Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ndoto za Mchana za Nidhamu ya Kidemokrasia

Habari:

Mnamo siku ya Jumatano tarehe 17/03/2021, John Magufuli (61) aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifariki dunia katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam, na Mama Samia Suluhu Hassan (61) aliyekuwa Makamu wa Raisi aliapishwa kuwa Raisi mpya wa Tanzania Ijumaa ya tarehe 19/03/2021.

Maoni:

Utawala uliopita ulipachikwa sifa na kutukuzwa kutoka kwa baadhi ya watu kiasi cha kufikia hatua ya raisi aliyefariki kuitwa "Shujaa wa Afrika". Lakini mara tu baada ya kifo chake mambo yalijionesha na kuthibitisha kinyume chake, na hili linakazia ukweli kuwa mfumo wa demokrasia na wafuasi wake ni waovu, matapeli na warongo.

Ripoti mpya ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/2020 iliyowasilishwa kwa Raisi Samia tarehe 28/03/2021 inaonesha kuwa, Shirika la ndege la serikali la Air Tanzania (ATCL) limepata hasara ya Tsh bilioni 153.542 katika kipindi cha miaka  mitano iliyopita,  na Tsh bilioni 60 kwa mwaka jana 2019/2020 pekee, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) umeleta hasara ya Tsh bilioni 35, Mamlaka ya Bandari (TPA) imesababisha hasara ya Tsh bilioni 3.7 billion, Halmashauri za Wilaya zimeleta hasara ya Tsh bilioni 18.

Yote haya yanaonesha ubadhirifu mkubwa wa mabilioni ya shilingi unaofanywa na serikali kupitia mikataba na malipo ya kitapeli kama vile zabuni na matumizi haramu kupitia Hazina ya nchi, mambo yaliyofichwa yasijulikane katika utawala uliopita. Serikali iliyokuwa ikijigamba kwamba inapambana na rushwa, inaonesha haikufanya chochote, ilikuwa kama au zaidi ya serikali zilizopita.

Vile vile, katika kipindi cha utawala uliopita, kulikuwa na uwekaji watu vizuizini kiholela na utekaji wa wanasiasa wa upinzani, wanahabari, wafanyabiashara, Waislamu wa kawaida, viongozi wa Waislamu (masheikh). Mfano ni pamoja na kutekwa kwa Abdul Nondo 07/03/2018, Steven Ngowo 19/02/2019, Philbert Gwagilo 2015, Ben Saanane 2017, Mdude Nyangali 06/05/2019, Azory Gwanda 21/11/2017, Salma Said 18/03/2016, Mohammed Dewji 11/11/2018, na kuwekwa kizuizini kiholela kwa Waislamu wengi ikiwa ni pamoja na wanachama watatu wa Hizb ut Tahrir / Tanzania ndani ya mwezi Oktoba mwaka 2017.

Zaidi ya hayo, kulikuwa na ripoti kuhusu mauaji mengi ya kutia shaka na kupotea kwa watu, kwa mfano kuokotwa kwa maiti katika fukwe za Coco (Coco Beach) jijini Dar es Salaam mwaka 2017, mauaji  na kupotea kwa watu wengi katika mkoa wa Pwani (Mkuranga, Kibiti, Rufiji).

Yote haya yanaonesha uovu na uhalisia wa upotofu wa mfumo wa kisiasa wa kidemokrasia ambapo watu hudanganywa kwa kulishwa uwongo na kupachikwa matumaini ya urongo.

Asili ya wanasiasa wote wa kidemokrasia ni kuitumia serikali kujitajirisha wenyewe kutokamana na pesa za Ummah kwa kisingizio cha kuwatumikia wananchi. Wanasiasa hao hawajali kuwajibishwa na watu, wala kuwajibishwa na Mwenyezi Mungu, kwani fikra yao ya kisekula haijali kuhusu muongozo wa Mwenyezi Mungu.

Katika Uislamu, siasa ni usimamizi na uchungaji wa mambo ya watu na ni amana kubwa, ambapo mwanasiasa hufuatiliwa kwa umakini na watu wa kawaida na taasisi imara ya “mahkamatul madhalim”, zaidi ya hayo mwanasiasa atawajibishwa vikali akhera. Hivyo, katika Uislamu, siasa si biashara ya kujinufaisha bali ni jukumu linalopaswa kubebwa kwa khofu na kumuogopa Mwenyezi Munvu (SWT). Ni jambo lenye kutarajiwa chini ya utawala wa Kiislamu (Khilafah Rashidah) vurugu mechi la rushwa na ufisadi halitakuwepo, tofauti kabisa na lilivyoshamiri leo katika mfumo wa kibepari.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu