Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bobi Wine: Sura Bandia ya Mfumo Uliofeli

Habari:

Kampala (CNN) - mgombea uraisi wa upinzani wa Uganda Bobi Wine amekamatwa mara ya pili katika mwezi huu, kwa kuchochea maandamano yenye vurugu. Mwanamuziki huyu maarufu aliyegeuka na kuwa mwanasiasa alikamatwa wakati akiwa katika kampeni mashariki mwa Uganda, kulingana na mtu wa karibu wa Wine - imepita wiki tu tangu akamatwe mara ya kwanza. "Gharama ya uhuru ni kubwa lakini ni lazima tuishinde," nukuu ya tweet ilisomeka katika akaunti yake rasmi, ikielezea kukamatwa kwake mnamo siku ya jumatano.

Jeshi la polisi la Uganda halikupokea simu kutoka CNN, lakini katika taarifa iliyotumwa katika wavuti wake rasmi siku ya jumatano, inspekta jenerali ameeleza kuzidisha umakini juu ya maambukizi ya virusi vya Korona wakati wa matukio ya kampeni.

Maoni:

Muelekeo wa vijana wa Uganda: Uchambuzi wa idara mbalimbali kuhusu vijana wa uganda (2011),  umebaini changamoto zinazotokana na ongezeko la idadi ya watu:

Uganda ni nchi iliyo na idadi kubwa ya vijana wachanga zaidi duniani huku zaidi ya asilimia 78 ya watu wapo chini ya miaka 30. Na Chini ya vijana milioni nane wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 15-30, Uganda ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kikubwa cha vijana wasiokuwa na ajira Afrika chini ya  jangwa la Sahara. Ingawa inafanya juhudi katika uchumi, bado inakumbana na changamoto katika kukidhi mahitaji ya vijana wa leo na changamoto zao za kesho ikizingatiwa ongezeko la idadi ya watu inayofikia asilimia 3.2 kwa mwaka.

Rais Yoweri K. Museveni na Chama Chake Tawala cha National Resistant Movement Party (NRM) amekuwa katika madaraka tangu 1986 na kuwa rais pekee aliyekaa madarakani kwa muda mrefu nchini Uganda na katika kanda ya Afrika Mashariki. Pamoja na changamoto za ongezeko la watu, idadi ya vijana kwa wakati huu inafikia zaidi ya asilimia 80.  Idadi ya watu inamfanya Museveni na chama cha NRM kutokuwa na mvuto kwa vijana. Haswa baada ya wengi kutokuwa na ajira na mapato madogo ya mishahara miongoni mwa waajiriwa. Kizza Besigye ambaye alihudumu kama rais wa chama cha kisiasa cha Baraza la Mabadiliko ya Kidemokrasia (FDC) na kuwa mgombea asiyewahi kushinda katika chaguzi za urais za Uganda kuanzia 2001, 2006, 2011, na 2016, akishindwa na  Yoweri Museveni, tangu wakati huo amepoteza ladha ya kugombea tena nafasi hiyo.

Zaidi ya hayo, utawala wa kimabavu na mbinu za jeshi inazotumia kusambaratisha upinzani wowote dhidi ya NRM na utawala wa Museveni, [na hii imekuwa ndio sura ya siasa ya Uganda tangu kuzaliwa kwa Taifa hilo ], imewaweka mbali na kuwatenga vijana katika ushiriki wa kisiasa nchini humo. Bila hata chembe ya shaka, kutokuwa na hamu ya kupiga kura na kutoshiriki matukio ya kidemokrasia itakuwa ni jambo la kawaida  wakati wa uchaguzi wa mwaka 2021, matumaini ya mabadiliko kupitia michakato ya kidemokrasia ni ndoto isiyowezekana. Kyagulanyi Ssentamu [Bobi Wine] mwanamuziki kijana aliyegeukia kuwa mwanasiasa ambaye anatoka katika maisha ya kawaida, ambaye anatambulika na vijana wengi na anatokea katika kabila kubwa la [Baganda], amekuwa mgombea anayefaa kwa ajili ya kufufua mfumo ambao tayari umefeli (urasilimali) ambao ndio haswa uliosababisha mateso na kuwafukarisha watu.

Sura bandia iliyowekwa na ugombea wa kiti cha urais wa Bobi Wine na kampeni zisizo na vurugu na mwito wa kushiriki katika zoezi la uchaguzi kwa wingi inaashiria kwamba baada ya chaguzi tano mtawalia ambazo zote Museveni alishinda. Watu wamekata tamaa ya kukitoa mamlakani chama cha NRM kupitia kura kwa kuwa matokeo yanajulikana. Historia imeonyesha hili nchini Uganda ambapo maraisi wamekuwa wakitolewa nje na kuingizwa ndani ya afisi kwa mtutu wa bunduki, kutokana na hili ni wazi kwamba nchi hii kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ni jambo la kutarajiwa. Kwa Bobi Wine, kuendelea kuwaweka watu ndani ya mabano ya mfumo, kunamfanya awe ni sura mpya bandia ya mfumo ambao tayari umefeli katika kiwango cha ulimwengu.

Mbadala wa Ubepari ni Uislamu huo ndio ukweli kutoka kwa Muumbaji wa mwanadamu, maisha na ulimwengu. Mfumo ambao ulitawala kwa zaidi ya karne kumi na tatu kabla ya kuanguka kwa Khilafah ya Kiuthaman mwaka 1924.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Omar
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 07 Disemba 2020 18:36

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu