Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wametelekezwa lakini Wamenakiliwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

India imepiga marufuku filamu ya wasifu ya BBC kuhusu dori ya Waziri Mkuu Narendra Modi katika ghasia za 2002 katika Jimbo la Gujarat. Filamu hiyo ilionyesha ripoti iliyompata Modi kuhusika moja kwa moja na “mazingira ya kutokujali sheria” yaliyowezesha vurugu hizo. Katika taarifa ambayo BBC iliitoa kufuatia maagizo ya India ya kupiga marufuku filamu hiyo, ilisema kuwa filamu hiyo “ilifanyiwa utafiti wa kina kulingana na viwango vya juu zaidi vya uhariri”. (Al Jazeera.com)

Maoni:

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, pamoja na chuki yake kwa Waislamu, sio tu mtu mwenye nia ovu ya kipekee bali ni fikra iliyobuniwa kwa uangalifu, iliyotekelezwa na inayoendelea ya wakoloni wa Uingereza. Baada ya ghasia za 1857, serikali ya Uingereza ilitambua kwamba kugawanya watu ni muhimu kwa ajili ya uhai wao wenyewe katika eneo hilo, na imani ilikuwa ndio silaha yao waliochagua. Watawala wa Uingereza walipanda mbegu za ghasia za kikabila nchini India kwa kupotosha historia na kukandamiza ukweli wa maelewano matukufu yaliyotekelezwa na watawala wengi wa Kiislamu. Kwa hiyo, mwili mpana ambao ulikuwa ndio makao ya dini zote mbili bila ghasia zozote za kikabila uligeuka kuwa uwanja wa kafara mnamo 1947.

Pakistan na India zilipata uhuru uliosimamiwa na kudhibitiwa mtawalia tarehe 14 na 15 Agosti 1947. Ilizingatiwa kuzaliwa kwa mataifa mawili, ambayo yangestawi na kupiga hatua mara tu yakitengana kutoka kwa kila mmoja kwa kuchora mipaka. Mchakato wote tangu mwanzo hadi mwisho ulikuwa muovu, matokeo yake yalikuwa mataifa mawili yaliyozaliwa mfu, yaliyooza tangu miaka 75 iliyopita. Huenda Magharibi iliondoka ardhini lakini iliendelea na mchezo wake mchafu, ikijua kwamba kwa Waislamu, dini ni sehemu muhimu ambayo inaweza kupigwa kila inapohitajika ili kupata athari zinazohitajika. Katika historia yote wamekaa kimya juu ya kadhia ya Kashmir, kwani kuwa na kadhia hii ni muhimu kumweka hai uadui. India imetumika kama fimbo kwa Pakistan, ikipata uungwaji mkono wote na uhalifu wake wote ulifungiwa macho na UN na mashirika mengine ya kimataifa, kama vile 'Israel' inavyofinikwa na kulindwa ingawa ulimwengu mzima unaweza kuona jinai za kikatili zinazofanywa Kashmir pamoja na Palestina.

Filamu hii ya hivi majuzi haijafichua chochote ambacho kilikuwa hakijulikani kwa Wapakistani na jumuiya ya kimataifa. Modi alitangazwa kuhusika na kupanga na kuwa mshirika katika ghasia za Gujrat za 2002 ambazo zilitokea wakati akiwa waziri mkuu wa jimbo hilo na mauaji yaliyofuata ya maelfu ya Waislamu huko Gujerat, ambayo yanajulikana kama Mauaji ya Gujerat, na ambayo Modi alipata lakabu ya “Mchinjaji wa Gujerat”.

Mtawala wa Kiislamu ndiye mlinzi wa maisha na heshima ya Umma wa Kiislamu. Majeshi ya Kiislamu ni walinzi wa ardhi na maisha ya Waislamu. Pakistan, nchi yenye nguvu za nyuklia, ikiwa na moja ya majeshi yenye nguvu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kukaa karibu na Kashmir na India, ina Waziri Mkuu wake anaye onyesha hamu yake ya uhusiano wa amani na ushirikiano na India na kusuluhisha mizozo iliyoibuka ikiwemo Jammu na Kashmir, huku watu wa Kashmir wakiishi maisha mapya ya kuzingirwa tangu 2019. Hata hivi leo, misikiti inabomolewa, Waislamu wanachomwa moto na wanafurushwa katika maeneo nchini India huku uongozi wetu ukiota ndoto za mafungamano ya kirafiki. Hizi sio fikra za kiongozi au mlinzi. Hizi ni fikra za mfanyibiashara ambaye ana mafungamano yake ya kifedha na kisiasa na makafiri na kubakia hai kwake kuko katika kulinda na kueneza mipango yao. Na hakupaswi kuwe na mkanganyiko katika hili kuwa mwanasiasa wa kiraia tu anafanya. Matendo hayo yote yanasaidiwa na kuungwa mkono na uongozi fisadi wa kijeshi.

Kunusurika kwa Umma wa Kiislamu kuko chini ya kivuli cha Khilafah. Kunusurika huku si lazima tu kwa maisha ya dunia hii bali Akhera yetu inategemea hili. Uislamu kama mfumo hauwezi kutabikishwa kwa kuchanganywa na urasilimali wa kimada. Imani ya Muislamu inaweza kutangazwa kwa kukariri kalima (shahada) lakini ni kama ufunguo katika kuwasha, mafikio yanaweza kufikiwa tu kwa kuendesha gari na kuwa barabarani. Watoto wetu wa Kiislamu hawana haja ya kufanywa nguruwe wa Magharibi, kufanyiwa majaribio na kuandikiwa ripoti kuwahusu. Watoto na ndugu zetu ni “Simba wa Mwenyezi Mungu” ambao hawawezi kubabaishwa na mlio wa sarafu za dhahabu. Masikio yao yanapaswa kuzizoe sauti za panga zenye kupigana. Nguvu za kiakili na kijeshi zinazofungamana na Hukmu za Shariah zitajenga upya Ummah ambao hautalinda tu kile tulichonacho, bali utapata kile ambacho ni cha Mwenyezi Mungu na kimechukuliwa na wafuasi wa Shetani. Baada ya hayo chini ya kivuli cha Khilafah na katika utiifu wa Mwenyezi Mungu (swt), tutaeneza ujumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na pamoja na kuandika historia mpya, kwa hakika tutakiregesha kile kilicho chanwa  na makafiri.

[لاَّ يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاء مِن دُوْنِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللّهِ فِي شَيْءٍ إِلاَّ أَن تَتَّقُواْ مِنْهُمْ تُقَاةً وَيُحَذِّرُكُمُ اللّهُ نَفْسَهُ وَإِلَى اللّهِ الْمَصِيرُ]

“Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.” [3:28]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu