Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Teknolojia Bandia ya Kina chini ya Maadili ya Kiliberali Inaangamiza Maisha ya Maelfu ya Wanawake

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 21 Oktoba 2022 BBC iliripoti juu ya hadithi ya Mwanaharakati wa upingaji maovu Kate Isaacs. Kampeni zake za kuzuia maudhui ya wazi  yanayowafanya wanawake kuwa vyombo burudani na faida zilifikiwa huku video zikitengenezwa kwa kutumia picha yake. Video hizi "za uwongo wa kina" zinaweka uso wake kidijitali juu ya waigizaji wengine ili kuunda hisia potofu kwamba alihatarisha viwango vyake mwenyewe vya maadili. Mbinu hizi hapo awali zilitumika kufedhehesha kisiasa au kwa matumizi ya kejeli kwa watu mashuhuri.

Hata hivyo, ulafi na ugaidi wa wanawake wa kawaida ndio mwelekeo mpya unaojitokeza. Wanaume na mashirika mengine maovu yameelewa nguvu ya mbinu hizi za kulipiza kisasi au kulazimisha kujisalimisha kwani wanawake huhisi kutokuwa na uwezo wa kuchukua hatua yoyote. Tishio liliongezeka wakati anwani za nyumbani pamoja na za kazini za Kate zilipochapishwa chini ya video - mazoezi yanayojulikana kama doxing (uanikaji hadharani taarifa za kibinafsi za mtu).

Amenukuliwa akisema; "Ilikuwa ni ukiukaji - kitambulisho changu kilitumiwa kwa njia ambayo sikuiridhia .... nikawa na wasiwasi kabisa - 'Ni nani anayeijua anwani yangu? Je, aliyefanya hivi ni mtu ninayemjua? Nilikuwa nikifikiria, Niko matatizoni sana hapa, hii sio tu baadhi ya watu kwenye mtandao wanaozungumzia, hakika kuna hatari kubwa."

Maoni:

Upatilizaji matumizi ya teknolojia chini ya maadili huria ya urasilimali unamaanisha kwamba kupata pesa kutokana na kuwadhalilisha wanawake sio uhalifu kabisa. Maumivu ya familia na marafiki kutazama maudhui haya mara nyingi huwaweka wanawake katika maisha ya ukimya na kunyenyekeshwa. Wanawake wengi wamenaswa katika mizunguko ya unyanyasaji na maangamivu ya kifedha wakijaribu kuzuia video kama hizo kuzunguka kwa umma. Uharibifu wa maisha ya kijamii na kitaaluma ya mwanamke ni ncha tu ya barafu. Athari za afya ya akili za kuanikwa waziwazi kabisa kwa unyanyasaji bila udhibiti wowote zimesababisha baadhi ya wanawake kujiua.

Mwanaharakati anayehusika alikuwa mwathiriwa wa mianya ya sasa ya sheria inayohusiana na "kutengeneza na/au kusambaza picha za faradha bila idhini".

Tayari ni kosa nchini Scotland kusambaza picha au video zinazoonyesha mtu mwingine katika hali ya faragha bila idhini yake. Lakini katika maeneo mengine ya Uingereza, ni kosa tu ikiwa inaweza kuthibitishwa kuwa vitendo kama hivyo vilikusudiwa kumsababishia mhasiriwa fedheha. Huu ndio mwanya wa kisheria unaomaanisha kuwa waundaji video mara nyingi hawakabiliwi na mashtaka ya jinai. Kuna watu wanaotengeneza nyenzo zenye uharibifu kama kazi yao kamili. Mtengenezaji mmoja alieleza kwamba kuna pesa za kutosha katika kazi hii kwa yeye kamwe kutoiacha. Amenukuliwa akisema; "Kwa mtazamo wa maadili, sidhani kama kuna kitu ambacho kingenizuia," anasema. "Ikiwa nitapata pesa kutokana na marupurupu nitaifanya, hiyo ni wazi."

Mipango ya serikali ya Uingereza ya Mswada wa Usalama Mtandaoni kote nchini imekuwa chini ya marekebisho mengi na kucheleweshwa mara kwa mara. Sheria hizo mpya zitampa mdhibiti wa mawasiliano, Ofcom, uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya tovuti yoyote inayodhuru watumiaji wa Uingereza, bila kujali mahali walipo duniani. Mapema mwezi huu, hata hivyo, Waziri wa Utamaduni Michelle Donelan alisema yeye na timu yake sasa "wanafanya kazi kwa jitahada za juu kabisa" kuhakikisha mswada huo umewasilishwa.

Hata hivyo, punde tu uwongo wowote wa kina unapochapishwa na kusambazwa mtandaoni, ni vigumu kuuondoa kwenye mzunguko kabisa na uharibifu kwa maisha ya wanawake mara nyingi hauwezi kutenduliwa.

Ukosefu huu wa haraka unaakisi mtazamo wa thaqafa ya Kimagharibi na ni udhalilishaji wa wanawake kama vyombo visivyo na ubinadamu vinavyothaminiwa tu katika upande wa huduma. Thamani ya wanawake kama heshima inayopaswa kuchungwa na kulindwa ni kadhia ya uhai na kifo ambayo haiwezi kuwa na "mwanya" wowote chini ya Khilafah. Viongozi wa waliopita, kama Umar Ibn al Khattab, wangetuma majeshi yote kushughulikia ukiukaji wowote wa usalama wa wanawake. Katika nyakati hizi za utovu mkubwa wa usalama, ni wazi kwamba wanawake wasiokuwa Waislamu wanahitaji Khilafah kama vile wanawake wa Kiislamu wanavyohitaji.

Mtume Muhammad (saw) alikuwa anawasifia sana wanawake wema na wasafi. Alisema:

«الدُّنْيَا كُلُّهَا مَتَاعٌ وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَة الصَّالِحَة»

“Dunia nzima ni starehe, na starehe yake bora ni mwanamke mwema.” Wakati mmoja alimwambia khalifah wa baadaye, 'Umar:

«الَّتي تُطيعُ زوجَها إذا أمرَ، وتسرُّهُ إذا نظرَ، وتحفظُهُ في نفسِها ومالِهِ»

“Mwanamke ambaye anamtii mumewe akimuamrisha, na (mumewe) anafurahika akimtazama, na anajihifadhi nafsi yake na mali ya mumewe kwa ajili ya mumewe.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu