Jumapili, 12 Rajab 1446 | 2025/01/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Haitoshi kuwa na Mkuu wa Jeshi ambaye ni Hafidh wa Quran

Mkuu wa Jeshi lazima awe Munafidh (Mtekelezaji) wa Quran

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM), Jenerali Michael Erik Kurilla, alimuita Mkuu wa Majeshi ya Pakistan (COAS), Jenerali Syed Asim Munir, mnamo tarehe 15 Disemba 2022. Mkuu huyo wa CENTCOM alifahamishwa kuhusu "kukabiliana na ugaidi" pamoja na mpaka wa Pakistan na Afghanistan.

Maoni:

Mkuu mpya wa Majeshi aliyeteuliwa, Jenerali Syed Asim Munir, alirithi kujisalimisha kwa Kashmir Iliyokaliwa na India kusikopendwa sana, kama matokeo ya fundisho la Bajwa. Badala ya kuhamasisha wanajeshi wa Pakistan kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa kupitia Jihad, Jenerali Bajwa alifanikisha usitishaji mapigano kwenye Mstari wa Udhibiti (LoC), akisema, "Tunahisi ni wakati sasa wa kuzika yaliyopita na kusonga mbele."

Kuhusu mpaka wa magharibi wa Pakistan, Bajwa alishirikiana katika vita vya Marekani dhidi ya "ugaidi," akiimarisha mpaka na Afghanistan, badala ya kufanya kazi ya kuiunganisha Afghanistan na Pakistan kama dola moja, kama Uislamu unavyodai.

Baada ya kuchukua madaraka, mkuu huyo mpya alisema, "Wacha niweke wazi, vikosi vya jeshi vya Pakistan viko tayari kurudisha vita kwa adui, ikiwa vita vitalazimishwa juu yetu." Hata hivyo, Jenerali Asim hakuzungumza juu ya kuanzisha vita ili kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa kwa mabavu, kama Uislamu unavyotaka. Badala yake, alisema, "Ulimwengu lazima uhakikishe haki na kutoa kile kilichoahidiwa kwa watu wa Kashmiri kulingana na maazimio ya [Umoja wa Mataifa]."

Kuhusu mpaka wa magharibi wa Pakistan na Afghanistan, mkuu huyo mpya wa jeshi alijitolea kupambana na "ugaidi." Kwa hiyo anafuata nyayo za Musharraf, na wale waliokuja baada yake katika kulinda maslahi ya Marekani kwa gharama ya jeshi letu. Kuhusu ziara ya kamanda wa kijeshi wa Marekani, ni uthibitisho kwamba mkuu wa jeshi amejitolea kufanya muungano na Marekani.

Kama sehemu ya kujenga sura yake, imekuzwa kwamba Jenerali Asim ni Hafidh wa Quran Tukufu, kwa sababu Waislamu wa Pakistan wanaupenda Uislamu. Hata hivyo, haitoshi kuwa Hafidh katika wadhifa wa mkuu wa jeshi lenye nguvu zaidi la Waislamu duniani. Kamanda wa kijeshi lazima pia awe Munafidh (Mtekelezaji) wa Quran Tukufu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahina 60:9]. Kinacho hitajika kwa ajili ya utabikishaji ni kumaliza muungano na ushirikiano na Marekani.

Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha,

[وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Maidah 5:45]. Kinacho hitajika kwa ajili ya utabikishaji, ni kumaliza nidhamu ya kikafiri nchini Pakistan, na kuregesha hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt).

Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha,

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni” [Surah Al-Baqarah 2:191]. Kinacho hitajika kwa ajili ya utabikishaji ni kuhamasisha majeshi kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa kwa mabavu.

Chochote kando na hili mambo ni yale yale.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu