Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mabadiliko Halisi Hayawezi Kutarajiwa Kupitia Uchaguzi Chini ya Demokrasia

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Chama cha Pakistan Tehreek-i-Insaf (PTI) cha Imran Khan mnamo tarehe 17 Julai 2022 kiliipiku PML-N kwa kushinda angalau viti kumi na tano, katika uchaguzi mdogo muhimu. Viti kumi na tano vilikuwa ndani ya viti ishirini vilivyoachwa wazi, baada ya kuondolewa kwa wanachama wa PTI, waliokuwa wamempigia kura Hamza Shehbaz wa PML-N kwa kwa wadhifa wa afisi ya waziri kiongozi wa Punjab.

Maoni:

Makubaliano ya uongozi wa kijeshi wa Pakistan na chama cha upinzani cha PDM, ikiwemo PML-N, yalikuwa ya kutowashinikiza kuondoka madarakani. Makubaliano hayo yalikuwa ya kuwaruhusu kukamilisha muhula wa mabunge ya sasa hadi Agosti 2023. Kuhusu uchaguzi, vyama vya PDM vilitaka taasisi hizo kukaa mbali na uchaguzi. Walikuwa na imani kwamba wanaweza kushinda uchaguzi wao wenyewe. PML-N pamoja na PPP vilipendelea kusimamia wateule wao wenyewe, badala ya kutafuta usimamizi wao kwa taasisi hizo.

Uamuzi wa Mahakama ya Upeo wa kutoruhusu kura za wajumbe waliopinga kuhesabiwa katika uchaguzi wa Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi, ulikuwa wakati taasisi hiyo ilipokuwa ikijitayarisha kwa uchaguzi wa mapema. Hata hivyo, IMF ilipinga uchaguzi wa mapema. Mahakama ya Upeo kisha ikajaribu kudhibiti matokeo ya uamuzi wake. PML-N ilikuwa na imani kwamba itashinda uchaguzi mdogo. Kwa hivyo ilikubaliana na mpangilio wa Mahakama ya Upeo kutatua mgogoro wa Punjab, mkoa mkubwa zaidi wa Pakistan.

Ushindi wa PTI ni matokeo ya raia kukasirishwa na sera zilizoamrishwa na IMF zinazotabikishwa na serikali ya PDM. Mgogoro wa kiuchumi na mfumko wa bei unaotokana nao uliathiri sana wapiga kura wa Punjab. PML-N, katika juhudi zake za kuiondoa serikali ya Imran Khan iliahidi tikiti za uchaguzi kwa wagombea ambao hawakuwa maarufu sana katika maeneo bunge yao. Hili liliwakasirisha baadhi ya wateule ambao waliondoka PML-N na kujiunga na PTI na kushinda uchaguzi kwa kiti cha PTI.

Haya ni matokeo ya kushangaza kwa PDM na taasisi. Taasisi hiyo haikuitelekeza PDM. Kwa kweli ilikaa mbali na uchaguzi kama PDM ilivyodai, na ilishangazwa na matokeo. Lakini, kukaa mbali kwa taasisi hiyo na uchaguzi kutaondoa shinikizo kwa Jenerali Bajwa kutoka ndani ya safu na faili ya jeshi. Safu na faili zilitaka Jenerali Bajwa kutumia mamlaka yake kuiondoa serikali ya PDM na kuitisha uchaguzi wa mapema.

Baada ya matokeo ya uchaguzi, vyama vya PDM havitataka uchaguzi wa mapema, hasa wakati athari kubwa ya mfumko wa bei bado inaonekana kwa raia. Imran Khan atashinikiza kufanyika kwa uchaguzi wa mapema akihisi anaweza kushinda idadi ya wengi. Muda utasema sasa jinsi uongozi wa kijeshi utakavyofanya.

Hakuna mabadiliko ya maana yanayotarajiwa katika sera kutokana na ushindi wa PTI katika uchaguzi wa Punjab. Ikiwa PTI itaunda serikali huko Punjab na haiwezi kulazimisha uchaguzi wa mapema, italazimika kufanya kazi ndani ya vikwazo vya bajeti vilivyoidhinishwa na IMF. Uchaguzi huu na siasa za sasa nchini Pakistan si chochote zaidi ya mvutano wa madaraka kati ya taasisi inayoongozwa na Jenerali Bajwa, Imran Khan na vyama vya PDM. Hakuna chochote kizuri kinachotarajiwa kutoka kwake. Uchaguzi chini ya Demokrasia utawarudisha tu wanasiasa waliofeli kutawala na sera zile zile za zamani zilizofeli. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayomaliza mzunguko huu mchafu wa uchaguzi, ambao hutumika tu kuwarudisha tena wanasiasa, waliokataliwa na raia miezi michache iliyopita.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Moez – Wilayah Pakista

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu