Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kulaani kwa Maneno na Majibu Dhaifu ya Kijeshi Kutoka kwa Dola ya Pakistan Kunaihamasisha Serikali ya Kihindu Kuwachokoza Waislamu Waliovamiwa Kashmir na Katika Mstari wa Udhibiti

Na: Yahya Malik*

Al-Jazeera imeripoti kwamba wanajeshi watatu wa India waliuawa kwa silaha zilizorushwa kutoka upande wa Kashmir, wakati Pakistan imetangaza kufariki kwa wanajeshi wake wawili na mwengine kujeruhiwa na makombora kutoka India, katika mstari wa udhibiti unaotenganisha pande mbili hizo. (Al-Jazeera Net)

Mstari wa Udhibiti (LoC) unagawanya Kashmir iliyo kombolewa na Kashmir iliyochini ya uvamizi, imekua nukta shinikizo kwa India kihistoria, ambayo Dola ya Pakistan huipatiliza kila inapotaka kuishinikiza India katika bonde la Kashmir lililochini ya uvamizi. Ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano (CFVs) katika mstari wa udhibiti kawaida huwa unaanziswa na Dola ya Pakistan, kama njia ya kujaribu kutoa msaada kwa upinzani wa kujihami eneo la Kashmir. Baada ya kuzindua Vita dhidi ya Ugaidi, serikali ya Pakistan ilitelekeza usaidizi kwa upinzani wa kujihami, ikaweka upya makubaliano ya kusitisha vita katika LOC mnamo 2003 na kupeana nafasi kwa serikali ya Kihindiu kuweka mikakati ya kuimarisha uvamizi wao wakimabavu katika maeneo ya Jammu na Kashmir.

Nukta ya kilele katika mapambano kati ya Pakistan na India katika Mstari wa Udhibiti ilikuwa mnamo 29 Septemba 2016, pale India ilipodai kufanya oparasheni katika Mstari wa Udhibiti huku askari wa Kihindi wakipenya mpaka ndani ya upande wa Kashmir unaotawaliwa na Pakistan. Madai ya oparasheni ndani ya Pakistan yalikataliwa haraka na jeshi la Pakistan, ikafuatiwa na shambulizi la kijeshi katika maeneo ya Uri na kuuliwa kwa Mujahid mashuhuri wa Kashmir Burhan Wani. Tangu hapo India imechukua sera za kiuchokozi katika Mstari wa Udhibiti, kila mara ikianzisha CFVs katika eneo hilo. Kupitia kupitisha sera za kiuchokozi katika LoC, serikali ya Kihindu imelenga kubadilisha mikakati na kugeuza hali ya uongozi katika eneo hilo. Malengo ya serikali ya India, kupitia sera za kiuchokozi ni kuishinikiza serikali ya Pakistan iwakane waziwazi wapinzani wa kujihami walio Kashmir, ambapo msaada wowote kwa upinzani wa kujihami katika Kashmir utanasibishwa na tishio la kivita kati ya India na Pakistan vitakavyo anziswa na serikali ya India. Kupitia uhamasisho kutoka kwa serikali ya Marekani, serikali ya India chini ya Modi imetishia kuendelea kwa athari ya vita, ikiwa vikundi vya kijeshi vitasaidiwa na serikali ya Pakistan.

Hii ni kubadilisha kabisa hali iliyoko katika Mstari wa Udhibiti, ambalo kihistoria limefikiriwa kuwa chini ya milki ya serikali ya India, ambayo imetumiwa na Pakistan kuweka shinikizo la kijeshi kwa India katika Kashmir. Kilicho sababisha kugeuka kwa hali ya uongozi katika Mstari wa Udhibiti ni kuweka wazi, kujitenga na kuacha kutumia nguvu za kijeshi kwa Pakistan katika kusaidia makundi ya upinzani wa kujihami na serikali ya Pakistan kukataa kusaidia Waislamu wanao dhulumiwa ndani ya Kashmir kupitia njia za kijeshi.

Kwa kutangaza kuwa Kashmir haina suluhu ya kijeshi, viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan, wameihamasisha serikali ya India kuendelea na sera yake ya kiuchokozi katika Mstari wa Udhibiti. Serikali ya Kihindi wanauhakika kuwa Pakistan hawawezi sababisha majibizano ya kijeshi, hivyo kuamua kukandamiza vikundi vyote vya upinzani wa kijeshi katika eneo la Kashmir. Badala ya kukana mapambano ya kijeshi na Pakistan, India imechua njia za kijeshi na shinikizo kuhakikisha Pakistan inatii ahadi yake ya kutosaidia kikundi chochote cha upinzani wa kujihami eneo la Kashmir. Ingawa Pakistan haijibu kwa kukiukwa makubaliano ya kusitisha vita (CFVs) na India katika eneo la Mstari wa Udhibiti, inavyo fanya serikali ya Pakistan ni kwa lengo la kujilinda, kudumisha heshima ya jeshi ndani ya nchi na kubadilisha lawama kwa India kwa majeruhi yeyote yatakayo tokea kwa sababu ya uchokozi wa India. Tawala zilizopita zimejaribu kuuza sera za kujitenga kwa India juu ya Kashmir iliyovamiwa. Kama sera ya kujivua lawama mbele ya Waislamu walioko Pakistan. Hata hivyo umma unazidi kupinga mbinu hii ya kujidhalilisha mbele ya serikali ya India.

Kuna uchungu na hasira zilizokithiri ndani ya Pakistan kuhusiana na kukaliwa kimabavu kwa Kashmir na serikali ya India. Waislamu walioko Pakistan hawatakubali kabisa kudhibitiwa kwa Kashmir na utawala wa Kihindu, Kashmir inatazamwa kuwa ardhi ya Waislamu na kisheria ni milki ya Waislamu.

Hata hivyo, suala la Kashmir litasuluhishwa kwa njia za kijeshi pekee, ambapo nguvu za kijeshi za Pakistan zitatumiwa kumaliza uvamizi haramu wa India eneo la Kashmir. Njia hii ya kijeshi haiwezekani kupitia muundo ulioko wa serikali ya Pakistan, ambayo imekana waziwazi na kujitenga kwa suluhu ya kijeshi. Nikupitia kurudisha Khilafah pekee kupitia Njia ya Utume ndani ya Pakistan ndio itakayo tekeleza sera za kijeshi katika kuzikomboa ardhi zote za Waislamu, hili litaleta matokeo ya kukombolewa kwa Kashmir kutoka kwa mikono ya serikali ya Kihindu.

فَلَا تَهِنُواْ وَتَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱلسَّلۡمِ وَأَنتُمُ ٱلۡأَعۡلَوۡنَ وَٱللَّهُ مَعَكُمۡ وَلَن يَتِرَكُمۡ أَعۡمَـٰلَكُمۡ

“Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.”  [Muhammad 47:35]

*Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan

*Imeandikwa kwa ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 267

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 18 Aprili 2020 15:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu