Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali ya Sharif Yaidhinisha Sera zenye Madhara kwa Viwanda

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Hivi majuzi, Benki Kuu ya Pakistan (SBP) ilipandisha viwango vya riba hadi 15% katika hatua ya kuzuia mfumko wa bei. [Newsweekpakistan] Siku chache baadaye serikali ya Pakistan ikapandisha bei ya gesi kwa 335% kwa watumiaji na kushindwa kupunguza bei ya gesi kwa kiasi kikubwa ili kupunguza shinikizo kwa sekta ya viwanda. [Dawn] Mabadiliko haya yakijumuishwa na bei ya juu ya petroli yanaongeza hali ya uchumi wa Pakistan kuwa mbaya zaidi katika siku za usoni. Serikali ya Sharif ilipaswa kuwa rafiki wa kibiashara, lakini inaonekana dawa iliyoagizwa na IMF haijabadilika.

Maoni:

Uchumi wa Pakistani ambao ungali unakabiliwa na mshtuko wa virusi vya korona sasa unakabiliwa na mfumko wa bei uliokithiri kwa sababu ya bei kubwa ya nishati na sarafu duni. Kutia kidonda msumari wa moto, suluhu iliyoainishwa na IMF kwa serikali ya Khan na ambayo sasa imepangiliwa upya kwa serikali za Sharif haionyeshi dalili ya kupungua.

Chini ya agizo la IMF, SBP imepandisha viwango vya riba na serikali imeongeza bei ya gesi na petroli. Zaidi ya hayo, serikali ya Sharif imeahidi kuongeza kodi, ambayo pia inajumuisha ushuru wa mara mmoja wa 10% kwa sekta ya viwanda vikubwa kwa mwaka mmoja ili kukusanya zaidi ya bilioni 400 za Pakistan ($ 1.93 bilioni).

Madhara ya jumla ya hatua hizi yataiumiza tu Pakistan na kuifanya nchi hii kuwa tegemezi milele kwa mipango ya marekebisho ya kimiundo ya IMF (SAPs). Kwa kuongeza viwango vya riba, mikopo inayohitajika kwa viwanda itakuwa ghali na hii itaathiri uzalishaji. Zaidi ya hayo, gharama kubwa za nishati ya kuzalisha na kusafirisha bidhaa zitazifanya bidhaa hizo zisiwe na ushindani katika masoko ya kimataifa. Hatua mithili ya hizo zilizopitishwa na serikali mtawalia tayari zimeangamiza viwanda vya nguo vya nchi hii. Pakistani ambayo awali ilikuwa ni kiongozi wa soko la nguo tayari ameanguka kama India na Bangladesh.

Kadhalika, kuvitoza ushuru viwanda vya Pakistan bila ya kushughulikia tatizo msingi la kuporomoka viwanda ni kichocheo cha maafa. Viwanda vya Pakistan vinahitaji uwekezaji zaidi sio kidogo. Vinahitaji miundombinu ya hali ya juu itakayoviwezesha kushindana ndani na nje ya nchi. Badala yake, wenye viwanda wanatawanya pesa nyingi ili kujenga vituo vyao wenyewe vya kuzalisha umeme kwa nia ya kuhakikisha usambazaji wa umeme bila kukatizwa, na hii inawafanya kuwa na ushindani mdogo.

Vikwazo vingine vya sera za IMF ni pamoja na kupungua zaidi msingi wa viwanda wa Pakistan, ukusanyaji mdogo wa fedha za kigeni na ukosefu mkubwa wa ajira. Ukosefu zaidi wa ajira unamaanisha kodi kidogo na kodi kidogo itasababisha shinikizo la kifedha kwa serikali kukopa kutoka kwa benki za biashara kwa viwango vya juu vya riba. Shukrani kwa IMF, serikali ya Pakistan haiwezi kukopa kutoka kwa SBP ili kuziba nakisi ya fedha.

Inaonekana kwamba msukumo wa sera hizi zote umeundwa ili kuhakikisha kuwa serikali ina fedha za kutosha kulipa mikopo kwa wakopeshaji wa kimataifa kwa viwango vya juu vya riba. Si ajabu basi kwamba wakopeshaji wa kimataifa wanaendelea kuikopesha Pakistan kwa sababu sera za IMF zinadhamini mapato mazuri. Hakuna kufikiria jinsi ya kuiondoa Pakistan kutokana na mikopo ya IMF na uagizaji ghali wa mafuta kutoka nje. Vile vile, hakuna serikali hadi leo iliyoweka mkakati madhubuti wa kuifanya Pakistan ijitegemee.

Kinachotakiwa ni mwelekeo mpya kabisa wa kurekebisha uchumi wa Pakistan na hili linaweza tu kutokea chini ya Khilafah kwa njia ya Utume pekee.

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfaal: 24]

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu