Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jaribio la Kutapatapa la Kundi la BRICS la Ukombozi kutokana na Mfumo wa Kimagharibi Uislamu Pekee ndio Unaweza Kuukomboa Ulimwengu kutokana Utawala wa Magharibi
(Imetafsiriwa)

Habari:

Shirika la Habari la Reuters liliripoti, “JOHANNESBURG, Agosti 24 (Reuters) - Wakati mwanauchumi wa Uingereza alipounda neno fupi la BRIC miongo miwili iliyopita ili kuashiria Brazil, Urusi, India na China, hakuwa akilini mwake na muungano ambao ungejaribu kupinga utawala wa Magharibi katika masuala ya kilimwengu... Katika uamuzi wa kushangaza katika mkutano mmoja wa kilele wa wiki hii jijini Johannesburg, kundi hilo liliialika Saudi Arabia, Iran, Ethiopia, Misri, Argentina na Umoja wa Falme za Kiarabu katika klabu hiyo. Hatua hiyo inalenga kuongeza nguvu ya BRICS kama mabingwa wa kile kinachoitwa Mataifa ya Kusini ya Ulimwengu, ambayo mengi yao yanahisi kutendewa visivyo haki na taasisi za kimataifa zinazoongozwa na Marekani na mataifa mengine tajiri ya Magharibi.”

Maoni:

Watu wengi wa dunia wanatamani kukombolewa kutokana na utawala dhulma wa Magharibi. Utawala wa Magharibi unatabanni ukoloni kama njia ya kulazimisha mamlaka na uwezo wake kwa nchi za Ulimwengu wa Tatu. Nchi hizi zinazoendelea ndizo tajiri zaidi katika upande wa maliasili, lakini, la kushangaza, ni dhaifu zaidi, kwa sababu ya viongozi ambao ni vibaraka wa Magharibi.

Nchi zenye nguvu zaidi kati ya nchi hizi zinazoendelea, ambazo ni sehemu ya nchi za BRICS, zinatamani uhuru kutoka kwa mfumo wa kimataifa wa Magharibi, au ushiriki ndani yake. Wanatamani kujiunga na klabu ya nchi zenye nguvu zaidi za kikoloni duniani. Hii ni ili kuweza kujikinga na madhara ya kumezwa na dola kubwa za kikoloni. Pia wanataka kuvuna baadhi ya yale ambayo dola kubwa zinakamata.

Ama kuhusu nchi zinazounda mhimili wa BRICS, yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, wanajidharau wenyewe. Uchumi wao ni robo ya uchumi wa dunia. Idadi yao ni asilimia arubaini ya idadi ya watu duniani. Ardhi yao inaenea zaidi ya mabara matatu. Hata hivyo, wanakosa dira ya kisiasa ya kuhamasisha uwezo wao kamili, na kujikomboa kutoka kwa utawala wa Magharibi.

Kinachoziunganisha nchi hizi ni kile kilicholeta pamoja mafahali watatu msituni dhidi ya simba, kama inavyosimuliwa katika hadithi ya Kiarabu. Ni ghariza ya kuhifadhi maisha na maslahi ya kimada. Hawakuletwa pamoja na fikra imara ya kimfumo ambayo wanaikumbatia kwa pamoja. Kwa hivyo muungano wao unaweza kuporomoka, ikiwa wahusika watagombana juu ya maslahi makubwa zaidi ya kimada. Hiki ndicho kinachotokea kati ya nchi hizi za BRICS kwa sasa.

Kwa upande mmoja, China na Urusi zinakuja pamoja ili kujilinda kutokana na Marekani inayowalenga. Marekani inajaribu kuwanasa ndani ya kitanzi cha nchi zilizo na uhusiano, au zinazoshirikiana, na Marekani na Magharibi. Hata hivyo, kwa upande mwingine, India, Brazil na Afrika Kusini kwa kweli ni nchi zinazozunguka katika duara karibu na Marekani, kufikia kiwango cha wakala, na hivyo kuunda kitanzi cha Marekani.

Kwa hivyo, haifikiriwi kwamba "muungano" huu utakuwa na uwezo wa kujikomboa kutokana na utawala wa Marekani. Hata kama nchi hizi zilikuja pamoja kwa lengo hili, hakika halitafikiwa na nchi hizo tatu kuu. Hatafikiwa na hata nchi nyengine zinazoendelea zilizopendekezwa kujumuishwa katika mapendekezo ya upanuzi wa BRICS, kwani nyingi ni dola vibaraka wa Marekani, pia. Hatima ya muungano huu ni kufeli kabisa. Kuingia kwa nchi hizi mpya katika kundi hilo ni kukwamisha lengo lake linalotarajiwa. Ni hata kudhibiti na kulinyonya shirika, na watoaji maamuzi katika ulimwengu wa Kimagharibi, haswa Marekani.

BRICS inafanya kazi kwa makubaliano na hilo linawasilisha "kizuizi kikubwa" katika kufanya maamuzi, alisema Jakkie Cilliers, mwanzilishi wa taasisi yenye makao yake makuu mjini Pretoria ya Mafunzo ya Usalama (ISS). "Kwa muda mrefu, maoni yangu ni kwamba kutoepukika kwa uhasimu kati ya China na India pengine ndiyo changamoto kubwa ambayo BRICS itakabiliwa nayo hatimaye," aliiambia AFP.

Kwa kuongeza, kuna udhaifu mkubwa wa upande mkuu wa tatu katika kundi hilo, Urusi. Urusi inaogopa vita kutoka Magharibi. Inatishiwa wa uhai wake ndani ya klabu ya dola za kikoloni zenye nguvu zaidi duniani, ikiwa sio kuwepo kwake. Kuhudhuria kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov, badala ya Putin, sio chochote ila ushahidi wa hofu ya Putin ya kukamatwa. Putin ndiye mlengwa wa hati ya kimataifa ya kukamatwa, kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine. Kwa hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov alitumwa kama mwakilishi wake.

Kuondoka kwa mkoloni wa sasa, mfumo wa kimataifa hakuwezi kufikiwa na dola dhaifu za kitumwa. Dola zinaweza tu kukwepa ikiwa zitaungana kwenye fikra sahihi ya kiitikadi inayokinaisha akili na kuafikiana na umbile (Fitra) la mwanadamu. Ni lazima iweke uadilifu miongoni mwa watu wake na watu wengine duniani. Fikra hiyo pekee ndiyo inaweza kuwa badali ya kihadhara ya itikadi ya kisekula na mfumo wa kibepari.

Itikadi ya kisekula ni fisidifu na inapotosha. Haikinaishi akili na haiafikiani na umbile la ndani (Fitrah). Imezua hali mbaya ya kihadhara na kiroho kote duniani. Imezalisha magonjwa mbalimbali ya kisaikolojia katika jamii za wanadamu.

Mfumo wa kibepari unachochea ulafi wa mali. Ulijilimbikizia mali nyingi sana za ulimwengu mikononi mwa watu wachache wafisadi, huku wanadamu wengi wakiteseka kutokana na umaskini na uchochole.

Hivyo basi, ukombozi kutoka kwa utawala wa mabepari wa kisekula unaweza kupatikana tu kwa kutabanni Dini tukufu ya Uislamu. Hiyo pekee ndiyo imani sahihi na mfumo sahihi unaothibitisha haki, na kubatilisha batili, na kuijaza ardhi uadilifu na nuru. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا]

“Yeye ndiye aliyemtumiliza Mtume Wake kwa uongofu na Dini ya haki, ili apate kuidhihirisha juu ya dini nyengine zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi.” [Surah Al-Fath 48:28].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu