Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Vita vya Uchina Dhidi ya Uislamu ndani ya Turkestan Mashariki Vitasitishwa na Khilafah Rashidah---

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni pana ya kufichua ukweli kutokana na mzozo wa Uchina na Waislamu walioko Turkestan Mashariki ambao wanaendelea kupitia kampeni ya mauaji kutoka kwa Uchina tangu 1863. Zaidi ya Waislamu wa Uyghur milioni moja wamefariki ndani ya mashambulizi yaliyotokea mnamo 1949 ambapo utawala wa Kikomunisti wa Uchina ukiongozwa na Mao Zedong ulipochukua hatamu na kupiga marufuku uhuru wa eneo hilo na kuliteka kuwa ni sehemu ya Uchina. Waislamu wa eneo hilo walihamishwa na kutawanywa ndani ya mikoa ya Uchina. Lakini Waislamu wa Uyghur waliokuwa na misimamo hawakujisalimisha kwa Wachina; wakaleta mwamko wa mapinduzi mnamo 1933 na 1944 na mapinduzi yakaendelea ndani ya eneo hilo dhidi ya uvamizi wa Uchina kama ilivyokuwa mnamo 2009.

Uislamu ndio sababu msingi ya chuki ya kudumu kutoka kwa Wachina dhidi ya Waislamu wa Uyghur. Misikiti yao ni miongoni inayolengwa na Uchina katika muendelezo wa sumu yake dhidi ya Uislamu. Ilivunja takribani misikiti elfu 25 mnamo 1949 na takribani misikiti 500 pekee ndio iliyobakishwa ndani ya eneo hilo kubwa. Leo, Uchina imeachana na nusu ya ukomonisti wake katika "uchumi" lakini bado inaendelea kupambana na athari zozote za udini hususan miongoni mwa vijana. Hii ndio sera ya kikweli inayofanyiwa kazi na Uchina ndani ya eneo hilo.

Licha ya yote hayo. nishati ya Waislamu inaendelea  kuwepo ndani ya Turkestan Mashariki ambayo imewezesha kurudi tena kwa athari za Uislamu katika maisha, hususan vijijini. Mtafaruku uliolikumba eneo hilo unaendelea kila wakati mpaka sasa na umelifanya kuwa eneo tofauti na mengine kutokana na ukosefu wa utulivu kwa sababu ya mabomu na vitendo vya vurugu dhidi ya serikali na maamuzi ya kutaka kujitenga. Hatima yake ni imekuwa sehemu dhaifu ndani ya serikali. Kwa kujibu hilo, Uchina inafuatilia kwa makini maisha ya Waislamu wa Uyghur na kuvidhibiti vyombo vya habari kutofuatilia mauaji na kamatakamata inayofanya katika kiza kwa kutumia nguvu ndani ya eneo hilo. Pia inawafuatilia Waislamu wa Uyghur waliotoroka na walio na sauti nje chini ya kisingizio cha "ugaidi" imefaulu kuwashika wengi kupitia njia za kiusalama wa kimataifa hususan kutoka nchi za Asia ya Kati na Pakistan.

Lakutia msumari wa moto ni kuwa dhuluma hizi za Uchina dhidi ya Waislamu wa Uyghur zinafanyika mbele ya macho na masikio ya mamilioni ya Waislamu duniani pasi na wao kushinikiza dhuluma hizi kuondoshwa. Hii ni kwa sababu mamilioni ya Waislamu wametapakaa na hawakuunganishwa pamoja chini ya dola, dola ya Ummah, dola ya Uislamu kukosekana kwa Khilafah ambayo kila Muislamu aliye na uwezo lazima afanye kazi kuirudisha tena na kumtafuta Khalifah, imamu anayesimamia mambo kwa uzuri na mwenye kulinda na kuwa ngao ambayo nyuma yake Waislamu wanapigana, kama ilivyosimuliwa katika Sahih Al-Bukhari kutoka Abu Huraira (ra) aliyesema: Mtume (saw) alisema: «وَإِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imamu ni ngao kutoka nyuma yake munapigana na munajilinda." Na kisha Uchina na wengine hawatojaribu kuwadhuru Waislamu kwa sababu watafahamu kuwa ukandamizaji wao utafuatiwa na malipo maradufu. Hakika Mwenyezi Mungu ana nguvu na muweza.

Ijumaa, Jumada I 1440 AH -25 Januari 2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Februari 2020 16:05

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu