Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watawala wa Waislamu Wambakisha Hai Bwana wao wa Kimagharibi

(Imetafsiriwa)

Habari:

"Leo, tunatia saini mikataba miwili mipya inayoakisi ushirikiano wetu wa kina juu ya Afghanistan. Ya kwanza yanaiasisi Qatar kama dola ya ulinzi ya Marekani nchini Afghanistan," alisema Blinken.

Qatar itaanzisha makutano ya Marekani ndani ya ubalozi wake nchini Afghanistan ili kutoa huduma fulani za kibalozi na kufuatilia hali ya usalama ya vituo vya kidiplomasia vya Marekani nchini Afghanistan, Blinken alisema. (news.cn)

Maoni:

Kama ilivyo kwa nchi nyingine za Kiislamu, viongozi wa Qatar ni watumishi wa Magharibi na hakuna hata mmoja wao aliye na uhusiano wowote na Uislamu na wala hawana ikhlasi na Waislamu. Kuanzia Syria hadi Afghanistan usaliti wa uongozi wa Qatar kwa Uislamu na Waislamu unadhihirika mchana peupe, walifanya kazi bila kuchoka kutumikia maslahi ya Bwana wao Marekani kwa kucheza dori ya kuzuia mapinduzi ya ikhlasi ya Syria, ili kuisaidia Marekani katika kushinda vita ambavyo ilishindwa dhidi ya Mujahidina jasiri wa Afghanistan kwenye uwanja wa vita kupitia mazungumzo ya mezani.

Kiuhalisia uongozi wa nchi za Kiislamu yaani Pakistan, Iran, Saudi Arabia, Imarati, Qatar nk. hauna mizizi miongoni mwa jamii bali zimeweza kukwamia kiti cha enzi kwa msaada wa serikali za Kimagharibi. Ili kulinda maslahi ya Magharibi, watawala hawa hawavumilii harakati au chama chochote kinachofichua mipango ya makafiri ambayo hatimaye inafichua uhusiano wao na bwana wao wa kikoloni wa Kimagharibi dhidi ya Waislamu na Uislamu. Na watawala hawa wafisadi waliokosa maadili na wenye fikra za kushindwa huruka kwa urefu wowote ile kumsaidia Bwana wao dhidi ya Uislamu. Watawala hawa aghlabu huonekana wakitamka baadhi ya maneno ya Kiislamu ili tu kuudhihirishia Ummah kuwa wako pamoja na Uislamu lakini kiuhalisia watawala hawa wako pamoja na Makafiri.

Sisi kama Umma wa Kiislamu tunatakiwa kuuondoa mfumo huu wa kikoloni wa kidemokrasia wa kirasilimali na kufanya kazi ya kusimamisha mfumo wa Uislamu yaani Khilafah la sivyo watawala hawa vibaraka wafisadi watafanya mambo kuwa mabaya zaidi kwani wanaendelea kumtumikia Bwana wao wa Kimagharibi maadamu mfumo huu ungali katika mamlaka.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohammad Adel

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu