunga katika mkataba kwa kuhifadhiwa ima na RasulAllah (saw) au Maquraysh. Bani Khuza’a walichagua kuingia katika mkataba wa RasulAllah (saw) na ahadi yake, na Bani Bakr wakachagua Maquraysh na ahadi yao. Kwa hivyo, habari ilienea kuwa watu katika Bani Bakr waliwashambulia Bani Khuza’a na Maquraysh wakawasaidia Bani Bakr. Kufuatia hilo, Amr ibn Salim Al Khuzaa, kiongozi wa Khuza’a, alikuja kwa RasulAllah (saw) kumuarifu kuhusu shambulizi la khiyana la Bani Bakr, kwa usaidizi wa Maquraysh, katika khiyana hiyo, iliyokiuka sharti la vipengee vya Mkataba wa kusitisha vita wa Hudaybiyah. Alikuja Madina na kusimama mbele ya Mtume wa Allah (saw) katika Masjid An-Nabawy na kumuomba msaada, akisema,      

يا رب إني ناشد محمدا                      حلف أبينا وأبيه الأتلدا

هم بيتونا بالوَتير هُجَّدا                       وقتلونا ركعـاً وسجـدا

“Ewe Mola, hakika mimi namuomba Muhammad

Kwa mkataba wa baba yetu na babake, unaokirimiwa

Wametushambulia kwa ghafla

Na wakatuuwa tukiwa katika rukuu na sujudi”

Ukiukaji huu wa wazi wa mkataba wa kusitisha vita pamoja na RasulAllah (saw) wa Maquraysh, ulitosha kwa RasulAllah (saw), kama kiongozi wa kihakika wa jeshi pamoja na kiongozi wa kimfumo na wa kisiasa, kutoa jeshi la Waislamu. Zaidi ya hayo, utoaji huu jeshi sio tu wa kuwapa afueni Khuza’a na kuitisha “msamaha” kutokana na khiyana hiyo, bali ni kuvunja ngome za Maquraysh na kuifungua Makkah. Na hii ni wakati ambapo Makkah ilikuwa miongoni mwa makabila ya Kiarabu katika Bara Arabu mithili ya Washington ilivyo sasa.

Mfano mwengine unaoashiria kutolegeza msimamo kwa Waislamu inaposhambuliwa hadhi yao, ni tukio la Bani Qaynuqa’. Yahudi mmoja kutoka kabila la Bani Qaynuqa’ alifichua uchi wa mwanamke wa Kiislamu. Muislamu mmoja akamuona sokoni humo na kumuua kwa heshima ya mwanamke huyo mmoja wa Kiislamu. Kisha, Mayahudi wengi walikuwako sokoni humo, wakampa shahada kwa kumuua Muislamu huyo na mambo yakachacha. Pindi habari hizi zilipomfikia Mtume (saw), pasi na kusitasita aliamuru kutoka kwa majeshi. Hili halikuwa tu kwenda kukusanya pesa za umwagaji damu (diyah) ya Muislamu yule aliyeuliwa au kuitisha msamaha kwa ajili ya mwanamke yule aliyedhulumiwa, bali ilikuwa kulizingira kabila lile, baada ya yeye (saw) kuamuru kufurushwa kwao.

Ama kuhusu kesi ya Bani Quraydhah, ambapo hukmu ya Sa’ad ibn Muadh (ra) ilikuwa si nyengine isipokuwa ni hukmu iliyojengwa juu ya maadili ya Kiislamu, na ilikuwa sawia na utukufu wa damu ya Muislamu na heshima yake.

Alihukumu kuuliwa kwa wanaume wao na kuchukuliwa matekwa kwa wanawake na watoto wao. Hii haikuwa ni hukmu kutoka kwa mtu aliyekuwa na kisasi cha kale dhidi ya Mayahudi hawa. Hukmu yake ilikuwa sambamba na mafundisho msingi ya Uislamu mtukufu, kiasi ya kuwa Wahyi uliridhia hukmu hiyo, kwa Hadith ya Rasulullah (saw),

«لَقَدْ حَكَمْتَ فِيهِمْ بِحُكْمِ اللَّهِ مِنْ فَوْقِ سَبْعِ سَمَوَاتٍ»

“Hakika umehukumu kwa hukmu ya Allah aliye juu Mbingu ya Saba.”

Mifano mitukufu ya kulinda mipaka maalumu katika historia ya Waislamu iko mingi. Wakati huo, Ummah na majeshi yake walibeba misimamo imara iliyo hitaji vita dhidi vya mara kwa mara, kuanzia vita kwa walioritadi ili kuilinda Itikadi ya Kiislamu, hadi ufunguzi wa ardhi, mithili ya Ufunguzi wa Amouriah kutokana na mwito wa mmoja wa wanawake katika wafungwa wa kike wa Roma miongoni mwa Waislamu huru, na ufunguzi wa Sindh kwa sababu ya haramia mmoja aliyeivamia meli ya Waislamu katika bahari wazi na kadhalika. Lakini, huo ulikuwa wakati ambao Waislamu walikuwa na umbile la kisiasa na kiongozi wa umbile hilo alikuwa wa kisiasa, kijeshi na kimfumo. Kwa hivyo huu ulikuwa wakati ambao mfumo wa Kiislamu ulikuwa ndio muongozo wa Ummah huu na dola yake, na hukmu za kisheria za Kiislamu zilikuwa zikitekelezwa juu ya uhalisia, zilizoitisha kuwepo kwa misimamo imara

Hakika, kukosekana kwa Uislamu katika usimamizi wa Ummah na ule wa Itikadi ya Kiislamu katika sera ya kijeshi ya majeshi ya Waislamu, pamoja na kubadilishwa kwa watawala waliobandikwa na Wamagharibi juu ya vichwa vya Waislamu kutawala kwa ukafiri na kwa utaifa na uzalendo, Waislamu na majeshi yao hawanyoshi kidole kulinda matukufu ya Waislamu. Hii ndio hali ilivyo Palestina, Kashmir, Syria na sasa Burma au nyuma ilivyo kuwa Bosnia-Herzegovina miongoni mwa kwengineko. Lau muda wote huu, Ummah ungekuwa na kiongozi kama Mtume (saw), au Khalifah kama Abu Bakr (ra), Umar (ra) na Mu’tasim (ra), kamwe hawangewakubalia Mayahudi, isipokuwa watawaliwe kwa Sheria ya Allah, kama ilivyo elezwa katika Hadith ya Mtume wa Allah (saw),   

«تُقَاتِلُونَ الْيَهُودَ حَتَّى يَخْتَبِيَ أَحَدُهُمْ وَرَاءَ الْحَجَرِ فَيَقُولُ يَا عَبْدَ اللَّهِ هَذَا يَهُودِيٌّ وَرَائِي فَاقْتُلْهُ»

“Mutawauwa (yaani Waislamu) Mayahudi hadi mmoja wao atajificha nyuma ya jiwe, jiwe hilo litasema (kwa kuwasaliti), ‘Ewe mja wa Allah Yahudi huyu hapa nyuma yangu; muuwe.’”

Na kwa Mabudha kamwe hawangekubali chochote kwao isipokuwa hilo. Hawangekubali kutoka kwa Amerika, isipokuwa yale ambayo Mtume (saw) aliwakubalia Maquraysh wakati wa Ufunguzi wa Makkah.

Na hawangekubali kutoka kwa Warusi isipokuwa yale ambayo Sa’ad ibn Muadh aliyahukumu kwa kabila la Bani Quraydhah na Ufunguzi wa Moscow … na kukubali yoyote mengine yasokuwa haya yanapingwa na Uislamu kama aibu, fedheha na kuipa kipaumbele akili, ambayo yote haya yanagongana na Uislamu. Allah (swt) asema, 

وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ

“...Na izza iko kwa Allah, na kwa Mtume wake, na kwa waumini, lakini wanafiki hawajui.”

[Al-Munafiqun: 8]

Imeandikwa kwa Ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 198

Bilal Al-Muhajer – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 18 Aprili 2020 15:49

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu