Jumatatu, 06 Rajab 1446 | 2025/01/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wale Wanaotawala na Wanaotaka Kuutawala Ummah Wanatafuta Dhamana ya Mustakbali wao Ubavuni mwa Mabwana zao wa Magharibi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uturuki: Mwenyekiti wa Chama cha Republican People's Party Kemal Kilicdaroglu alikwenda London, mji mkuu wa Uingereza, kufanya msururu wa ziara. Wakati wa ziara yake nchini Uingereza, Kilicdaroglu alikutana na duara na wawekezaji wa sayansi na teknolojia. (Chanzo: Mashirika ya Habari)

Maoni:

Mwenyekiti wa CHP Kilicdaroglu alikuwa ameenda Marekani na alikuwa amekutana na baadhi ya duru huko kabla ya ziara yake nchini Uingereza. Wakati huu, kiongozi wa CHP Kemal Kilicdaroglu alizuru Uingereza pamoja na ujumbe. Alikutana na baadhi ya wawekezaji wa Uingereza.

Katika taarifa yake kuhusu safari hiyo, Kemal Kilicdaroglu alisema lengo la ziara yake nchini Uingereza ni kwamba Uturuki inahitaji uwekezaji safi wa kigeni ili kujikwamua kutoka katika mgogoro, na kwamba ikiwa fedha safi zitakuja, fedha chafu zitatoka, na kwa njia hii, pesa zitashuka kwa watu, kumaliza ukosefu wa ajira na kung'oa dawa za kulevya kutoka mitaani, na kwamba hili ndilo suluhisho pekee kwa mzunguko wa mgogoro. Aidha, Kilicdaroglu alisema kuwa ana mipango mikubwa sana kwa Uturuki na kwamba mwisho wa Novemba unapaswa kutazamwa.

Na pamoja na hayo, Mwenyekiti wa CHP Kilicdaroglu alisema katika ujumbe wake jijini London kwamba alifanya mkutano jijini London na hazina 14 kubwa ambazo zimewekeza pauni bilioni 100 katika sehemu mbalimbali za dunia, kwamba ataleta fedha hizo Uturuki, kwamba zitakuja kwa nguvu mno, kwamba hakukuwa na wachukuzi wa riba kubwa kati ya wale aliokutana nao, kwamba wote walikuwa wawekezaji na kwamba hakuna wafanyibiashara wa dawa za kulevya kabisa.

Haishangazi kwamba Mwenyekiti wa CHP Kilicdaroglu alizuru Uingereza ambayo mnamo Machi 3, 1924, ilivunja Khilafah, dola ya Waislamu ya miaka 1300. Chama cha CHP, chama kilichoanzisha Jamhuri, kimeshikamana na kuandamana bega kwa bega na Waingereza kwa miaka mingi. Uingereza inataka sasa kuiregesha madarakani CHP, ambayo itatimiza kikamilifu maslahi yake ya kisiasa nchini Uturuki na kanda, kama ilivyo fanya hapo awali.

Ziara ya kiongozi wa CHP Kilicdaroglu jijini London ni ziara ya kisiasa zaidi kuliko ya kiuchumi. Kwa sababu uchumi na siasa ni fahamu mbili zisizotengana. Ziara hii huenda inahusiana na uchaguzi ujao wa Rais wa 2023. Ziara hii ni ya kupokea maelekezo kutoka kwa Uingereza, adui mkubwa wa Uislamu na Waislamu, kwenye ramani ya utendakazi kwa Uturuki.

Kwa upande mwingine, kwa hakika haishangazi kwamba Kilicdaroglu anavutiwa na Uingereza inayoharibu mazao na ng'ombe na ni Kafiri wa kibeberu ambaye anawasifu mno na kukaa ndani yao. Watangulizi wa awali wa Kilicdaroglu pia walikuwa wamezaa mapenzi makubwa na upendo kwa Uingereza kwa sababu nguvu ambayo CHP inaitegemea ni Waingereza.

Sio kweli kwa Kilicdaroglu kusema kuwa alikwenda Uingereza kutafuta pesa safi ili kumaliza mgogoro wa kiuchumi nchini Uturuki. CHP haijali kamwe ukweli kwamba watu nchini Uturuki wanaishi katika dhiki ya kiuchumi. Wasiwasi pekee wa Kilicdaroglu ni kuingia madarakani na kutimiza maslahi ya kiwango cha juu ya Waingereza, ambao anawategemea.

Wamiliki wa hazina, ambao Kilicdaroglu anawataja kuwa wasafi, wamenyonya damu ya Waislamu kwa miaka mingi na kuiba mali ya Ummah kama mwizi. Tena, wenye hazina hawa na serikali ya Uingereza iliyo nyuma yao wametulia, kupora na kunyonya mali ya Ummah kama genge. Sasa, bila aibu yoyote au hata haya, Kilicdaroglu anawasifu wafadhili hawa. Anataka kuwatakasa na kuwafanya wasio na hatia. Aidha, kuhusu taarifa za Kilicdaroglu, hizi si za kweli. Hazina hizi kubwa wote ni walanguzi wa dawa za kulevya. Hazina hizi au mashirika haya ni wachukuzi wa riba wa kimataifa wanaowanyonya watu na hawakubali thamani yoyote ya kibinadamu au ya kiakhlaqi ili kuchuma pesa zaidi.

Kuhusu ahadi ambazo Kilicdaroglu alizipata kutoka kwa wamiliki hawa wa hazina kuwekeza Uturuki, wawekezaji hao wa kibepari hawana huruma na mtu yeyote; hawawekezi isipokuwa ikiwa watapokea mara kumi ya kile wanachotoa. Je, Kilicdaroglu alitoa ahadi gani ili kuwavutia wawekezaji hawa nchini Uturuki? Ni ahadi gani alizotoa? Alifanya makubaliano gani? Isitoshe, Kilicdaroglu hana mamlaka yoyote kwa sasa kutimiza matakwa yao!

Enyi Waislamu;

Wale wanaotawala na wanaotaka kuutawala Ummah wanatafuta dhamana ya mustakbali wao ubavuni mwa mabwana zao wa Magharibi. Wanazunguka mabara kwa ajili ya hili. Wanawaomba msaada wanapokuwa na shida. Wanapumzika ndani yao. Wanatafuta heshima na adhama ubavuni mwa Makafiri wa kibeberu. Lakini, heshima na izza ziko kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Waumini pekee.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yilmaz CELIK

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu