Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jinsi Vita Vilivyoshindwa vya Amerika Dhidi ya ‘‘Ugaidi’’ Vingali Vinawatoa Kafara Watu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Thomas West, Mwakilishi Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika kwa Afghanistan, katika hotuba yake ya hivi majuzi katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS) alisema: "Kwa kweli ninaogopa - na nadhani hii ni itifaki - kwamba tunachokiona sasa ni kusimama kidogo katika miaka 44 ya mzozo na kwamba tunaweza kuona kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika wakati wowote”.

Kando na hayo, Wajumbe Maalumu wa Pakistan na Iran kwa Afghanistan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tajikistan wameeleza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba Afghanistan inageuka kuwa kimbilio salama la ugaidi. Kauli hizi zote zinatolewa wakati ambapo mashambulizi ya kijasusi dhidi ya raia yameongezeka kwa kiasi kikubwa. Afghanistan hivi karibuni imeshuhudia mashambulizi kadhaa mabaya kwenye Misikiti, shule, na kando kando ya barabara katika wiki iliyopita. Moja ya mashambulizi haya mabaya yalitokea ndani ya taasisi ya elimu, na kuacha zaidi ya mashahidi 50 - wengi wao wakiwa wanafunzi wa kike.

Maoni:

Tangu kushindwa kijeshi kwa Marekani na NATO nchini Afghanistan, na kufuatia kubadilishwa kwa utawala wa jamhuri ulioungwa mkono na Magharibi kwa Imarati ya Kiislamu, Marekani imetumia sera mbalimbali dhidi ya Imarati ya Kiislamu hadi sasa. Marekani imekuwa ikifanya misheni zake nchini Afghanistan, moja kwa moja au kupitia serikali zake vibaraka za kieneo.

Marekani inaona maslahi yake yako katika ufuatiliaji kamili juu ya Imarati ya Kiislamu na vile vile kuitaka iunganishwe na mfumo wa sasa wa kisekula wa kilimwengu ili kuigeuza Imarati ya Kiislamu hatua kwa hatua kuwa moja ya washirika waliojitolea wa Marekani katika eneo hilo. Marekani inajaribu kuamiliana na Imarati ya Kiislamu kwa msingi wa sera ya "Karoti na Fimbo" ili ikengeuke kutokana na misimamo yake ya Kiislamu.

Sera hiyo inatumika kutia shinikizo la kisiasa, kiuchumi, na mfumo wa thamani kwa Imarati ya Kiislamu; hata hivyo, Marekani na washirika wake wamekuwa wakijaribu kuzidisha shinikizo ardhini kwa kufanya mashambulizi ya kijasusi na milipuko mibaya. Hivyo basi, Marekani na nchi za kieneo zimechukua misimamo ya pamoja dhidi ya Afghanistan, wakiita kama 'Hifadhi Salama ya Ugaidi' na kitovu cha Vita vya wenyewe kwa wenyewe - hivyo ndivyo wanavyoendelea kuitaka Imarati ya Kiislamu kusalimu amri kwa matakwa yao hatari na/au mandhari fiche. Ndio maana mitandao ya kijasusi ya nchi za kieneo inatekeleza mashambulizi ya kigaidi ya kikatili dhidi ya raia wa Afghanistan kwa mujibu wa maagizo ya idara ya kijasusi ya Marekani ambayo yana lenga kuishinikiza Imarati ya Kiislamu na kuwatoa kafara watu wanaodhulumiwa na wasio na ulinzi.

Mbali na mashambulizi ya kijasusi, wakoloni wa Kimagharibi na vibaraka wao wanatumia ‘Nguvu laini’ na hatua za kithaqafa dhidi ya Imarati ya Kiislamu. Haki za binadamu, haki za wanawake, serikali jumuishi, maandamano ya mitaani ya wanawake, kampeni za vyombo vya habari, na shughuli za mashirika ya kiraia ambayo ni mabaki ya uvamizi uliopita na mfumo wa kijamhuri na sehemu ya nguvu laini na za kithaqafa hutumiwa dhidi ya Imarati ya Kiislamu kwa njia iliyo pangiliwa.

Ni vyema kutaja kwamba kampeni ya Magharibi, "Vita dhidi ya Ugaidi", chini ya uongozi wa Marekani ambayo kwa hakika ilikuwa ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu imeona kushindwa. Hata hivyo wanatumia neno ‘ugaidi’ dhidi ya serikali. Mnamo mwaka wa 2001, "Vita dhidi ya Ugaidi" ambavyo kwa kweli vilikuwa ni vita dhidi ya Uislamu wa kisiasa vilitangazwa - vita ambavyo Magharibi ilitaka kuepuka mwamko wa mfumo wa Kiislamu na kuwaangamiza wafuasi wa wazo hili.

 Ama kwa wakati huu, kila serikali inafafanua neno 'ugaidi' kulingana na maslahi yake, kutokea kwa kuwataja maadui zake kama magaidi na wafuasi wa ugaidi. Ingawa, ikiwa mtu atatafuta maana ya neno hili katika Kamusi ya Oxford, atapata ni: "matumizi ya vitendo vya vurugu ili kufikia malengo ya kisiasa". Hiyo ni kusema, dola za Kimagharibi na watawala wasaliti wa eneo hili wanafanya mashambulizi ya kikatili ya kijasusi dhidi ya raia ili kuhakikisha maslahi yao. Kwa hakika, huu ndio ugaidi ambao kwao wameainisha maslahi yao.

Wakati huo huo, Marekani inajaribu kulazimisha matakwa yake maovu kwa Imarati ya Kiislamu huku nchi za kieneo zikikaribisha mandhari kama hizo hatari za kinyama, zikitenda ukatili zaidi kuliko wanyama katika kuwaua watu wasio na hatia ili kuiridhisha Marekani ili kudumisha mamlaka yao na / au kuhakikisha madeni kutoka Benki za Kimataifa na/au IMF.                                                                                                                                                               

Imarati ya Kiislamu lazima itambue kwamba ‘Nguvu’ ni mtihani mkubwa wa Mwenyezi Mungu (swt). Nguvu ni baraka za Mwenyezi Mungu (swt) ambayo inatutaka tuwe wenye kushukuru kwa ajili yake; na tukiichukulia kuwa ni jambo la kawaida, hii itamaanisha, tumepofusha macho yetu juu ya neema za Mwenyezi Mungu (swt). Kushukuru maana yake ni kwamba ni lazima tuitumie ‘Nguvu’ kulingana na kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) ameamuru.

Nguvu isiyo onyesha upinzani na/au ubwana juu ya shinikizo za adui; nguvu isiyo onyesha mamlaka na ushupavu; nguvu isiyo tangaza Mfumo wa Kiislamu (Khilafah) na utabikishaji kamili na wa mara moja wa Uislamu, hii [nguvu] kwa hakika itatupeleka kwenye kukufuru neema na kufeli katika mtihani wa Mwenyezi Mungu (Ibtilaa). Tunapaswa kutambua kwamba sio sisi tunaopeana ‘Nguvu’ na ‘Izza’ bali ni Mwenyezi Mungu (swt). Hivyo tusijigambe wala tusije tukafikiri kwamba kupitia kuchukua nguvu, mtihani wa Mwenyezi Mungu (swt) umefika mwisho, Jihad imekatika na Mwenyezi Mungu (swt) ameridhika kabisa. Kwa hakika 'Nguvu' inatokana na Nusrah (msaada) wa Mwenyezi Mungu (swt), na Atampa amtakaye na ataichukua kutoka kwa amtakaye, ili ibainishe nani anayeshukuru na nani asiyeshukuru, na nani aliye hadaiwa na njama za adui na mapambo ya dunia na nani ambaye hajahadaiwa. Kama alivyosema Suleiman (amani iwe juu yake) kuhusu nguvu zake:

[قَالَ هَذَا مِن فَضْلِ رَبِّي لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيٌّ كَرِيمٌ]

“Akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu.” [An-Naml: 40].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Saifullah Mustanir
Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu