Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Kweli Imran Khan Anajumuisha Harakati Halali ya Kujitolea Muhanga na Yenye Matunda?! 

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Serikali ya Pakistan imempiga marufuku Waziri Mkuu aliyeng’atuliwa mamlakani, Imran Khan, kufanya mkutano mkubwa, uliopangwa kufanyika jijini Islamabad na kuwasaka wafuasi wake katika uvamizi kote nchini, ikiwakamata mamia. Marufuku hiyo ya tarehe 24 Mei 2022 ilikuja saa chache baada ya polisi mmoja kuuawa wakati wa moja ya uvamizi huo, wakati mfuasi mmoja wa kiongozi huyo wa zamani alipofyatua risasi baada ya maafisa kuingia nyumbani kwake jijini Lahore.

Waziri wa Mambo ya Ndani Rana Sanaullah alimuonya Bw Khan kwamba "hataruhusiwa kuvuruga amani jijini Islamabad" na atakamatwa ikiwa itahitajika, endapo mkutano huo utaendelea. Bw. Sanaullah mapema siku hiyo alimtuhumu Bw. Khan kwa kutaka kuleta hali kama ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mapema wiki hii, Bw. Khan aliwataka wafuasi kukusanyika Islamabad mnamo tarehe 25 Mei 2022 kwa ajili ya mkutano mkubwa wa kuishinikiza serikali ya Bw. Sharif. Maandamano hayo, alisema, yataendelea hadi tarehe ya uchaguzi wa haraka itakapotangazwa. (Chanzo: ABC)

Maoni:

Yeyote anayefikiri kwamba Imran anajumuisha harakati halali ya kujitolea muhanga, baada ya kuondolewa kwenye wadhifa wake na sura mpya ya utawala kuchaguliwa mahali pake, amekosea sana. Imran Khan anajua vyema, kwanza kabisa, jinsi watawala wanavyochaguliwa na kuendeshwa na watunga sera halisi nchini, kikundi ndani ya uongozi wa kijeshi. Kisha ndipo wanapoidhinishwa na bwana halisi wa utawala, aliyeketi katika Ikulu ya White House. Imran anajua kwamba mfumo wa demokrasia nchini, kama nchi nyengine za kidemokrasia kote duniani, ni mangati tu ya uhuru wa kumchagua mtawala na katiba.

Hata hivyo, kiuhalisia, demokrasia yenyewe ni sehemu ya mbele ya pote la watu wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa lenye kuwaelekeza wanasiasa, kuwaagiza sera ambazo wanapaswa kuzitekeleza kwa ufasaha. Wanasiasa wanapaswa kuwa na nidhamu katika utekelezaji wao, au watakabiliwa na adhabu au hata kuuawa. Kuna mifano mingi ya hili katika historia ya demokrasia nchini Pakistan pekee. Kuuawa kwa Liaquat Ali Khan, Zulfiqar Ali Bhutto na Benazir Bhutto ni mifano tu inayothibitisha hili. Kwa hivyo, chaguo la kuwakamata au kuwafukuza baadhi ya wawakilishi, mawaziri na mawaziri wakuu waliochaguliwa sio chaguo pekee. Ni miongoni tu mwa machaguo rahisi zaidi, sio chaguo la mwisho kabisa lenye mkanganyiko, kwa kuwa viongozi hawa wa duni wa kisiasa ni wanyenyekevu na watiifu mbele ya pote hilo la ushawishi na mkuu wake halisi, Washington.

Hivi ndivyo watu wengi wanakisia au kushuku, lakini hawana uhakika. Iwapo wangekuwa na uhakika au wangehakikishwa, hawangekubali kunyenyekea chini ya utawala haramu, mtiifu kwa makafiri wakoloni, maadamu utawala huo unaweza kuhudumia maslahi ya Marekani, kabla ya kutupwa, kutumika.

Harakati ya Imran Khan nchini italeta tu maovu kwa watu wa Pakistan. Kwa hakika, pote la watu wenye ushawishi mkuu wa kisiasa lilimwacha Imran huru na hai kwa maslahi yake binafsi. Harakati ya Imran inaupa utawala huo fursa na kisingizio cha kuwakandamiza wapinzani halisi wa utawala huo. Kukamatwa kwa zaidi ya 400 kati yao ni mfano wa hilo, hivyo kumwachilia Imran ni njia ya kufikia lengo. Cha kusikitisha ni kwamba, mapambano duni juu ya madaraka yana gharama kubwa kwa watu kulipa. Ama kuhusu uchaguzi wa mapema, ni unyakuzi mwingine tu wa mamlaka, ambao kwao wananchi hawana faida wala hisa. Utawala na katiba, chanzo cha mateso ya watu, havitabadilika kupitia uchaguzi. Uchaguzi utabadilisha tu sura ya serikali na sura ya pote la watu wenye ushawishi mkuu wa kisiasa.

Hata tukiuchukulia ushindi wa Imran Khan katika uchaguzi, ambao uwezekano wake ni mdogo, basi je, Imran ana dira ya kiitikadi, kisiasa na kiuchumi itakayoitoa nchi katika mgogoro wake?! Jibu ni hapana. Lau Imran angekuwa na maono makubwa, angekuwa tayari ameyatekeleza alipokuwa madarakani. Hata hivyo, Imran amefilisika kama watawala wengine Ruwaybidah (duni) waliomtangulia, pamoja na watawala wote wa duni watakaozaliwa kutoka tumboni mwa pote la watu wenye ushawishi mkuu wa kisiasa la demokrasia katika siku zijazo.

Harakati ya Imran inatumikia utawala wala haiudhuru, au maslahi ya bwana wake kwa vyovyote vile. Zaidi ya hayo, kwa kuuchunga mtaa wa Pakistan kufuata sarabi ya mabadiliko kwa njia ya demokrasia, Imran anaupotoa Ummah kutoka katika harakati ya kuleta mabadiliko ya kweli, kupitia kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, juu ya magofu ya utawala huu uliofeli. Hivyo basi, kwa harakati yake, Imran anawapotoa watu kutoka katika kukomesha hali mbaya ya kiuchumi na kisiasa nchini, ambapo mfumko wa bei na ukosefu wa ajira umeongezeka mno, na ambapo njia yake pekee ya kuepuka ni kuhukumu kwa yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt).

Hivyo basi, wenye ikhlasi wanaoshiriki katika maandamano hayo, pamoja na wengine wengi walio kimya nchini, lazima wadai mabadiliko ya kweli nchini. Wasiruhusu uongozi wowote wa kisiasa, kutoka serikalini au upinzani, kuwahadaa, kwa kuhakikisha uendelezwaji wa mfumo usionufaisha, bali unaleta madhara makubwa. Ni lazima wasikubali kuunguzwa kama kichocheo cha matamanio ya kibinafsi ya wanasiasa wasio na dira kwa ajili ya madaraka. Ama kwa watu wenye ikhlasi wenye nguvu na madaraka, ni lazima wasafishe safu zao za wasaliti na kuupindua uongozi wa kisiasa na kijeshi, na kulifagilia mbali pote la watu wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa na ushawishi wa Kimagharibi kutoka katika nchi yetu. Yote hayo yanaweza tu kufanywa kwa kutoa kwao Nusra yao kwa uongozi wa kisiasa wa mabadiliko ya kweli na ukombozi kutoka kwa ukoloni, Hizb ut Tahrir, ili kusimamisha dola ya utukufu na ushindi, Khilafah kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu